US Election Coverage 2008

US Election Coverage 2008

Oh come on now...loosen up! O'Drama is made in jest. There is a local DJ here who goes by the name of DJ Drama and he calls himself Barack O'Drama....don't take things too seriously brethren, okay?

Nyani..thanks for your answer. I was hoping kwamba kwa sababu tumebahatika kuwepo kwenye nchi hii inayothamini demokrasia basi hata tukitofautiana ki-itikadi bado tutaheshimiana (I mean kuheshimu wapinzani wetu). Ninaamini we can remain civil even if we disagree on issues lakini we can live life beyond politics. Ndio maana nikawa nashangaa kwa sababu hizi siasa za kuanza name calling eg "O'Drama" ni za watu ambao hawajakomaa.
Thanks mkuu
 
Ndio maana nawasihi muanze kuwasikiliza Rush Limbaugh, Sean Hannity, Glen Beck, Laura Ingraham, Michelle Malkin, Bill Cunningham, Neal Boortz, Bill O and more mpate dose ya reality. Liberal media ni wachovu wa akili. Hivi Air America bado ipo kweli?

....umeishiwa kweli kweli wewe,all of the people eti Cunningham na stupid michelle Malkin,kwa ajiri ya watu kama hao ndio maana Republican itapigwa landslide kuanzia senate mpaka White house come November,Americans are so smart kuwasikiliza hao wendawazimu.
 
badala ya kuongea issues nyie mmeng'ang'ania hayo mastory ya kizembe!!
Clinton kakamatwa uongo, sasa anataka kutoa droo, kwamba Obama nae hivi sijui vile.......kuhusu Obama na hizo story hakuna jipya ni mavi ya kale!!.
naona tunaenda in cycles tu, hii thread inafikia point sasa inatakakuwa kama zile za kina naniliii(majina kapuni), hamna cha maana zaidi ya udaku, ushabiki na utoto ulovuka mipaka!!!........itabidi kadampinzani, mwk, kubwajinga, mtindiowaubongo na vikaragosi wengine wahamie humu ili tujue moja.


Hope hawajakusikia na mimi sitawaambia kabisa, vinginevyo jiandae kwa mangumi!
 
....umeishiwa kweli kweli wewe,all of the people eti Cunningham na stupid michelle Malkin,kwa ajiri ya watu kama hao ndio maana Republican itapigwa landslide kuanzia senate mpaka White house come November,Americans are so smart kuwasikiliza hao wendawazimu.

Ni kwa ajili ya hao hao ndio maana Ronald Wilson Reagan alishinda mihula miwili na ni kwa ajili ya hao ndio maana George Walker Bush alishinda mihula miwili. Yes, Americans are very smart!!
 
I can't stand Michelle Malkin, I would rather listen to the rest. Hata Savage ni bora, lakini huyu? I usually watch O'Reilly factor na Countdown at the same time lakini siku Ms. Malkin akiwa kwenye kiti cha Bill...ni no no kwangu..I just don't like her period.
 
Nawashauri mwanze kumsikiliza Rush Limbaugh....jamaa kwa kweli anachekesha sana...I mean he is very funny!!

Halafu wale watu waliokuwa wanazimia kwenye mikutano ya Obama mbona siwasikii tena...kulikoni?
 
Ndio maana nawasihi muanze kuwasikiliza Rush Limbaugh, Sean Hannity, Glen Beck, Laura Ingraham, Michelle Malkin, Bill Cunningham, Neal Boortz, Bill O and more mpate dose ya reality. Liberal media ni wachovu wa akili. Hivi Air America bado ipo kweli?

Kwanza kabisa, ina maana Kada, Mwafrika, Mwanakijiji et al ni vikaragosi?

Pili, unaelezeaje Sen. Dodd ku-dispute madai ya Obama?

ndio ni vikarogosi, wao ndio ukaa kubishana kutwa juu ya vitu visivyo mbele wala nyuma....alimradi "kupaushana," kurushiana kebehi, mipasho na uswahili ulokithiri!!! mfano ile thread yenu ilofutwa ya "tumevamiwa" nini cha maana kilikuwa pale???

Dodd ni Irish toka CT, lau kama leo unamwona mtu wa maana ati kwasababu tu ana-qn credibility ya Obama basi safari ndefuu bado unayo!!! Dodd ali-endorse Obama, kwasababu tu shoga zake wakina Uncle Teddy na Kerry walifanya hivyo.....usiamini kila kitu unachosikia!!!
huyo Dodd na Joe Biden, ni watu wa kuangalia sana, kimsingi wao ndio wanawakilisha unafiki kwa definition yake sahihi.
mwisho ni kwamba, support ya Obama hasa toka kwa hao superdelegates(kama Dodd & the like) haipo solid na Clintons wanalijua hilo na ndio maana bado wamo ktk mchuano!!!! THINK & think hard....
kuna battles kemkem zinaendelea ktk democratic party, kuna wale wasiotaka Gov. Dean kuwa DNC chair(clinton supporters na ndio hao wamesababisha chaos in MI na FL), really liberals(obama-maniacs, ready for change and color blind america) against wannabe liberals(some clinton supporters and pple like dodd, bado mzungu ni bab'kubwa, believe in franchise politics na dynasties)....south against north, hivyo basi utaona jinsi mchakato huu ulivyo complicated!!
sasa kuwa makini unaposoma magazeti na kunywa hilo "hannitorade" angalia lisije likakuparia.!!!!
 
ndio ni vikarogosi, wao ndio ukaa kubishana kutwa juu ya vitu visivyo mbele wala nyuma....alimradi "kupaushana," kurushiana kebehi, mipasho na uswahili ulokithiri!!! mfano ile thread yenu ilofutwa ya "tumevamiwa" nini cha maana kilikuwa pale???

