Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
yeye kuutaka urais sio jawabu la wananchi nao kumtaka rais mkigoma,naona kwa hiyo cd ya ukigoma aliyoamua kucheza ndo itamharibia zaidi
 
Inatakiwa kuheshimu maoni ya wengne c kila kitu upinge tu.

Zitto anatakiwa kutubu katika chama chake kuwa amekosea.

Napata wasiwasi na mienendo ya Zitto kwa sasa kwani inaonesha imekisa hekima na busara.

Ni hayo tu yangu
We nae vipi mie hapa si nimetoa maoni yangu au unataka nitoe ya kwako?
Afu mleta mada anazungumzia Zitto au kufa kwa chadema? Zitto sio lolote wala chochote ndani ya chama na kama kufa atakufa yeye kisiasa lakini chadema itaendelea kuwepo!
 
Sana sana aanze kufikiria uwaziri mkuu baada ya Dr Slaa kuchukua nchi 2015.. Zito anabweteka bure!!! Iwapo ana akili timamu atang'amua kuwa kasi ya watanzania kuipenda CHADEMA ni kwa ajili ya Dr Slaa!!
 
Zitto ni sawa na HIV-Virus (CD4).
Ukweli Wa Zitto:

Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Halima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho

Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.

Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.

Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka.. anajaribu kukiua CHADEMA kwa maslahi ya CCM. Chunguzeni hela alizonazo.

Huyu mtu ni mpokea rushwa balaa.... vogue, anayo, Hummer Anayo na VX yote kanunuliwa na Rostam

nawakilisha

Kwa vile Zito katangaza wazi kuwa "urais" anaupenda, kwa vile watu wake wa karibu wamesema kuwa lazima rais wa 2015 atoke Kigoma, kwa vile kwa nyakati mbalimbali tumeona kuwa Mh Zito amekuwa na matamshi ya kung'ata na kupuliza; kukana na kukiri baadaye kuwa kasema, kwa vile hata uenyekiti wa Chadema aliwania akanyamazishwa na Chama, ....
nadiriki kusema Chadema haitapona kuvurugwa na Zito Kabwe, na hatimaye kusambaratishwa kama vilivyokuwa vyama vya NCCR Mageuzi, na CUF....
kisha Zito atatimkia chama kingine dhaifu ili atimize azma yake ya kuwania urais kupitia chama hicho au ugombea binafsi. Chadema ikitaka kubaki imara isiyapuuze sana yanayoendelea.
Huu ni mtazamo wangu tu... ninaweza kupingwa..

 
Chama kikiwa kikubwa (complex) namna hii, lazima kuna watu tofautitofauti. Wenye kuudhi, kufurahisha, burudisha, 'kukera', kuhamasisha, etc. Ah, mii sijali. CDM my party, hata kigoma yote ikirudi ccm. Tokeni hapa wote, mnaniudhi.
 
Zitto anatumiwa na magamba ili awasafishie njia kwani hana uwezo wa urais.Chadema muwe makini na hawa makuwadi wa magamba.
 
Clinton na Harper wamejiandaa kwa muda gani?..Kina Putin, Kibaki, Kagame M7 na wengine kibao walianza toka enzi za Uhuru..Kichuguu mkuu wangu watu hawa wote huandaliwa nyuma ya pazia na sii watu wanajitokeza tu kama unavyosikia ktk Tv na magazeti..Mtoto wangu miye alikuwa shule ktk hafla ya shule aliulizwa swali - Utataka kuwa nani ukikua?.. mtoto alijibu - " I wonna be The Prime Minister of Canada.." Watu walimpigia makofi na kushangilia badala ya kumpuuza... Mkuu wangu huyu ni mtoto wa miaka 8 tu, walokuwepo sii wajinga kumshangilia na kumpa moyo na heko japokuwa wanajua ni ndoto haiwezekani kiurahisi, lakini it's the message behind it ndio wenzetu wanacho kitazama. Nguvu ya majibu kama yale na sii kufadhaika..Mijinga kina sisi tunamtazama Zitto na kuanza kupiga mahesabu...

Nina imani kuwa huwa hawajiandai kama ambavyo mwenzetu Zitto anavyojiandaa; tunaweza kujadiliana hilo. Kati yao wote uliotaja hapo, hakuna hata mmoja aliyewahi kutangaza nia za kuwania ukuu wa nchi miaka mitano kabla ya uchaguzi. Wote wamakuwa wanatangaza wakati wa mchakato wa uchaguzi tu; na wengine wao huwa wanapata ukubwa wa nchi kwa sababu ya kuwa viongozi wa vyama vyao. Kupiga kampeini na kuunda organization za uchaguzi muda mrefu kabla ya uchaguzi huwa ni dalili ya udhaifu mkubwa sana kwa candidate.

Halafu kumbuka kuwa kumshangilia mtoto na kumpa moyo katika jambo lolote ni jambo la kawaida sana na ni tofauti na kumshangilia mtu mzima ambaye unajua kuwa analofanya si sahihi. Zitto angeweza kukaa kimya akiwa na plani zake akisubiri wakati wa mchakato wa uchaguzi ndipo atangaze nia yake. kwa nini afungulie mode ya uchaguzi mapema namna hiyo. Ninaweza kuwa ni mjinga kwa macho ya wengine lakini naamini kuwa nina busara za kutosha sana kuona mapungufu ya Zitto katika swala hili la urais.
 
Tafadhali wabunge makini wa Chadema angalieni msitumike kukivuruga chama chenu.Chadema ni chama tawala mbadala Tanzania na ni chama tawala 2015.
 
well said mkuu...

Zitto is very smart, but not a presidential material!! he is not strategic, and most of all, zitto ANAWASHWA-WASHWA SANA na tamaa zisizofichika hadi kuparamia lile mama fisadi ili apate pesa

Funguka zaidi mkuu, una maana naye ni Marioo?!
 
Wed, Jul 25th, 201
Headlines / Tanzania |


By Teonas Aswile


The Northern Kigoma MP and CHADEMA Deputy General Secretary, Zitto Zubery Kabwe has denied the rumors/whispers which connect him with the speeches given by MPs in Kigoma All Starts Concert held in Kigoma Region recently.

zitto1.jpg


Northern Kigoma MP, Zitto Kabwe (4Th from Left) with other MPs who attended Kigoma All Starts Concert held in Kigoma few weeks ago, as pictured when they were greeting the majority.

Zitto Kabwe quoted 23[SUP]Rd[/SUP] July, 2012 Mwananchi Newspaper headline which states Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015, (not official translation) ‘MPs purify Zitto way to 2015 Presidency.'


Responding to the rumors Zitto said first all the public should know that all MPs who participated in the event namely, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), Deo Filikunjombe (CCM), Halima Mdee (CHADEMA), Joshua Nassari (CHADEMA), Esther Bulaya (CCM) and others were invited by the Concert Coordinator who also was among the musicians, Mwasiti Almasi. Other MPs invited did not attend after sending excuses.


Also he said all MPs invited were given caution that it was the Entertainment invitation so there were no any political agendas which would be discussed.

"So they were given chance of greeting Kigoma people who appeared for the concert. So it is unfortunate if there is any legislator who spoke about politics and 2015 General Election. I should not be associated with what MPs spoke to the public in Kigoma."

Zitto Kabwe who has also been linked with 2015 Election interest via his party, CHADEMA has said the party has no Presidential candidate because the time is not yet.


He warned Tanzanians to stop thinking about 2015 General Election while there are still different challenges which face the society and have to be worked upon.


SITAKI KUHUSISHWA NA MAKANUSHO YA WABUNGE WALIOKUWA KIGOMA-​
Zitto Z Kabwe

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kuyasema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi bali nilisaidia 'logistics' tu. Lengo la kushauriana na Vijana wa Kigoma All Stars kuwaalika wabunge kutoka vyama mbalimbali lilikuwa ni kuonyesha umoja na mshikamano wa nchi bila kujali vyama vya siasa.

Wabunge wote walioalikwa waliambiwa hii ni shughuli ya muziki na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa. Ni bahati mbaya sana kuwa kuna matamshi ya kisiasa yalitamkwa katika shughuli ile.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu. Mimi kama mlezi wa KigomaAllStars na vijana wenyewe tulijikita katika 'shukrani Kigoma' kwa watu wa Kigoma.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma.

Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.​





 
zitto kwanza aoe ili apate heshima bila ilo anabaki kuwa msela tu na hafai kupewa heshima kama ya january! yule dada aliezaa nae kwanini hamuoi? ni wingu baya either alitolee ufafanuzi au amuoe!
 
