Urusi yalaumu nchi za Magharibi na Kyiv kwa 'mauaji

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,938
Urusi yalaumu nchi za Magharibi na Kyiv kwa 'mauaji yaliyotekelezwa na wanajihadi'

Maafisa wakuu wa Urusi wameishutumu moja kwa moja Ukraine na nchi za Magharibi kwa kuhusika katika shambulio baya la ukumbi wa tamasha la Moscow, baada ya kundi la Islamic State (IS) kudai kuhusika.

IS imetoa video ya ukatili huo, lakini Vladimir Putin na washirika wake wawili wamedai wanajihadi hao walisaidiwa na ujasusi wa Magharibi na Ukraine.

Ukraine imekataa "uongo" wa Urusi.

Hali hiyo ina uwezekano mkubwa zaidi kwa sababu Marekani ilikuwa imeionya Urusi kuhusu shambulio lililokaribia siku 15 kabla.

Urusi inasema watu 139 waliuawa wakati watu wanne waliokuwa na silaha walipovamia jumba la tamasha la Crocus City Hall Ijumaa jioni. Wengine 22 bado wako katika hali mbaya, wakiwemo watoto wawili, maafisa wanasema.

Raia wanne wa Tajikistan wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutekeleza mauaji hayo. Washukiwa wengine wanne wameshtakiwa kwa kusaidia ugaidi.

Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak alisema ukweli kuhusu wahalifu na "kutofaulu kwa huduma za usalama za Urusi ni jambo lisilopingika". Nchi za Magharibi pia zimekejeli simulizi ya Kremlin.

Kiongozi wa Urusi alikiri wakati wa mkutano wa televisheni siku ya Jumatatu: "Tunajua uhalifu ulifanywa na Waislam wenye itikadi kali ... tunataka kujua ni nani aliyeamuru."

Alidai kuwa maswali mengi yalisalia bila majibu, akirudia madai yasiyo na msingi kwamba washambuliaji walijaribu kukimbilia kusini mwa Ukraine.
 
Taratibu tutapata ukweli wa mambo.... lkn kwa hili wa magharibi wanaonyesha wazi kuhusika kutokana na utabiri wao wa kinafiki.....
 
Isis ni wana jihad na mkakati wao mkubwa ni kupigana ili dunia nzima islimu mkakati ambao kamwe hauwezi kuungwa mkono na nchi yoyote ya magharibi hata Urusi na China hawawezi kukubali huo uwenda wazimu.

Hivyo Russia isisingizie nchi za magharibi kwa hilo shambulizi. Vikundi vya kigaidi kama Usis, Al Qaeda nk piga ua kamwe haviwezi kukubali kufadhiliwa na makafir.
 
VIDEO




Vikosi vya Urusi vya Ardhini leo Vimeinga ndani zaidi ya Mji wa ChasovYar
muda wowote mji Utakuwa mali ya Urusi Vikosi Vinakatiza Ndani ya Viunga Vya Mji bila Shida yeyote
 
Ukisikia Nchi Kuangamia Ndio huku
hapa Ni Kiev mji mkuu police kabisaa Hata Aibu Hana


 
Back
Top Bottom