USA vs N.Korea Military Power

Bado unaamini Gaddafi na Saddam = na NK kweli? Mruhusuni USA avurumishe makombora ndio ujue "Style wanayoijua wao" maana yake ni nini. Kumbuka ni nusu karne sasa wanazoza tu.
nkuu mnaongea tu. ila hamjui madhars yake
 
Nimekumbuka enzi za utotoni huko,mikwara kama hii. kweli watanzania mazingira yanafanana. Tunapenda sana kushadadia mambo,hadi tunajipa upande kama vile na sisi ni sehemu ya raia wa hizo nchi.
Wakati mtu mmoja akitoa bastola,kwenye mkusanyiko mnatawanyika wote,achilia mbali washawasha ama mlio wa risasi tu kama upo ndani unaingia uvunguni mwa kitanda.
Tufanye kazi,tuwe wazalendo kwa nchi yetu hatimae ipate nguvu za kiuchumi. Tuiombee dunia amani pawe mahali salama kwa kuishi binadamu.
Kuna unabisha tafakari ya zenji au hapo mkuranga tu.
 
Kitu ambacho hujui ni kuwa uwezo wa Attack Submarine moja ya U.S. ni sawa na 30 za north korea......ni ngumu kufananisha NK & USA kwenye nguvu za kijeshi
kinachowaweka kwenye usawa ni nuklia tu, uchumi hauna nafasi, hoja za kujadili ni je north korea anaweza kurusha nuklia ndani ya u.s.a..?
 
vita sio lelemama atakaeregeza ndio atakae umia unaweza ukawa na vifaa vzuri ila ukiwaiwa utashindwa kujipanga na vifaa vyako vikawa si chochote...
 
Samahani jamani!
Hivi chanzo kikuu cha hili vuguvugu la vita ni nini?

Kwanini hasa wanataka kupigana!!!?
 
Sasa kama NK yupo fiti kama unavyotuaminisha, ebu tueleze imekuwa vipi US kuzipenyeza meli zake za kivita mpaka kuingia kwenye Ras ya NK?
Wao hawana tatizo na Mmarekani alipo, Halafu hawapo kwenye Ras ya NK, Correct "Wapo kwenye rasi ya Korea" ikijumuisha South so hajaingia kwenye ardhi au NK territory as full kama unavyotuaminisha
 
Labda niwawulize. Mlishawahi kuona display ya zana za USA? Hana mbwembwe kama za akina kiduku
Tumeshaona mpka tumechoka, Youtube zipo zimejaa kila nchi inafanya kwenye maadhimisho yake
 
China ndo anaeongoza kwa Uchumi duniani, Mmarekani alipitwa kama sikosei mwaka jana au juzi walitangaza
 
Siyo mkono bro. Kwa upande wa majini N. Korea wapo njiema sana. Na upande wa ground wapo na multiple rocket launcher 2400 wakati USA wapo na 1200.
Unachekesha sana kama upo Kijiwe cha kahawa! USA ni ishu ingine
 
Allies! NK hana allies wa kutosha. USA akiingia vitani uje anao marafiki kadhaa nyumba yake....UK, Canada, South Korea, Japan, Israel, etc
 
Sasa kila siku silaha zinatengenezwa watu wanajiimarisha kijeshi na hawana sehemu ya kuzipeleka, hapo lazima vita itokee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…