Dodd ni Irish toka CT, lau kama leo unamwona mtu wa maana ati kwasababu tu ana-qn credibility ya Obama basi safari ndefuu bado unayo!!! Dodd ali-endorse Obama, kwasababu tu shoga zake wakina Uncle Teddy na Kerry walifanya hivyo.....usiamini kila kitu unachosikia!!!
huyo Dodd na Joe Biden, ni watu wa kuangalia sana, kimsingi wao ndio wanawakilisha unafiki kwa definition yake sahihi.
mwisho ni kwamba, support ya Obama hasa toka kwa hao superdelegates(kama Dodd & the like) haipo solid na Clintons wanalijua hilo na ndio maana bado wamo ktk mchuano!!!! THINK & think hard....
kuna battles kemkem zinaendelea ktk democratic party, kuna wale wasiotaka Gov. Dean kuwa DNC chair(clinton supporters na ndio hao wamesababisha chaos in MI na FL), really liberals(obama-maniacs, ready for change and color blind america) against wannabe liberals(some clinton supporters and pple like dodd, bado mzungu ni bab'kubwa, believe in franchise politics na dynasties)....south against north, hivyo basi utaona jinsi mchakato huu ulivyo complicated!!
sasa kuwa makini unaposoma magazeti na kunywa hilo "hannitorade" angalia lisije likakuparia.!!!!

Na wewe uko ndumilakuwili....wewe Dodd alipon-endorse O'Drama ulichekelea na kusema ni big deal halafu leo unampiga madongo...sasa sijui bora lipi..Hannitorade au Gongo?
 
Na wewe uko ndumilakuwili....wewe Dodd alipon-endorse O'Drama ulichekelea na kusema ni big deal halafu leo unampiga madongo...sasa sijui bora lipi..Hannitorade au Gongo?

yote ni hatari kwa afya yako!!! kama nilishabikia basi ilikuwa siku za mwanzo mwanzo kabla ya kujua baadhi ya fwakts kwa undani..................
hivi mara ya mwisho lini umeona supporter wa HRC ana dispute claim yeyote iliyotolewa na Hillary!??? hata hiyo issue ya Bosnia ni nani ktk watu wake kasema hata ile, "ama kweli pale alikuwa kachemsha"..hakuna, so swali linakuja, je Dodd is for real au mzushi flani tu anaetaka historia isimuhukumu!!??.
 
yote ni hatari kwa afya yako!!! kama nilishabikia basi ilikuwa siku za mwanzo mwanzo kabla ya kujua baadhi ya fwakts kwa undani..................
hivi mara ya mwisho lini umeona supporter wa HRC ana dispute claim yeyote iliyotolewa na Hillary!??? hata hiyo issue ya Bosnia ni nani ktk watu wake kasema hata ile, "ama kweli pale alikuwa kachemsha"..hakuna, so swali linakuja, je Dodd is for real au mzushi flani tu anaetaka historia isimuhukumu!!??.

Kuhusu Dodd nikuulize wewe na endorsee wake Obama...

Halafu sijasikia Obama-maniac yoyote aki dispute claims za kusponsor hizo bill...oooh wait a minute...Obama-maniacs can't even mention a single accomplishment of his...
 
Kuhusu Dodd nikuulize wewe na endorsee wake Obama...

Halafu sijasikia Obama-maniac yoyote aki dispute claims za kusponsor hizo bill...oooh wait a minute...Obama-maniacs can't even mention a single accomplishment of his...

ama kweli mazoea yanatabu........tatizo lako umezoea ku-debate na kina nanilii!!! yaani unarudia yaleyale, nimechoka na umeshinda!.
 
Nyani Ngabu,YNIM,Kitila,jmushi1,

..jamani nimesikia Obama naye anashikwa shati ktk mambo yafuatayo:-

1.kwamba hakuwa Constitutional Law Proffesor.
2.Kwamba amesema amepitisha mswaada, wakati ukweli ni kwamba ame-propose tu na mswaada haukupita
3.Kuna mswaada ambao Chris Dodd anahoji ushiriki na mchango wa Obama.

..naomba clarification na specifics za madai hayo. pia naomba utetezi wa pande zote mbili- for and against Obama. naomba tusiweke ushabiki hapa.

