Utatuzi wa mgogoro wa Russia na Ukraine kwa njia ya amani ni chaguo pekee

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG31N1584423478.jpg


Wakati mgogoro wa Ukraine ukiendelea kwa mwaka mmoja na nusu sasa, huku nchi za magharibi zinaonekana kuendelea na nia yake ya kuchochea mgogoro huo na kutaka utatuliwe kwa njia ya kijeshi, China na nchi za Afrika zimeonekana kupendelea zaidi mgogoro huo kutatuliwa kwa njia ya amani, hasa kutokana na kuwa njia iliyochaguliwa na nchi za magharibi inaonekana kutokuwa na mafanikio.

Tangu mgogoro wa Russia na Ukraine uanze mwaka mmoja na nusu uliopita, mawasiliano kati ya Russia na nchi za magharibi kimsingi yamekwama. Si nchi za magharibi ambazo ziko tayari kuisikiliza Russia, na Russia pia imekuwa na msimamo mkali haitaki kuzisikiliza nchi za magharibi. Lakini katika kipindi chote cha mgogoro huu Russia imekuwa na mawasiliano ya karibu na China na nchi za Afrika.

Ni ukweli usiofichika kuwa mgogoro wa Ukraine umeziathiri nchi zote duniani kwa namna tofauti. Sekta ya kilimo barani Afrika imeathiriwa sana kutokana na nchi za Afrika kuwa waagizaji wakubwa wa ngano na mbolea kutoka Ukraine na Russia, kwa hiyo kukomeshwa kwa mgogoro huo ni jambo lenye maslahi kwa nchi za Afrika. China pia ikiwa ni nchi jirani ya Russia na mdau mkubwa wa mambo ya usalama ikiwa ni mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kukomesha kwa mgogoro pia jambo la maslahi kwake.

Viongozi kadhaa wa nchi za Afrika wamekutana mara mbili na Rais Vladimir Putin na viongozi wengine waandamizi wa Russia tangu mgogoro uzuke. Kwanza ni mwezi Juni mwaka huu ambapo ujumbe wenye viongozi Afrika Kusini, Misri, Senegal, Congo-Brazzaville, Comoro, Zambia, na Uganda, ambao walitoa pendekezo lenye mambo 10 ili kutatua mgogoro huo. Na pia wamekutana mwezi Julai mwaka huu kwenye mkutano wa kilele kati ya Russia na Afrika. Kwenye mikutano yao viongozi wa nchi za Afrika wameendeleza kuhimiza utatuzi wa amani wa mgogoro huo.

Pendekezo la utatuzi wa amani la nchi za Afrika lilifuatia pendekezo la China lenye mambo 12, ambalo kama ilivyo kwa pendekezo la Afrika, kutokana na nchi za magharibi kuendelea kuona vita inaendelea halijaleta mabadiliko yoyote.

Hali halisi kuhusu mgogoro kati ya Russia na Ukraine inaonesha kuwa mgogoro huu umeleta taabu kwa nchi zote hata nchi za Ulaya, ambako kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta kulikosababishwa na vita hiyo, gharama za maisha zimepata na watu wa huko wanatusema. Lakini kwa kuwa Marekani ndio msimamizi mkubwa wa vita hiyo kwa upande wa nchi za magharibi, nchi za Ulaya zinalazimishwa kukabiliana na machungu ya gharama za maisha ili kutimiza azma ya Marekani.

Mapendekezo ya utatuzi wa amani wa mgogoro kati ya Russia na Ukraine yamevutia ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa, kutokana na kuwa na hamu ya kuona utulivu kati ya Russia na Ukraine, na hatimaye kufanya bei ya mafuta na bei ya nafaka kurudi katika hali ya kawaida. Kwa mantiki ya kawaida hili ni jambo jema. Lakini licha ya ukweli kwamba mapendekezo haya ni muhimu, kutokana na ukweli kwamba yanaweza kutoa changamoto kwa sifa ya Marekani ya kuwa mtatuzi mkuu wa mgogoro huo, yamepuuzwa kwa makusudi na hata kutopewa nafasi na nchi za magharibi. Lakini ukweli umedhihirisha kuwa pendekezo zuri litaendelea kuwa pendekezo zuri, na hatimaye litafuatwa bila kujali limetolewa na nani.
 
Hizi insha mnazoandika hazina umuhimu tena, ulimwengu wa leo hamna taifa linaloruhusiwa kumega ardhi ya jirani kibabe babe, haya yalitendeka karne za zamani wakati dunia bado haikua imechorwa mipaka. Leo hii hata ndugu wanalumbana kisa ardhi, hata Tanzania ni muungano lakini unakuta washiriki wa huo muungano wamekaa mkao wa kushukiana likija suala la ardhi, Mtanganyika ukiingia Zanzibar unataka ardhi, jamaa wanakua wakali sana, japo nyote ni taifa moja, mnaoongea lugha moja tena mnashiriki kila aina ya mila na desturi, hao Wanzazibari ni makabila ya Wahehe, Wasukuma .n.k waliovushwa na Waarabu kipindi cha utumwa, mnashiriki vinasaba kabisa.

Mrusi alijichukulia Crimea kibabe, hakuridhika anataka achukue ardhi zaidi, kaingia kwenye hii operation akisema anaifanya kisa anaondoa NAZI Ukraine, mara anazuia Ukraine isijiunge NATO, mara anataka kulinda mikoa yenye watu wanao ongea lugha ya Kirusi, yaani vijisababu vya kila aina.

Tukitumia huo mfano wa kusema wanamega ardhi ya Ukraine kisa kuna watu wanaongea lugha ya Kirusi wanaonyanyaswa, hiyo ni kama kusema Malawi iivamie Tanzania na kutwaa mkoa wanaoishi Wanyasa kisa serikali ya Tanzania ina malumbano na Wanyasa. Au upande wa Kenya na Wamaasai.

Ifike mpate aibu, kwanza wale mnaounga huu udhulumaji kisa hisia za kidini, mlioaminishwa eti Urusi kwa kuivamia Ukraine inakomoa Marekani maana huwa mnahubiriwa kuwa Marekani ndio adui wa dini yenu.

Urusi itosheke na hii ardhi yote...iache hako kataifa kadogo hapo pembeni maana kataendelea kuitia aibu.

A324BBEF-12E5-409E-A0CB-7355E922EA2A_w1080_h608_s.png
 
Kama ni kubembeleza mataifa ya magharibi yalimbembeleza sana Putin asiingie vitani., lakini badala yake akajawa na kibri kwa kuwawekea meza ndefeefu eti anawakomoa ,mpira umebaki kwake Sasa,
Amalize vita aliyoanzisha mwenyewe

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom