Inawezekana, Ila
Best army ni combination ya navy, Airforce na land forces,
Kwa best army kura yangu ningempa USA,
PIA IWAPO utafuatilia technology nyingi za kijeshi russia yupo nyuma ya USA, Yaani USA wanainvest pesa kubwa sana kutafiti na kugundua vitu vipya, Jiulize kina f15 eagle walitoka mwaka gani, Alaf russia alitoa 4th generation mwaka gani, nani alianzisha stealth technology,(kumbuka f117 night hawk), Fuatilia kuhusu NIMITZ CLASS CARRIERS, , yan ni mbo mengi,
My take: ni ugunduz mzuri, Najua halitatumika, Limewekwa mkwara tu. Ila ni hatua kubwa kwao(japo haina manufaa kwetu)
Ila je ipo vipi mbele ya anti-ballistic systems, Kumbumba us antiballistics system inadetect tangu pale ballistic inapokua launched.
US army still ni strongest n the best
Kabla sijasema mengi labda nikurudishe nyuma kidogo kwa swali lifuatalo: Kama Merikani ilishindwa kukabiliana na magaidi walio rusha ndege tano na kuzibamiza kwenye majengo nyeti ndani ya aridhi ya Merikani leo hii Wamerikani ndiyo wajifanye wanaweza kukabiliana na missiles mahili za Warusi?? Oh, one more thing - remember Russian Technology is what flys American to space!! Hapo nimejaribu kujibu kwamba American army ni strongest kwa banana Republics not Russian Army Wanerikani wanakili hilo hawawezi kuwatunishia misuli Warusi wataishia kwenye makeke makeke kama kawaida yao na kutisha tisha third World Countries not the real McCoy.
Back to the main point, Mkuu labda nikujibu pointwise - ntaanza na statement yako ya mwisho: Ku-detect ICMB inaporushwa! Ukweli wa mambo ku detect ni kitu kingine na ku-intercept na kuharibu warheads ni kitu kingine.
Mkuu ni hivi: unaweza kuwa na uwezo wa kuona a niddle in a haystack lakini hilo aliwezi ku-save your skin, kwa maneno mengine hoja ya ku-detect in advance ignition ya booster roketi za ICBMs hiyo aisaidii kitu, itaona moto/smoke alright so what? - Mkuu, cha muhimu hapo ni: Do you have an interceptor yenye uwezo/capability ya ku-track a multiple thermonuclear warheads zinazo ambatana na dummies? kumbuka warheads zote (real na dummies) zinakuwa programmed kwa aligorithms za kuziwezesha ku - manoeuvre zikiwa in a terminal phase, mbinu hizo za Warusi zimewafanya Wamerikani na nchi za magharibi wakili kwamba awana system za kuweza kukabiliana na makombola ya ambayo yako highly unpredictable yakiwa kwenye terminal phase. Kwa mtu ambaye anaelewa wanamaanisha nini awezi kushangaa - lakini waswahili watakuja hapa na hoja nyingine za ajabu - wanajaribu kupinga vitu ambavyo ni obvious.
Kuna jamaa alikuja na hoja eti Wamerika wana uwezo wa kushambulia ICBMs pindi zinapo rushwa kutoka kwenye silos zake, wanacho sahau ni kwamba silos hizo ziko proctected na batteries za a no nonsense S-300MV au S-500 na Pantsir2 - missiles za Airdefence system tajwa zina uwezo wa kutambua aina zote za ndege za vita za nchi za magharibi (bombers na fighters), Drones, Cruise missiles hata artillary shells - zina uwezo vile vile wa kutambua missiles za adui na za kwao, range za missiles za S-300MV, S-500 na Pantsir2 ni kuanzia mita hamsini mpaka 500KM - sasa ni kombola gani linaweza kukatiza kwenye such unpregnable defence system!
Yaani sijui kwa nini baadhi ya members wa JF awajiuliza kwa nini Wamerikani na Israel pamoja na ujeuri wao na majigambo walinywea baada ya Warusi kuweka Airdefence system tajwa hapo juu nchini Syria, wamebaki kulalama lalama eti Putin ashitakiwe for war crimes, si Wamerikani na washirika wao wana ndege na cruise missiles karibu na Syria na Ghuba sasa mbona awashambulii bases za Warusi huko Syria au majeshi ya Asaad tangu Urusi iwape onyo kali - they know what to expect ndiyo maana awathubutu.
Repeat: Americans can't intercept latest Russian or Chinese ICMBs including airborne hypersonic vehicles ladden with termonuclear or conventional pay load and they know it, na mifano tunayo ya ku prove a point-miezi michache iliyo pita Warusi Walivurumisha supersonic cruise missiles kutoka bahari ya Caspician zikuruka umbali wa 1500KM mpaka Kwenye target nchini Syria, sasa kama Wamerica wengekuwa na uwezo wa ku-intercept Russian missiles mbona hawakufanya lolote, badala yake siku ya pili waliondoa the only aircraft carrier kwenye Ghuba/Gulf wakaipeleka umbali ambao range za Russain cruise missiles azewezi kuifikia!!!