Mambo mengine yanakera sana,tunapenda sana unafiki na uongo.Tunazusha mjadala ilimradi una maslahi na kundi fulani basi,tunalishabikia bila kujali muda tunaoupoteza!
 
unalolidai si sahihi sana kwani kabwe ni mzuri sana wa kujenga hoja na kusimamia anachokiona kuwa kiko sahihi...Hii tabia amekua nayo toka akiwa pale UDSM na sidhani kama ni unafiki kuwa na different opinion against the majority......

Kupanga hoja na kuzitetea si sifa pekee ya kuwa kiongozi anayefaa, kwani inawezekana ni njia ya kujitafutia umaarufu. Zitto hayuko tayari kukosolewa, na angalia mada hii ilipoteremshwa hapa alivyojitahidi kujenga hoja ya kutetea nafasi ya yeye kuwani urais, na kutaka kuleta vpande vya video clips ili kuwadhalilisha wabunge wenzake Halima Mdee na Nassari..

Uongozi bora ni pale wananchi wanapokuona unafaa na wala si wewe kuhaha kutafuta nafasi hiyo hata pale wanapokuona hufai.

Zitto bila kuonea aibu anaweza hata kukisaliti chama chake, kama huamini ipo siku utayaamini maneno yangu. Kitendo cha kuwasaliti Halima Mdee na Dogo wa Arumeru Mashariki ni dalili wazi za udhaifu ambao kiongozi alitakiwa kuwa na ustahimilivu pamoja na uvumilivu kwani vinginevyo ni kujenga ubinafsi ambao kwa kiongozi haufai kabisa, na kabisa kuweka ufa kati yake na viongozi wenzake. Sishangai kama viongozi wenzake wa Chadema wanamvumilia ila tu kwa ajili ya kujenga chama na kukwepa kuweka nyufa wameamua tu kumsitiri pale chamani. Kumbukeni ya Kafulila, Kaburu na Zitto ni damu ile ile. Anachohofia ni kuhadaiwa na CCM kama ilivyotokea kwa Kaburu ambaye amenyong'nyezwa kama tu aliyepigwa sindano ya ganzi hasikik kabisa.

Mara zote viongozi wa Chadema wanapopata matatizo katika jitihada zao za kutetea wananyonge na taifa hili Zitto amekwepa. Hoja ya ukwepaji mwenyewe ameshawahi kumtamkia Speaker Makinda kipindi cha mchakacho wa kukataa posho, alipomshinikiza kumwadabisha, Zitto alisema atatumia njia za kianafunzi kwa kuchangia hoja bungeni kila siku na hivyo shinikizo la kutohudhuria bungeni halitamwandama kwa vile hadidu rejea za bungeni zitaonyesha mahudhurio kwa kuchangia. Alitamka wazi atamzidi kete Makinda kwa ujanja wa kianafunzi. Kwa hiyo kwa mtazamo wangu huwezi kuongoza nchi kwa ujanja ujanja wa kianafunzi, ni kuleta matatizo makubwa kwa taifa, tutajuta kuwa na kiongozi wa kitaifa wa aina hiyo anayeongoza nchi kwa mtindo wa ujanja wa kianafunzi.

Kwa kifupi tu Zitto Kabwe ni jeuri na hatari na inabidi kuwa makini sana kwa kufuatili Nyendo zake, na sishangai kama anaweza akawa anauma huku na huko ili kujenga jina la kulinda nafasi yake na masilahi binafsi.
 
Ndugu yangu Zitto, kama unafahamu nchi ina mambo mengi ya kushughulikia badala ya kila leo nani atakuwa rais, kwanini basi uyaanzishe kila wakati??? Maanake Kigoma siyo mara ya kwanza; Una haki ya kutoa mawazo yako, lakini huyapeleki au kuyatoa kwa jinsi inavyotakiwa.

 
Clinton na Harper wamejiandaa kwa muda gani?..Kina Putin, Kibaki, Kagame M7 na wengine kibao walianza toka enzi za Uhuru..Kichuguu mkuu wangu watu hawa wote huandaliwa nyuma ya pazia na sii watu wanajitokeza tu kama unavyosikia ktk Tv na magazeti..Mtoto wangu miye alikuwa shule ktk hafla ya shule aliulizwa swali - Utataka kuwa nani ukikua?.. mtoto alijibu - " I wonna be The Prime Minister of Canada.." Watu walimpigia makofi na kushangilia badala ya kumpuuza... Mkuu wangu huyu ni mtoto wa miaka 8 tu, walokuwepo sii wajinga kumshangilia na kumpa moyo na heko japokuwa wanajua ni ndoto haiwezekani kiurahisi, lakini it's the message behind it ndio wenzetu wanacho kitazama. Nguvu ya majibu kama yale na sii kufadhaika..Mijinga kina sisi tunamtazama Zitto na kuanza kupiga mahesabu...

