Usafi wa mikono baada ya kutoka haja

Usafi wa mikono baada ya kutoka haja

Wewe waona mavi tu. Niliona mdada wa kazi sehemu kwenye biashara ya chakula anapenga kamasi kwa mkono bila kitambaa halafu anaendelea kusonga ugali bila wasiwasi. Kamasi na kinyesi kipi bora?
Hamna kilicho na afadhali mkuu, au wewe unaonaje?
 
MI NADHANI WEWE UNGEJIITA KIPINDUPINDU,Bora tu uendelee kuwa unaosifika CHINA.Mada nyingine ngumu kwako.
 
Hili ni janga la taifa. Na chimbuko lake ni uarabuni wenyewe wakiita kutawaza. Likaletwa kwetu, watu wa pwani wakalidaka, na sasa limeenea karibu nchi nzima. Kila choo unakuta ina ndoo moja, yenye maji na kopo kwa pembeni. Inatumika masaa 24, huku maji yakiongezwa bila kuoshwa wala kuosha kopo kwa kisingizo eti, hivi ni vifaa vya chooni, lazima viwe vichafu. Na mbaya zaidi hakuna sabuni na sinki la kunawa. Kinyesi hakiondoki kwa kunawa na maji tu, mtu anatoka na uchafu, anashika vitasa na kupeana mikono au kupika. Wanaume tuna nyongeza: unachupuka popote kujisaidia haja ndogo, unashika ''tango'' kwa vidole, (pengine umetoka kutifua), ukisogea mbele unampa mtu mkono kumsalimia, au unanunua mhindi unakata, kumpa mwenzako...
Na bado anakuyekupa kipande cha hindi aliweka kidole mdomoni kutoa mahindi nyuma ya meno na kulamba tena 😂
 
Pressure ya kutosha kabisa.
Huwa zinasafisha vizuri sana kuliko hata maji ya kopo na mkono, sasa sijui changmoto yako iko wapi? Nahisi umezoea kuchamba kwa maji ya kopo na mikono
 
Huwa zinasafisha vizuri sana kuliko hata maji ya kopo na mkono, sasa sijui changmoto yako iko wapi? Nahisi umezoea kuchamba kwa maji ya kopo na mikono
Labda😅. Nitaendelea tu na huu ushamba kwa kweli. Sihitaji kubadilika
 
Usafi wa mpishi ni jambo zito sana, ni uaminifu pia kwa wateja wako, usipokuwa msafi wewe basi jua unawadhuru walaji na biashara yako. Kuna walaji pia hawajali kabisa hata kuwe kuchafu kwa mama lishe au mgahawani jua nao ni shida huko wanapoishi.

Makumbusho niliwahi mwambia mkaanga chips pale hakuwa na na kunijibu 😅😅
Ila pia baadhi mahoteli makubwa kule ndani ukienda unaweza lia kwa mbaali maana 3 or 5 star inafunika funika kidogo 😂
 
Back
Top Bottom