..kwa maoni yangu hii kampeni imekuwa kero na utoto. yaani pande zote mbili zimefuka mipaka ya kampeni chafu. inabidi uwe makini sana kuchambua mchele na pumba.
Uchaguzi wa marekani wa mwaka huu ni unique na waki historia.Ni uchaguzi wa kihistoria kwasababu sasa factor za kutabiri nani anaweza kuwa rais zimeongezeka zaidi ya zile zilizokuwepo kwenye historia ya toka kuzaliwa kwa taifa la marekani!Wanaopenda kujaribu kutabiri masuala kama haya ya wamarekani huwa walikuwa hawapati shida sana kwani historia mara nyingi zimekuwa zikijirudia.This time kuna mmarekani mweusi na pia kuna mwanamke!Kuwepo na tofauti hii kwenye uchaguzi wa marekani mwaka huu kunapelekea mvutano wa hali ya juu kutokana na historia kuingiliana na utamaduni wa mmarekani.Ndio maana nasisitiza ni muhimu kuifahamu historia ya nchi ya marekani kabla ya kuamua kusema nani atashinda.Sheria ya Jim crowe ambayo ilikuwa yenye kuwabagua weusi ilikuwa ni sheria ya kawaida tu hadi mnamo mwaka 1965!Na sheria hiyo ambayo ilikuwa maarufu sana kwenye states level..ililetwa na kuwa federal law na rais ambaye alitokea kwenye chama cha Democracts ambaye aliitukuza sheria hiyo ya jim crowe na kufanya itambulike kitaifa mnamo mwaka 1920.Na kabla ya hapo sheria ilkuwa mbaya zaidi ambayo ni maarufu kama black codes ambazo zilkuwemo kwenye constitution ya marekani.Codes ambazo zilikuwa ni kama mweusi hatambuliki kabisa!Kwa wale waelewa wa mambo..hata kama una miaka 18 bado 1965 kihistoria ni juzi tu!Sasa zile black codes zikafanyiwa marekebisho na kuwa jim crowe!Yani Jim crowe kwao ndio ilikuwa haki kwa mweusi!All great leaders weren't concerned about humani rights..lakini still bado wako revered..so unaweza kuona kwamba wamarekani wa kawaida hawakuona kama hilo ni tatizo kwasababu licha ya kwamba jim crowe law ilikuwa officially abondened bado tu effects zake ziko wazi..American communities are always divided alongside those lines!Sasa hivi linawagusa wamarekani kwasababu mtu yule yule ambaye hawakutaka kumjadili sasa wanalazimishwa kufanya hivyo kwani anataka kwenda kwenye lile jumba jeupe ambalo halijawahi kukaliwa na mweusi!Je kisaikolojia wamarekani wanaweza kumuondoa Obama kwenye hali ya chini na kumfikiria ama kuimagine him in a oval office?Ni kweli media imejaribu kumpa tafu Obama!Lakini kwa wale wasiojua ni namna walioyokuwa wanataka kujionyesha mbele ya dunia kuwa demokrasia marekani imekomaa!Kwa marekani hii issue ya Obama ni jambo la ajabu sana na hakuna mtu yoyote asiyeijua historia ya marekani ataweza kulifahamu hilo!watabakia tu kusubiri nani kasema nini kwenye news especially pundits!Wamarekani wasiokuwa na elimu hawampi kura Obama kwasabau wao ndio mavictims halisi ambao hawaoni kama watu weusi ni watu wa maana.Halafu kuna wale ambao ndio wenye kumake big numbers of Obama supporters ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu na colleges!Hao sas ndio wenye kumsikiliza Obama na kugundua kuwa anachoongea ni sawa na movement maarufu ya wamarekani iliyoongozwa na Thodore Roosevelt,William H.Taft pamoja na Woodraw Wilson!wao waliongoza movement ambayo ni kama hii ya Obama ila ya kwao ilpewa jina la "PROGREVISM"Kipindi ambacho mabadiliko makubwa ya kiuchumi an kijamii kwenye ngazi zote za local na statewide zilifanyika!Badiliko ambalo lilikuwa baya ni Jim Crowe peke yake...ambapo bado inawatesa wamarekani!Sheria za haki za wanawake..kama vile "women suffrage" ambayo ni sheria iliyowaruhusu wananwake kupiga kura!,haki ya kupiga kura ya siri,haki ya wananchi kumchagua kiongozi(kipindi hicho walikuwa wanateuliwa)Sheria za kuwalinda consumers dhidi ya makampuni makubwa..kama vile sheria za vyakula.Wakati huo zilikuwa hazizingatiwi na watu walikuwa wakila uchafu mwingi!Kwakifupi kipindi hiki ambapo watu wanapoteza nyumba zao na makampuni makubwa kuwa na nguvu zaidi ya wananchi..ndio vilio vilivyoipa nguvu ile movement a late 19th century!Vilio vya sasa vya wananchi vinawiana na ujumbe wa Obama na ndio maana wafananisha kampeni yake na movement!Tatizo ni mweusi..nje ya utamaduni!
Kwa waelewa wa historia ya marekani na namna wananvyopiga kura..utaelewa kuwa uchaguzi wa wakati huu nu mgumu kutabiri kutokana na mchanganyiko wa issue zote hizo!Ila watu wasisahau kuwa hii nchi imekuwa ikiongozwa na idea za kilokole kwa karne nyingi sana!Na vita baridi pamoja na vita dhid ya ukomunisti ndio vilivyofacilitate wadini hao kuwa na influence..wakidai kuwa communisism ni against christianity na value zao wamarekani.Wafuatao waliingia madarakani kwa girini za ulokole huku wakiwa na yao moyoni;(1)Richard Nickson;maarufu kwa kashfa ya watergate pamija na kuipeleka nchi kwenye vita vya vietnam.
(2)Jimmy Carter;Yeye aliingilia policies za Irani na kusababisha Islamic revolution huko iran kipindi ambacho wamarekani walichukuliwa mateka kwenye ubalozi wao huko tehran!
(3)George W Bush na Iraqi..yeye aliwaambia wamarekani anakuja kuisafisha nchi na kurudisha kwa mungu kwani Clinton ameichafua kwa ufuska!Ni wadini hao hao wenye sera mbaya zenye kutaka kuiangamiza dunia ili mwisho wa dunia uwadie!Obama yeye anawawakilisha wale wamarekani waliochoshwa na mwenendo huo ambao sasa wanaanza kuona hauna mpango!Ila kama kawaida ya matajiri wakubwa wazungu watatumia hofu kwa wananchi ili wamwogope Obama..hofu iliyochimbukia kutoka kwenye sera za kibaguzi,udini na patriotism.Kwenda kupiga kura kwasababu mtu either ni mkristo ama mweupe badala ya anachosema ni suala ambalo limekuwa likiziongoza siasa za wamarekani na hivyo kuwaweka viongozi ambao hawajali issue za wananchi..badala yake wanawajali wale(makampuni) waliowachangia fedha nyingi..wananchi wanasahaulika hadi wakati wa uchaguzi tena huku wakingojea kuwatisha kwa either race ama vita dhidi ya magaidi.Na ndio maana Obama anaongoza kwa pesa za kuchangisha na amekataa kabisa pesa za makampuni..badala yake anachukua michango midogomidogo kutoka kwa mamilioni ya wananchi,na kwa hilo amesema atawatumikia wao!
 
jmushi1,

..ni vigumu sana kuwa-label wamarekani ktk kundi fulani. nimeona umeongelea ulokole na kuunganisha na Jimmy Carter,na George Bush.

..ningependa pia uwazungumzie John Kennedy,Ronald Reagan,George Bush, na Bill Clinton.

..mimi nafikiri mara nyingi Wamarekani huchagua Raisi ambaye wanaamini atarekebisha matatizo ya predessor wake.

..Jimmy Carter alichaguliwa kurudisha dhima ya serikali baada ya uhuni wa Richard Nixon.

..Ronald Reagan alichaguliwa ili kurudisha hadhi ya Wamarekani ktk duru za kimataifa baada ya kudhalilishwa kule Iran.

..Bill Clinton pamoja na udhaifu wake ktk masuala ya ngono, alichaguliwa ili kurekebisha matatizo ya uchumi yaliyoanzia kwa Reagan mpaka kwa George Bush.

..kuna jamaa yangu aliniambia Bill Cosby is not the most talented Black comedian. lakini kilichomfanya afanikiwe ni kuweza kujiuza kwa white audience.

..Obama naye kama anataka kufanikiwa kuwa Raisi itabidi ajenge imani ya watu weupe kwake. alianza vizuri, lakini haya madudu ya Pastor wake ni kama speed bumps.

..Mgombea mweusi anapaswa kuwahakikishia kwamba anakuja ku-serve Wamarekani wote, na siyo weusi wenzake.

NB:

..katika Marekani ya leo kuna wananchi weupe ambao wana maisha ya shida na hayana tofauti kabisa na ya weusi.

..Weupe masikini hawawezi kumuelewa mgombea mweusi anayejiuza kama civil rights leader.
 
jmushi1,

..Weupe masikini hawawezi kumuelewa mgombea mweusi anayejiuza kama civil rights leader.

Napenda kutofautiana na wewe. Kama utaangalia kwa makini Se. Obama ameji-distance na civil rights movement na kama utakumbuka these leaders are the ones who were accusing Barack of not being black enough..of not supporting civil rights movements and its causes...kama ule ujinga wa Jenna six..do you remember?
Sasa hivi they are moving to his side and they weren't there alipoanza mwanzoni...kwanza they never took him serious. Andrew Young aliwahi kusema wazi wazi kuwa barack shouldn't run for presidency kwa sababu bado ni mdogo? The same guy said "Bill Clinton is every bit as black as Barack. He's probably gone out with more black women than Barack".
I am glad kuwaona watu tofauti kwenye campaign trail ya Barack (kama Sen. McCaskill, gov.Richardson, etc) na sio akina Sharpton, Young, Jesse Jackson,etc.
 
Napenda kutofautiana na wewe. Kama utaangalia kwa makini Se. Obama ameji-distance na civil rights movement na kama utakumbuka these leaders are the ones who were accusing Barack of not being black enough..of not supporting civil rights movements and its causes...kama ule ujinga wa Jenna six..do you remember?
Sasa hivi they are moving to his side and they weren't there alipoanza mwanzoni...kwanza they never took him serious. Andrew Young aliwahi kusema wazi wazi kuwa barack shouldn't run for presidency kwa sababu bado ni mdogo? The same guy said "Bill Clinton is every bit as black as Barack. He's probably gone out with more black women than Barack".
I am glad kuwaona watu tofauti kwenye campaign trail ya Barack (kama Sen. McCaskill, gov.Richardson, etc) na sio akina Sharpton, Young, Jesse Jackson,etc.

nakuunga mkono, ninayo mengi ya kusema lakini muda sina!! upesiupesi tu ni kwamba maelezo ya Jokakuu yapo fraud aidha kwa makusudi au kwa ukosefu wa "ze dataz"(anajisemea FMES).......sina la ziada. Joka, jaribu kwenda deep juu ya candidacy ya Obama!!! he is not running as a black candidate.......

happy friday everybody!!..
 
jmushi1,

..ni vigumu sana kuwa-label wamarekani ktk kundi fulani. nimeona umeongelea ulokole na kuunganisha na Jimmy Carter,na George Bush.

..ningependa pia uwazungumzie John Kennedy,Ronald Reagan,George Bush, na Bill Clinton.

..mimi nafikiri mara nyingi Wamarekani huchagua Raisi ambaye wanaamini atarekebisha matatizo ya predessor wake.

..Jimmy Carter alichaguliwa kurudisha dhima ya serikali baada ya uhuni wa Richard Nixon.

..Ronald Reagan alichaguliwa ili kurudisha hadhi ya Wamarekani ktk duru za kimataifa baada ya kudhalilishwa kule Iran.

..Bill Clinton pamoja na udhaifu wake ktk masuala ya ngono, alichaguliwa ili kurekebisha matatizo ya uchumi yaliyoanzia kwa Reagan mpaka kwa George Bush.

..kuna jamaa yangu aliniambia Bill Cosby is not the most talented Black comedian. lakini kilichomfanya afanikiwe ni kuweza kujiuza kwa white audience.

..Obama naye kama anataka kufanikiwa kuwa Raisi itabidi ajenge imani ya watu weupe kwake. alianza vizuri, lakini haya madudu ya Pastor wake ni kama speed bumps.

..Mgombea mweusi anapaswa kuwahakikishia kwamba anakuja ku-serve Wamarekani wote, na siyo weusi wenzake.

NB:

..katika Marekani ya leo kuna wananchi weupe ambao wana maisha ya shida na hayana tofauti kabisa na ya weusi.

..Weupe masikini hawawezi kumuelewa mgombea mweusi anayejiuza kama civil rights leader.
Nakubaliana na wewe ila kumbuka kwamba Obama anataka kurun kama mmarekani na sio kama kibaraka wa mmarekani mweupe!Kumbuka hotuba yake maarufu ya 2002 ambayo alisema "there's no white america,there's no black america,there's no latino's or asians america..There is the UNITED STATES OF AMERICA!"mabadiliko anayotaka kuyaleta ni watu kupewa nafasi za uongozi based on their characters and qualifications and nothing else!Anataka ashirikiane na wale wote(wazungu,weusi,latino na asians) kuelekea kwenye mabadilko ya kweli..mabadiliko ambayo wamekuwa wakiyalilia kwa muda mrefu.Kumbuka kuwa Martin Luther King aliuawa sio kwasababu alitaka black power..NO!..bali alitaka wote wazungu na weupe waishi kama familia moja na kwa upendo!Maneno kama hayo ya upendo yalisababisha akauawa.Obama anasema kuwa weupe wana resentment na weusi wana anger..na hii ni kutokana na hali halisi ya kihistoria ambayo ndiyo ime ishape jamii ya wamarekani...weupe masikini wakiwa na resntment ya kuona wengi wao bado ni masikini huku kuna weusi(licha ya kwamba ni wachache)wakionekana kupata tumafanikio.na anger ya blacks wanaobaguliwa na masikini ambao pia ni wengi!Bill Cosby yeye ni mchekeshaji tu!Amepata mafanikio kwa kuwachekesha..lakini then huwa anzungumza mambo mabaya kuhusu weusi na hivyo kupendwa na weupe!Agombee urais ndio utagundua sura halisi ya mzungu!Kwani huwaoni wakina 50 cent wakitapanya pesa mbele ya wananwake wenye vichupi kwenye video zao.. wengi wao wakiwa weusi huku jamii zao zikisota na huku wazungu wakiwatajirisha kwa kuwaweka kwenye tv,kunua cd zao! na kuwafanya wawe ndio wawakilishaji wa jamii ya weusi?Ukitaja mtu mweusi marekani tah ha..unapata sura za kina 50 na lil wayne!na nyingine za walioko jela either kwa ubakaji ma ujambazi na drugs!Obama analeta picha ya tofauti kuwa hata mtu mweusi ana uwezo wa kufanya mabo mengine muhimu kwenye jamii ikwemo pia urais!
Umegusia issue ya Reagan.Reagan kama Obama aliraise kwenye occasion..kumbuka alifanikiwa kumuondoa Jimmy Carter kabla hajamalizia kipindi chake cha pili cha urais kwasababu ya issue ya mateka wa iran..na blunder iliyopelekea mapinduzi ya kiislam huko iran!waliamua kuvunja mwiko kama walivyofanya wakati wa Kennedy!Kumchagua mkatoliki kwani walokole wote waliopita(Nixon,na Carter)Waliitumbukiza marekani kwenye majanga ambayo hata wananchi hawakuweza kutabiri!Kipindi hicho ndio wakati ambapo kwa mara ya kwanza kulikuwa na Democrats waliojiunga na Reupublicans na kujiita Reagan Democrats..wakavunja miiko ya chama kwa kuepuka udini,wanachama ambao wako mpaka sasa!Watu walichoshwa..bahati nzuri Reagan sasa alikuwa mweupe huku akitoa speech mithili ya zile za Obama!.Speech zenye kuwaamsha wamarekani na kuwapa matumaini mapya!Jamaa alivunja historia kwa kuzomba kuta nyingi dhdi ya mpinzani wake kwenye historia nzima ya marekani!Ni kam Obama sema yeye ilikuwa laini zaidi kutokana na rangi again!George H.W Bush..yeye alikuwa makamu wa rais kipindi cha Reagan so akashinda kwa urahisi kwasababu ya sifa ya Administration ya Reagan ambaye anapewa sifa ya kuvimaliza vile vita baridi dhidi ya Russia kwa amani,kuliimarisha jeshi la wamarekani na kuwaletea maendeleo makubwa ya kibiashara especially wale matajiri!Bush mkubwa naye alifanya mambo ambayo ni dhahiri yanaonyesha ni kwa kiasi gani marekani imegawanyika huku jamii hii ikiwa haifahamu sio tu historia..bali hata kile kinachoendelea kwenye maisha yao na ya wanajamii wenzao!Almaarufu kama "out of touch"Mithili ya yale mapinduzi ya ufaransa ambapo wananchi wenye njaa wanamuomba malkia walau mkate kwao na watoto wao..malkia aliwajibu kuwa ni kwanini wasile keki?Hii inaonyesha wazi kuwa mbali na njaa iliyokuwa imeigubika ufaransa kipindi hicho..bado watawala wake hawalifahamu hilo..huku