Kuandaliwa au kujiandaa sipingani nalo nawe, ila mwandaliwa au anayejiandaa huwa na werevu wa kupima kwanza maneno anayotamka na kwa anaowatamkia na nafasi anapoyatamka. Pengine kutuliza kichwa na kupoza nerves kwanza itasaidia kupata neno la burasa na hekima badala ya kukurupuka kama Zittoa alivyofanya. Ulimi huweza kumwangamiza au kumsimamisha mtu na huu ndio ukweli wenyewe.

Kuna kauli ambazo zinakuwa na nafasi ya kuzipa uzito zitolewapo rasmi na kuna kauli ambazo ni misikhara ya kawaida hasa watu wawapo katika kadamnasi ya maburudisho ya kujirusharusha na kuhamasisha audience. Wakinitania jambo kama hilo mtu kama mimi hata kama nina matamanio nayo najua tu ni kuongeza tu furaha ya wasikilizaji na si jambo la kuweza kujenga hoja ya kulivimbia kama Zitto alivyofanya.

Kwa vyo vyote Zitto anakosa busara ya kawaida kama mambo mengi katika safu ya uongozi wa Chadema kitaifa, mwoga, hana ushirikiano wa wazi katika machungu ila katika matamu tu. Kukwepa kwepa huku katika mambo mengi ndiko huku tunakosema Rais wa nchi anabaki kurudi Magogoni kwa ajili ya kubadilisha nguo na maisha yake ni kwenye mahoteli ya kitalii nchi za nje akila kodi za wananchi kwa visingizio vingi tu vya mikutano isiyo isha. Je marais wengine hawana nafasi hiyo na kwa nini wanaamua kutulia katika nchi zao?

Hayo ndiyo yanayoweza kutupata tena tukiwaendekeza watu kama akina Zitto, vinginevyo wajirekebishe na umri upande kidogo bongo lao litatulia na labda anaweza kuturudishia matumaini, lakini kwa sasa hafai kuwa Rais.
 
Sana sana aanze kufikiria uwaziri mkuu baada ya Dr Slaa kuchukua nchi 2015.. Zito anabweteka bure!!! Iwapo ana akili timamu atang'amua kuwa kasi ya watanzania kuipenda CHADEMA ni kwa ajili ya Dr Slaa!!

Huo ndio ukweli, Kwani chama kimepata umaarufu lini?? Ni baada ya dr kugombea urais na watu kufunguka macho kwamba kuna mtu ana weza akawa mbadala

 
Nina imani kuwa huwa hawajiandai kama ambavyo mwenzetu Zitto anavyojiandaa; tunaweza kujadiliana hilo. Kati yao wote uliotaja hapo, hakuna hata mmoja aliyewahi kutangaza nia za kuwania ukuu wa nchi miaka mitano kabla ya uchaguzi. Wote wamakuwa wanatangaza wakati wa mchakato wa uchaguzi tu; na wengine wao huwa wanapata ukubwa wa nchi kwa sababu ya kuwa viongozi wa vyama vyao. Kupiga kampeini na kuunda organization za uchaguzi muda mrefu kabla ya uchaguzi huwa ni dalili ya udhaifu mkubwa sana kwa candidate.

Halafu kumbuka kuwa kumshangilia mtoto na kumpa moyo katika jambo lolote ni jambo la kawaida sana na ni tofauti na kumshangilia mtu mzima ambaye unajua kuwa analofanya si sahihi. Zitto angeweza kukaa kimya akiwa na plani zake akisubiri wakati wa mchakato wa uchaguzi ndipo atangaze nia yake. kwa nini afungulia mode ya uchaguzi mapema namna hiyo. Ninaweza kuwa ni mjinga kwa macho yeawengine lakini naamini kuwa nina busara za kutosha sana kuona mapungufu ya Zitto katika swala hili la urais.

Kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho, kimwingiacho katu hakimchafui. (Nabii Issa)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom