Urusi yaituhumu idara ya Ujasusi ya Uingereza MI6 kuunda kikundi cha mauaji kutoka Ukraine dhidi ya viongozi wa Afrika wanaoshirikiana na Russia

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Russia imeituhumu idara ya ujasusi wa nje ya Uingereza ya MI6 kuhusika na mpango wa kuunda kundi la wauaji au "Assassination Squad" ambalo kazi yake kuu itakuwa ni kuharibu miundombinu na kufanya mauaji ya viongozi wa nchi za Afrika ambao watakuwa wakishirikiana na Russia kiuchumi na kidiplomasia.

Shirika la habari la Russia limekariri chanzo cha kuaminika cha kijeshi kuwa Uingereza iliiomba Ukraine iandae kundi hilo la kufanya mauaji au "assassination squad" ambalo litakuwa na watu wapatao 100 ambao kazi yao kuu itakuwa ( kwa maagizo ya nchi za magharibi) kufanya uharibu wa miundombinu na mambo mengine yaani "sabotage" pamoja na kufanya mauaji ya viongozi wa nchi za Afrika ambao wameonyesha misimamo kuhusu kushirikiana na Russia kijeshi, kidiplomasia na kibiashara.

Chanzo hicho cha Tass ambacho inaaminika ni kutoka idara ya ujasusi wa kijeshi ya Russia ya GRU kimesema lengo kuu la operesheni hiyo itakuwa ni kuzuia nchi za Afrika kushirikiana na Russia kwa namna yoyote ile.

Mwezi ulopita Russia iliwakaribisha viongozi kadhaa wa nchi za Afrika mjini St Petersburg ambapo nchi hizo ziliahidi kushirikiana na Russia na pia kuahidiwa na Russia kupata msaada wa ngano bure. Kati ya nchi hizo nchi sita zilitoa tamko la kupinga azimio la Umoja wa Mataifa la kupinga uvamizi wa Russia kwa Ukraine.

Pia kwa muendelezo huo wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Russia kikundi cha askari wa kukodiwa cha Wagner kimekuwa ni sehemu ya majeshi ya nchi za Mali, Burkina Faso, Guinea na sasa Niger katika eneo la Sahara.

Katika mashinikizo yake kwa nchi za Afrika na kuwa kutumia nguvu yake ya pesa nchi za Magharibi zimeweza kuushawishi umoja wa kiuchumi wa nchi za magharibi wa ECOWAS kuhakikisha waunda jeshi la pamoja ambalo litaweza kuivamia nchi ya NIger kwa ajili ya kuirudisha madarakani serikali ilopinduliwa na jeshi ya raisi Mohamed Bazoum.

Wiki chache zilizopita jeshi la Niger likiongozwa na mkuu wa kikosi cha kumlinda raisi Omar Tchieni lilitangaza kufanya mapinduzi na kuondoa katiba ya nchi hiyo kisha baadae kutangaza baraza la mawaziri baadhi yao wakiwemo mawaziri wa zamani katika serikali ya raisi aliepita bwana Mahamoudou Issoufou.

Madai ya Russia juu ya kuundwa kwa kundi la mauaji dhidi ya viongozi wa Afrika ni madai ambayo ni very serious na yanopaswa kuchukuliwa kwa uzito wake hususan katika kipindi hichi ambapo viongozi wengi wa bara hili wamegawanyika juu ya mgogoro wa Russia. ECOWAS ni umoja ambao umekuwa ukipokea fedha nyingi kutoka nchi za magharibi fedha ambazo nyingi huishia mifukoni mwa viongozi hao kwa kufanya vikao visivyoeleweka.

Hivi sasa pia kumetokea mgawanyiko ndani ya ECOWAS juu ya uamuzi wa kuunda jeshi la pamoja ambalo kwa msaada wa nchi za Ufaransa na Marekani wa kutumia vyombo ya satelite na ndege zisizo na rubani litaweza kuivamia Niger kijeshi na huku wakti huohuo NIger ikiwa imepokea msaada wa kijeshi kutoka katika kundi la Wagner, Korea Kaskazini pamoja na nchi za Mali na Burkina Faso ambazo nazo zimeweka tayari majeshi yake kuisaidia Niger.

Mgogoro wa Russia na Ukraine na matukio yanoendelea ya Niger pamoja na madai ya Russia kuhusu kuundwa kwa kundi la mauaji dhidi ya viongozi wa Afrika ni uthibitisho rasmi kwamba sasa hivi bara la Afrika ni uwanja wa mapambano baina ya mataifa makubwa yanogombania rasilimali barani humo na pia ni kipimo cha akili na fikra za viongozi wetu wa kiafrika ambao hivi sasa wapo kwenye mtihani mkubwa.