Haya tuje kwenye jet fighters, hivi hujui kwamba Wamerikani walicopy designs za MiG-25 ndiyo wakahunda F-15 na F-14, soma kisa cha rubani wa Urusi aliye torosha MiG-25 na kuipeleka Ujapan baada ya kuhaidiwa angelipwa fedha nyingi akifakiwa kutorosha MiG-25 na design plan zake, Berenko alifanikiwa kuitirosha, baadae ndege ikawa dismantled na ikufungwa kwenye makreti ikasafirishwa kwenda Merikani ili kuchunguza teknolojia iliyo tumika kuhunda ndege ambayo kwa wakati huo ilikuwa inashikiria rekodi nyingi Duniani zikiwemo za kuwa na kasi kubwa pia na urukaji wa juu sana above sea level, Wamerika walijuwa hawana ndege kama hiyo wala ujuzi wa kuhunda kifaa kama hicho, wakati huo ndege walizo kuwa nazo ni aina ya Phantom na Super Hawk kama nakumbuka vizuri na zote zilikuwa na single rudder na single engine kama sikosei - baada ya ku copy MiG-25 ya Warusi ndiyo na Wamerika wakaja F-14 na F-15 zikiwa na design za twin rudder na engines wakaiga Warusi, watu awajui tu, Wamerikani wamekubuhu katika wizi wa teknolojia na design za Warusi linapokuja suala la jet fighters - kuanzia MiG-15/17(Korean War-Wamerikani walirubuni Rubani wa Korea Kaskazini watoreshe ndege tajwa), tukija MiG19/21(Jasusi wa Israel aliyekuwa anajifanya na Raia wa Syria alimtumia mwanamke kurubuni rubani wa Syria atoroshe MiG-21 kuipeleka Israel na alifanikiwa kuitotosha - baadae Wamerikani na Waisrael wakaifungua na kuangalia teknolojia iliyo tumika kuihuda) miaka ya hivi karibuni Wamerika tena waliwashurutisha Serikali ya Ukraine uwauzuie Sukhoi-27 walinunua ndege tatu au saba zilizokuwa zinatumiwa na jeshi la Ukraine na kuzipeleka Merikani ili wafanye reverse Engineering ndio walivyo, sasa swali - kwa nini walipania kujua Sukhoi -27 inavyo fanya kazi? ni hivi: mwaka 2003 Wamerikani waliwakaribisha Marubani wa Urusi nchi Merikani wakaja na ndege zao za Sukhoi-27 - wakatoa pendekezo la kutest ndenge za Urusi na Merikani katika urukaji, manuvrebility na dogfighting nk, nadhani Wamarekani walihisi uwezo wa Sukhoi kwa hiyo wakapendekeza majaribio hayo yafanyike kwenye bahari ya Pacific mbali kidogo na pwani ya Merikani ambako hakuna waadishi wa habari na cameras, Jeshi la Merikani alikutaka raia washuhudie kinacho endelea, majaribio yalipo anza kwa kushirikisha F-15, F-16 na F-18 a batch at a time, wanasema wana anga/marubani walishangazwa na uwezo mkubwa wa Sukhoi-27 karibu kwa nyanja zote za kivita hayo yalisemwa na wakuu wa jeshi la anga la Merikani - no Politics ni ma Professionals wanasema ukweli - hivyo tusishagae Wamerikani kununua ndege za Sukhoi-27 kutoka Ukraine. Binafsi sijawahi kusikia Warusi wakiagahika kuiba/torosha ndege za vita za Wamerikani -sijawahi!!!
Jaribuni kufatilia niliyo yaeleza humu mtajifunza mengi, mtagundua vile vile kwamba linapo kuja suala jet fighter design mkali ni nani.
Mwisho nimalizie kwamba the brains behind stealth aircraft technology ni Mrusi Dk Pyotr Y. Ufimtsev ambaye Physicist and Mathematician sijui ni watu wangapi wanalijua hilo - Mainjinia wa Lockheed wa huko Wamerikani walitumia mahesabu, vitabu na michoro vilivyo andikwa na mtaalamu huyo wa Urusi ndivyo viliwasaudia Wamerikani kuhunda ndege aina ya stealth, bila msaada wa Mrusi hao Merikani ingewachukua muda mrefu au wasingejua nini kunaedelea, watu wanakuja humu na maneno mengine ya kushangaza wanasahua kwamba Urusi ndiyo inaongoza Duniani kuwa na per capita kubwa ya Ma Engineers na Mathematicians.
Warusi walifanya tafiti nyingi za hali ya juu kwenye mambo mengi ya silaha na ndege za vita - Wamerikani utumia sana tafiti na machapisho ya Warusi katika kuhunda silaha na ndege na kuboresha hapa na pale inapo bidi.