wakidhani kuwa kila mtu anakula keki kama wao!Na hii ilitokea live hivi majuzi tu ambapo Bush hana habari kabisa jinsi ambavyo raia wa marekani anavyoteseka na bei ya mafuta pale alipoulizwa kuhusu bei kupanda hadi dola nne!Rais anaweza akaja akasema atashusha kodi kwa wamarekani..lakini wamarekani anaowazungumzia ni wale anaowafahamu yeye..class aliyotokea!Hili tatizo lilimkumba Bush senior aliyekuja na usemi wake maarufu wa "No more tax,read my lips"Akimaanisha kuwa sasa ni wakati wa kuwapunguzia wananchi kodi!Sasa wananchi wanashangazwa mbona hawaoni hayo mapunguzo?Baadae wanakuja kugundua mapunguzo hayo ni kwa matajiri peke yake.Wakamtupilia mbali kabla ya muhula wake wa pili..wakamleta Clinton ambaye naye alikuwa na sifa kama za Obama sema yeye ni mweupe..so ikawa rahisi kurelatem huku akizungumza lugha ya wananchi wa kawaida,na kuahidi kuwa kodi sasa ndio itapinguzwa kwa wamarekani middle class ambao ndio wengi na wenye kuihitaji!kauli ambayo ni maarufu kwa Obama this time around!Baada ya vipindi vyake viwili na matukio kadhaa ya kashfa za Monica pamoja na matatizo ya mashambulio ya kiugaidi..walokole wakaja tena na mpya kwamba ufuska na uliberal ambao umepelekwa mpaka white house ndio unaosababisha matukio haya yote mabaya marekani inayoyapata..Kwamba sasa Mungu amechukia for they just forsaken him!wakafanikiwa kuingiza kahofu kidogo huku wakisaidiwa na sysytem mbovu ya electoral coleges iliyompa Bush ushindi ambao wengi waliamini haukuwa halali!Nguvu kubwa za makampuni makubwa kuwarudisha watawala wao zilifanikishwa na jopo la majaji..na mara baada ya hapo bado marekani ikawa haitawalaki..rais hathubutu kwenda washigton kwani alikuwa akipigwa mayai viza na hali ya hatari na maandamano vikaigubika marekani..bush akaenda zake huko texas huku akifikiri aanzie wapi kwani hakuna mwananchi anayetaka kumuona!Then BOOOM!!more hofu!magaidi wameivamia marekani na sasa wananchi wanansubiri rais wao(ambaye ghafla amekuwa mpendwa)atoe tamko na ni kwanamna gani atawashughulikia magaidi hao!Yaliyotokea ni familia ya Bin Laden kukimbiziwa saudi na kunza kwa vita vya iraqi huku magaidi karibia wote(19)wakiwa wametokea saudi!sasa imagine kama wangekuwa wametokea iraqi!na huko iraqi wanaonufaika ni wenye makampuni ya uuzaji wa silaha kama kina Chenney na makampuni ya mafuta ya kina Bush...pesa zote zinazotolewa na Congress zinarudi mifukoni mwa kina Bush na washirika wake kwa namna moja ama nyingine!Kampuni zote za ulinzi,ujenzi na za mafuta na usafirishaji ni za marekani!viongozi wamewekwa na marekanihadi kazi ya udereva ni ya wamarekani..na pesa wanazolipwa zinatoka kwa wamarekani..so ni kama wanagawana bila kujali kwenye proces maisha ya raia wengi yanpotezwa bila sababu!wamarekani wamechoshwa na uhuni huo na ndio maana wako excited na Obama!Ila tatizo bado linarudi palpale..mweusi!Hivo ni wazi kwamba kusema vita viishe ni kujaribu kukata ulaji wa watu wenye nguvu kubwa duniani ambao wanaweza kukuondoa saa nusu tu kama ilivyokuwa wazi kwa saddam na wengine wengi waliopita kama kina lumumba na Nkrumah!wakina mandela na wengineo!Sitaki kumfananisha saddam na hao viongozi wengine!ila nachozungumzia hapa ni sera!sera ambayzo wamarekani wamechoshwa nazo..ambazo Obama anapromise kuzimaliza!Taitizo?once again unaweza kumalizia mwenyewe!Ndio maana Obama kwenye hotuba zake huwa anapenda sasa kusema.."WE WILL END THE TYRANNY OF OIL ONCE AND FOR ALL".."WE WILL CHANGE THE COUNTRY AND WE WILL CHANGE THE WORLD!Hizo ni baadhi tu ya kauli zake!Anajua kuwa akizibadilisha siasa za marekani..then dunia pia itabadilka!Wananchi ni kweli wamechoshwa..ila wana ubavu wa kupuuzia suala la kuwa Obama ni mweusi?Hilo tunasubiri kuona itakuwaje!
However..kuna wamarekani ambao wako aware kuwa heshima yao mbele ya dunia imeyumba huku supporters wake wengi wakipoteza uongozi wao kwa kumsupport Bush na siasa zake!Wanajua kuwa dunia imeshaanza kuwaangalia kwa jicho la kiaina..at the same time hawataki kuonekana kuwa ni bias..kwamba wanapiga kelele kuhusu demokrasia huku ya kwao ikitakiwa kufanyiwa kazi..watu wengi hawaelewi kuwa mambo kama haya yalianza zamani..kuanzia wakati ule Muhamad Ali alipogoma kwenda Vietnam kwa madai kuwa kuna vita hapo marekani kabla hajaamua kwenda kupigana vile vya nje ya marekani!Vita dhidi ya ubaguzi!Ni wazi kuwa utaona mgawanyiko mkubwa wa kijamii!Kihistoria..majeshi ya weusi(wakati huo walikuwa hawaruhusiwi kuchanganyika na yale ya weupe)ndio walifanikisha kwa kiasi kikubwa kwenye vita ya ukombozi wa ufaransa iliyoongozwa na wamarekani..lakini kwa mshangao mkubwa wa wengi..wanajeshi hao weusi walikatazwa wasishangile wakati wa shamrashamra za kuingia huko Paris kwasababu tu ni weusi na hawastahili heshma ya kibinadamu wala ya kushujaa!
Obama kumtenga mchungaji wake ni kuitenga hali halisi pamoja na historia yenye misukosuko ya marekani kwa ujumla!Mabadiliko anayotaka kuyaleta kusema ukweli yanatisha!Sio tu kwa matajiri wakubwa bali hata watu wa kawaida kama mimi tu!Kwanza kabisa ulinzi anaopatiwa huyu jamaa ni kama ule wa Bush mwenyewe ambaye ni rais!Ulinzi huu hakuuomba yeye!kwanza alikuwa akipuuzia!Lakini mwenyekiti wa kamati ya homeland security ya marekani ndiye aliyemuandikia barua mkuu wa secret services kumuomba kuwa Obama apewe ulinzi unaoendana na hali halisi ya kihistoria ya hapa marekani!Taifa ambalo kuna wakati walikuwa wakivalia rasmi kama vile wanakwenda kwenye party ama kanisani..kumbe wanakwenda kwenye "black lynching"ambapo ilikuwa ni kama sherehe wakati wa usulubishaji msalabani wa watu weusi!Weusi walikuwa wakikamatwa na kusulubishwa hadarani huku watoto,kinamama na waungwana wengine wakihudhuria kama vile ni concert flani hivi ama sherehe!Ilikuwa ni utamaduni wao!hawakuona kwamba ni unyama!Na bado kuna tamaduni nyingine wanazozikumbatia za kibaguzi na kinyama ambazo wao hawaoni kama kuna ubaya wowote!
Obama sasa anakuja na kusema kuwa yeye ndie anaye qualify kuwaleta pamoja weupe na weusi,weusi na latinos!Weusi na latinos nao hawapatani kwani mzungu keshawachonganisha kwa manufaa yake..esp ya kura na kuwaneutralize weusi na kuwasubdue kama sio second minority no more!(madai ya kuwa wazungu wanawaingiza mexicans wengi ili wawazidi weusi na kupoteza nguvu zao kisiasa na kijamii na kuwafanya wawe kundi la mwisho kwa wingi baada ya wazungu!Wazungu matajiri nao wanawaingiza wamexico isivyo halali ili kuwapa mishahara midogo..halafu wanawageukia weusi na kuwaambia kuwa hawa mexicans wamekuja kuchukua kazi zenu!chuki hapo tartiibu hadi ikakomaa!Wengi wao wamebakia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe wakigombea maeneo ya kuuza madawa(territories)na ndio maana Obama alistruggle ilipokuja kwenye kura zao!Uwezo wa kusema lolote kuhusu weupe anao kwasababu ni familia yake!Bibi yake na babu ni wazungu so as mom..na anasema amesikia vilio kutoka pande zote!Mambo mengi wameshindwa kuyatatua kwasababu ya divisions hizo!
Ubaguzi ukiwekwa pembeni..then Obama ndiye anayezungumza the right message at the right time..that also makes him the right person with the right message at the right time!Tatizo ni zile righteousness nyingine..kama vile to be with a right color,right religion and so forth..can he beat the odds?ofcourse it remains to be seen..so far he has proven so with his big coalition!however wamarekani wengi(wazungu)wanaompigia kura ni wale wa mainstream..waliosoma na wanaosoma..ambao wanajua wazi taifa lao linachukua mkondo mbaya na wanataka mabadilio yanayoendana na marekani ya sasa!marekani ya kila mtu(wahamiaji)Hta hivyo wamarekani wenye kukaa maeneo ya shamba..ambao bado pia ni wengi sana..bado ni wabaguzi wa kutisha!Ambao wameshuhudia marais weupe wenye sera za kibaguzi dhidi ya weusi..hivyo kuwapa wao wasiwasi kuwa sasa huyu mweusi naye atawawakilisha weusi hence black power..wengi wao pia wameathirika na sera za kiuchumi za republikan lakini kumpigia kura mweusi haiko kwenye damu kabisa!Kuna ambao piga ua hawawezi kumchagua mweusi!Kutokana na hilo..Simlaumu sana Clinton kwasababu anaijua historia ya nchi yake na ndio maana hataki kudrop out!Anajua jinsi wamarekani walivyokuwa vulnerable!Hataki Democrats waikose white house..wanajua kuwa wananchi wamechoshwa na republikans lakini haina maana kwamba watamchagua mweusi wa democrats!Kwamba hawa wazungu wanajua namna ya kuwatisha wananchi wao na kuwafanya wachague watu wanaowataka!Clinton na vibaraka wake kama kina sullivan wanajua kuwa maslahi yatapotea!Obama amesema atafunga milango yote ya special interest!matajiri na corruption no more in Washington!Anayo support na ulinzi wa kutosha!vitu vitakavyomsadia kuendelea kutoa ujumbe wake bila woga!Ila Clintons wanahisi Democrats wanaweza kuikosa white house kwasababu anajua issue ya kwamba ni mweusi inaweza kumlet down mwishoni!Fukuto kubwa limo ndani ya uongozi wa juu ambao wanasema sasa ni wakati wa siasa mpya kabisa!wanadai ni once in a history event..wakimaanisha kuwa kama Obama akipata urais inawezekana rais mwingine mweusi akajakupatikana baada hata ya karne moja or so!Kwamba akikosa nafasi hii kwasababu ya rangi yake then itakuwa imewarudisha nyuma sana wamarekani na once again kutia doa siasa za taifa lao na maybe Obama kuanza tena siasa za mika ya 60 za kugombea haki za binadamu!!Na hii ni kama vile wanavyotaka waonekane mbele za macho ya wanaulimwengu!Huku wakijua wazi kuwa atakayeweza kuirudisha heshima ya wamarekani mbele za mamcho ya raia wa kawaida wa ulimwengu huu ni Obama!The problem is ...race and more race!at least to the white house!
 
