Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Zitto ni sawa na HIV-Virus (CD4).
Ukweli Wa Zitto:

Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Halima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho...

Waandidhi mwajua mengi kwa vile mko kwenye lake-pond wanakoenda kuogelea wenye njaa ya kupata dagaa kwa njia ya mkato kupitia journalists.
 
JF tumekaa nyuma ya keyboard na kushambulia watu wanaodare kutangaza nia zao hadharani, wenye uthubutu. Tutaishia hivi hivi watu wanatangaza nia na sisi tunaona haiwezekani halafu inawezekana na watu wanakula nchi kama kawaida.

Nina uhakika 35-47% ya JF members hawakupiga kura 2010 huku wakiwa na vigezo ila wakaona ni usumbufu. Hao wapiga kura asilimia chache sana wanaijua JF na wanaelewa hiki kinachojadiliwa humu. Mwananchi na magazeti mengine ndio chanzo kikubwa cha habari kwa watu walio wengi na ndio maana mwenzetu anatuacha na JF yetu yeye huyoooo kwenye Mwananchi. Tunahitajika kuwaelemisha watu kwa kuwafikia na sio kuelemishana sisi kwa sisi ambao wote tunaelewa angalau kidogo.

ON Presidential Note: CDM hawajawa tayari kumwandaa mtu mmoja kuja kuichukua hii nchi, hivyo kila mtu anajiandaa kivyake na Zitto anafanya hivyo kwa sababu chama kama chama hakijakaa na hakitaki kukaa kikakubaliana kwamba sasa sote tupige kampeni juu ya huyu hata kama sio rasmi basi ieleweke. Urais isiwe kushtukizana, mtu aandaliwe ikibidi mwenyewe aanze kuiishi misingi hiyo ya ki-Rais.

Hizi mambo za kushtukizana ndio hizo zinaibuwa mtu kujivua lawama siku akichemsha. CDM needs to change their approach towards this president thing for sure to avoid last minute surprise.
 
Kuandaliwa au kujiandaa sipingani nalo nawe, ila mwandaliwa au anayejiandaa huwa na werevu wa kupima kwanza maneno anayotamka na kwa anaowatamkia na nafasi anapoyatamka. Pengine kutuliza kichwa na kupoza nerves kwanza itasaidia kupata neno la burasa na hekima badala ya kukurupuka kama Zittoa alivyofanya. Ulimi huweza kumwangamiza au kumsimamisha mtu na huu ndio ukweli wenyewe.

Kuna kauli ambazo zinakuwa na nafasi ya kuzipa uzito zitolewapo rasmi na kuna kauli ambazo ni misikhara ya kawaida hasa watu wawapo katika kadamnasi ya maburudisho ya kujirusharusha na kuhamasisha audience. Wakinitania jambo kama hilo mtu kama mimi hata kama nina matamanio nayo najua tu ni kuongeza tu furaha ya wasikilizaji na si jambo la kuweza kujenga hoja ya kulivimbia kama Zitto alivyofanya.

Kwa vyo vyote Zitto anakosa busara ya kawaida kama mambo mengi katika safu ya uongozi wa Chadema kitaifa, mwoga, hana ushirikiano wa wazi katika machungu ila katika matamu tu. Kukwepa kwepa huku katika mambo mengi ndiko huku tunakosema Rais wa nchi anabaki kurudi Magogoni kwa ajili ya kubadilisha nguo na maisha yake ni kwenye mahoteli ya kitalii nchi za nje akila kodi za wananchi kwa visingizio vingi tu vya mikutano isiyo isha. Je marais wengine hawana nafasi hiyo na kwa nini wanaamua kutulia katika nchi zao?

Hayo ndiyo yanayoweza kutupata tena tukiwaendekeza watu kama akina Zitto, vinginevyo wajirekebishe na umri upande kidogo bongo lao litatulia na labda anaweza kuturudishia matumaini, lakini kwa sasa hafai kuwa Rais.
Sawa ebu nambieni makosa ya Zitto ni yapi? walosema kwamba anafaa kugombea Urais ni hawa vijana wetu sio Zitto na kama kuna makosa yamefanyika tulilaumu gazeti la Mwananchi lakini maajabu ni kwamba story hii toka itoke watu wamekuwa na majibu yote wao wenyewe..

Hawa vijana Halima Mndee na Nasari hawajasema mahala popote ukweli - Wao walisema nini jukwaani.? Na hakuna mtu hapa JF anajua wala anataka kujua kwa sababu hawa wanaaminiwa hawakusema pengine hata wakisema hawakufika jukwaani.

I know wabongo wakiwa jukwaani husema vitu ambavyo baadaye huvijutia , beside niliwapinga tu walipotumia Ujana kuwa sababu ya Zitto kuchukua uongozi hata Ben alikuwa nami siku hiyo. Maneno haya sijayasikia leo tu ninawasoma vijana hawa mara kwa mara ktk tweet, M4C, marafiki wa Slaa na kadhalika lugha zao ni hizi hizi na hupelekeshana nao.

Gazeti limeandika, hawa jamaa wamekuja kuliruka gazeti lakini wasiseme walisema nini jukwaani, halafu kaja Zitto akasema kilichoandikwa ndicho walichosema kulingana na anavyokumbuka maana alikuwpeo uwanjani.. Mimi na wewe hatukuwepo lakini tunamwiona Zitto ndiye mwongo. Mbona siwasikii tena hawa vijana Halima na Nasari wakirudi kukanusha ya Zitto?.. Mimi nataka wao watuambie walisema nini ktk sherehe zile halafu tutapima na ushahidi utakaopatikana.. nani mkweli baina ya wao na gazeti la Mwananchi..

Zitto hahusiki kabisa isipooikuwa alipolisoma gazeti anachokumbuka ndicho walichokisema wahusika.. Hivi kweli yeye anatakuwa mjinga vipi apeleke uongo gazetini halafu ajitokeze na kusema well kilichoandikwa ndivyo walivyosema.. Bila shaka kama yeye ndiye aliwapa waandike hivyo angekaa kimnyaa ajifanye sio yeye lakini sio kujitoa mbele kuonyesha anakubaliana na gazeti wakati mtunzi ni yeye..It doesn't make sense..
 
JF tumekaa nyuma ya keyboard na kushambulia watu wanaodare kutangaza nia zao hadharani, wenye uthubutu. Tutaishia hivi hivi watu wanatangaza nia na sisi tunaona haiwezekani halafu inawezekana na watu wanakula nchi kama kawaida.

Nina uhakika 35-47% ya JF members hawakupiga kura 2010 huku wakiwa na vigezo ila wakaona ni usumbufu. Hao wapiga kura asilimia chache sana wanaijua JF na wanaelewa hiki kinachojadiliwa humu. Mwananchi na magazeti mengine ndio chanzo kikubwa cha habari kwa watu walio wengi na ndio maana mwenzetu anatuacha na JF yetu yeye huyoooo kwenye Mwananchi. Tunahitajika kuwaelemisha watu kwa kuwafikia na sio kuelemishana sisi kwa sisi ambao wote tunaelewa angalau kidogo.

ON Presidential Note: CDM hawajawa tayari kumwandaa mtu mmoja kuja kuichukua hii nchi, hivyo kila mtu anajiandaa kivyake na Zitto anafanya hivyo kwa sababu chama kama chama hakijakaa na hakitaki kukaa kikakubaliana kwamba sasa sote tupige kampeni juu ya huyu hata kama sio rasmi basi ieleweke. Urais isiwe kushtukizana, mtu aandaliwe ikibidi mwenyewe aanze kuiishi misingi hiyo ya ki-Rais.

Hizi mambo za kushtukizana ndio hizo zinaibuwa mtu kujivua lawama siku akichemsha. CDM needs to change their approach towards this president thing for sure to avoid last minute surprise.