Kulikuwa na mkutano wa Berlin mwaka 1884 hadi 1885 wa kuligawa bara la Afrika baina ya mataifa ya magharibi uliotishwa na Kansela Bismark lakini sasa hivi hakuna mkutano wa aina hiyo na kila nchi ya Afrika ijitafakari upya.

Mara hii kama ilivyokuwa kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia bara la Afrika limejikuta tena katikati ya viya ya Russia na Ukraine. Bara la Ulaya limeazimia kutoliachia bara la Afrika na uzalishaji wake wa rasilimali kuu na malighafi ambazo zahitajika sana huko Ulaya na Marekani. Halikdhalika Russia na China nao wameazimia kutoliacha bara hili na kulipoteza hivyo kukosa raslimali zake muhimu hususan madini ya Urainium na gesi asilia.

Uchambuzi huu umetumia vyanzo mbalimbali kama shirika la habari la Russia-Tass, Sky news, kijarida cha Spytalk na Bloomberg Surveillance.
 
Hizi tension nyingine bwana, kwahiyo tukianza kushuhudia mfululizo wa viongozi husika kunyakuliwa kwenda mawinguni ni kwamba MI6 washafanya yao.
Dunia sasa hivi ipo kwenye sintofahamu kubwa.

Russia wao wamesema hayo ni wajibu wa waafrika kuyafanyia kazi madai hayo mazito.

Au weye waamini tu taarifa za kijasusi zikitoka Marekani au Ulaya magharibi?
 
Dunia sasa hivi ipo kwenye sintofahamu kubwa.

Russia wao wamesema hayo ni wajibu wa waafrika kuyafanyia kazi madai hayo mazito.
Au weye waamini tu taarifa za kijasusi zikitoka Marekani au Ulaya magharibi?
Hiyo taarifa siyo ya kupuuziwa kabisa. wamefanya vyema kuwa alert hawa viongozi wetu kuchukua tahadhari. Intelijensia inatoka Urusi rasmi unaanzaje kuipuuzia na ni lazima walengwa iwaletee tension on the spot.
 
Putin akili zake hazina tofauti na viongozi wa CCM.Wote Wana propaganda za kitoto.Eti Dr.Slaa na Mdude wana kesi za uhaini.
Yeye Putin ndio anayechochea vurugu Africa kwa kutumia mamluki wake Wagner mercenaries.
Viongozi wa ECOWAS kutuma majeshi Niger, Putin kwa kulinda maslahi yake,anawachimba mikwara.Sasa Kati ya M16 na Putin nani muhuni hapa?
 
Putin akili zake hazina tofauti na viongozi wa CCM.Wote Wana propaganda za kitoto.Eti Dr.Slaa na Mdude wana kesi za uhaini.
Yeye Putin ndio anayechochea vurugu Africa kwa kutumia mamluki wake Wagner mercenaries.
Viongozi wa ECOWAS kutuma majeshi Niger, Putin kwa kulinda maslahi yake,anawachimba mikwara.Sasa Kati ya M16 na Putin nani muhuni hapa?
Wote wahuni ila dhamira ndio tofauti. Putin ana unafuu kuliko washenzi wa West sababu hana tamaa na rasilimali zetu ila lengo lake kuzuia West wasiendelee kufaidika na wizi
 
Hii si kama ile kesi yetu ya wahaini ?

20230618_202517.jpg
 
Putin akili zake hazina tofauti na viongozi wa CCM.Wote Wana propaganda za kitoto.Eti Dr.Slaa na Mdude wana kesi za uhaini.
Yeye Putin ndio anayechochea vurugu Africa kwa kutumia mamluki wake Wagner mercenaries.
Viongozi wa ECOWAS kutuma majeshi Niger, Putin kwa kulinda maslahi yake,anawachimba mikwara.Sasa Kati ya M16 na Putin nani muhuni hapa?
Russia ndio zake. Hata ukombozi wa Afrika alichochea sana na hajataka hata kuvhimba mchanga
 
Wote wahuni ila dhamira ndio tofauti. Putin ana unafuu kuliko washenzi wa West sababu hana tamaa na rasilimali zetu ila lengo lake kuzuia West wasiendelee kufaidika na wizi
Kwa akili ya kawaida ambayo hauhitaji uwe na PhD, Ukraine kipindi hichi yupo vitani na Urusi,anaweza kusumbuka kupeleka wanajeshi nje ya nchi wakati wenyewe wapo kwenye changamoto?
Nakumbuka Ukraine walikuwa na wanajeshi walinda amani nchini DRC ambao walikuwa sehemu ya vikosi vya umoja wa mataifa.Baada ya vita na Urusi kuanza wale wanajeshi walirudishwa Ukraine.Leo Ukraine wapeleke wanajeshi wao nje ?
Putin angetunga uongo mwingine lakini sio huu🤔
 
Back
Top Bottom