Capitol Hill,

..unge-quote posting yangu nzima ingethibitisha kwamba tuko pamoja. Obama amejaribu kuwa very inclusive ktk kampeni hii.

..tena watu weupe wa Iowa ndiyo waliowatia imani wazungu wenzao kumuunga mkono Obama.

..tatizo lilianza kampeni zilipofika South Carolina. kile kitendo cha kum-label Bill Clinton kuwa ni racists kilikuwa ni "typical" black american tactic.

..Pamoja na kwamba Obama amejaribu kuji-distance na masuala ya race, lakini kampeni yake ilivamiwa na watu kama Al-Sharpton, Jesse Jackson, wenye mazoea ya kutumbukiza race ktk kila suala wanalokabiliana nalo.

..Pia wako weupe[chris mathews, keith olberman, etc..] ambao kwa kutaka kujionyesha wanam-support Obama, na kwamba "wameendelea" sana, wakaanza kutumia rungu la racism dhidi ya Hillary na Bill Clinton. huwezi kuamini kwamba hata ile campaign ya 3am phone call kuna watu wameamua kui-enteprate on racial lines.

..Sasa race haikuletwa na Obama ktk uchaguzi huu. imeletwa na wapambe wake. kitu kibaya ni kwamba yeye Obama ndiye anayeathirika na hali hiyo.

NB:

..Kitendo cha Obama, mke, na wanawe,kuhudhuria Kanisa linaloongozwa na a radical black preacher nako pia hakumsaidii ktk kampeni yake.

..Kuna wanaodai kwamba Obama alimtumia tu Pastor Wright ili kujijengea uhalali mbele ya weusi wa south chicago. kumbuka Obama ni mzaliwa wa hawaii.
 
..tatizo lilianza kampeni zilipofika South Carolina. kile kitendo cha kum-label Bill Clinton kuwa ni racists kilikuwa ni "typical" black american tactic.

Mkuu unataka kusema Clinton Camp haikucheza foul ya kutumia race, kwamba ni Obama camp waliokurupuka na kuanza kuwaita Clinton Camp "racists"?
Unakumbuka ni maneno gani Fmr. President Clinton aliyasema yaliyoleta hasira kwa African american kule South Carolina? Unakumbuka Pres. Clinton alivyomfananisha Barack na Jesse Jackson...kwa ile comment ya "Jesse won South Carolina because of black voters"...tatizo ni kwamba Camp ya Sen. Clinton iliamua kuanza kwenda negative at all costs baada ya kupoteza Iowa caucus ambako polls na pundits walikuwa wakionyesha kuwa atashinda. Strategy yao ilikuwa ni kumuweka Mrs. Clinton as a "tough" candidate...and how do you get tough? You go nasty on your opponent, you get personal. Ndio maana wakaenda ku-dig zile picha za Obama na "msuli" wake kule Kenya, wakaanza kusambaza e-mails kwamba Obama ni muislamu na kutumia jina lake la kati na kumuhusisha na Palestinian organizations kwamba eti ali raise hela.
Issue ya Rev. Wright ni kweli ni ya kukemea. Lakini tusiwe naive hapa...I know huko unakokaa kuna African Americans au labda umewahi kwenda kwenye makanisa ya African Americans. Wengi wao wana share similar views za kuhusu AMERICA ya leo kwa sababu ya historia ya oppression, na wengi wamekuwa victims wa opression na un-equality na brutality ya law enforcement, mistaken identity na vitu vya namna hiyo. Angalia inner city surbubs..angalia mashule yaliyoko huko, tofauti kabisa na shule zilizoko kwenye surburbs za whites. You need more angalia Katrina.
Now don't get me wrong some of the problems are due to lack of being resposible lakini na Serikali nayo imechangia kwa kiasi fulani kwa sera zake.
 
Back
Top Bottom