Labda ni wewe tu ambaye hujui kuwa dr. Slaa ndiye raisi mtarajiwa wa jmt, kutinga ikulu kupitia tiketi ya chadema, na wananchi hawababaishwi na propaganda, wamekubali kukitosa chama maarufu na kikongwe kuliko vyote nchini kwa ajili ya chadema tarajio kuu la wananchi ni amiri jeshi mkuu kuwa dr. Slaa, usitarajie kuna kapukumeni na ubinafsi binafsi wake (zito) atawakengeusha freedom fighters. Ya zito ni mashuzi, kavimbiwa migebuka yeye na kufulila wake wanaoota kuifanya migebuka kitoweo cha kitaifa kwa mujibu wa tamasha lao la kibaguzi (kigoma)
 
zitto...mbona vijana wenzako akina mnyika, lissu, mdee, wenje, nyerere hawasemwi hivi...kutaka uongozi si vibaya ila sehemu ya kutangazia kijana...sio bungeni wala sio kwenye matamasha fuata taratibu za chama bwana...mie nakukubali na naikubali CHADEMA sana na naamini ndicho chama cha ukombozi toka kwa hawa majambazi wa ccm...ungana na wenzako jenga chama ili upate kura za kutosha...na uoe...tena mwanamke anaejielewa...thats all bro nakutegemea sana mtu wangu usiangushe chama cha vijana wenzako jenga chama jenga CHADEMA jenga TANZANIA...
 
Sawa ebu nambieni makosa ya Zitto ni yapi? walosema kwamba anafaa kugombea Urais ni hawa vijana wetu sio Zitto na kama kuna makosa yamefanyika tulilaumu gazeti la Mwananchi lakini maajabu ni kwamba story hii toka itoke watu wamekuwa na majibu yote wao wenyewe..

Mnde na Nasari hawajasema mahala popote ukweli wao walisema nini jukwaani. nahakuna mtu anataka kujua kwa sababu hawa wanaaminiwa. I know wabongo wakiwa jukwaani husema vitu ambavyo baadaye huvijutia. Beside niliwapinga tu walipotumia Ujana kuwa sababu ya Zitto kuchukua uongozi.. Maneno haya sijayasikia leo tu ninawasoma vijana hawa mara kwa mata ktk tweet, M4C, marafiki wa Slaa na kadhalika lugha zao ni hizi hizi.

Gazetiu limeandika hawa jamaa wamekuja kuliruka gazeti lakini wasiseme walisema nini, kaja Zitto akasema kkilichoandikwa ndicho walichosema.. Mbona siwasikii ttena hawa vijana wakirudi kumkanusha Zitto?.. Mimi nataka wao watuambie walisema nini ktk sherehe zile halafu tunapima na ushahidi utakaopatikana.. nani mkweli baina ya wao na gazeti la Mwananchi..

Zitto hahusiki kabisa isipooikuwa alipolisoma gazeti anachokumbuka ndicho walichokisema wahusika.. Hivi kweli yeye anatakuwa mjinga vipi apeleke uongo gazetini halafu ajitokeze na kusema well kilichoandikwa ndivyo walivyosema.. Bila shaka kama yeye ndiye aliwapa waandike hivyo angekaa kimnyaa ajifanye sio yeye lakini sio kujitoa mbele kuonyesha anakubaliana na gazeti wakati mtunzi ni yeye..It doesn't make sense..

Mkandala, pamoja na yote uliyosema, ukweli upo palepale Zitto leo Bungeni Dodoma alipotoka nje ya mada yake ya kuchangia Wizara husika na kuanza kutangaza nia ya kugombea Urais kuwa anafaa.

Kiongozi ye yote mwenye busara pale bungeni leo hapakuwa na ajenda ya kujadili wagombea Urais uchaguzi Mkuu ujao, lakini Zitto amechomekea mchango wake kuwa ni mtu anayefaa kuwa rais kwa sifa alizotaja yeye. Hicho ndicho tunachojadili hapa.

Mkandala, kwa busara ya kawaida tu Zitto hakutakiwa kuvimbisha kichwa katika suala kama hili ambalo watu walikuwa katika tamasha kwenye burudani ya muziki ambako ujuavyo uwapo jukwaani unajaribu kumpamba mtu kwa kila njia iwezekanayo, ingawa ni maua au kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa tu. Lakin maskini Zitto imemvimbisha kichwa hadi kuingia Bungeni kwa kutetea hilo.

Mkanda, huoni kama huo ni udhaifu wa wazi, kwani bora kwa busara ya kawaida angeamua kutuliza kichwa badala ya kuendelea kung'ang'ania hoja hiyo? Je, lile tamasha la Muziki lilikuwa kwa ajili ya kujitangaza kugombea Urais? Je walioalikwa waliandaliwa kumtanza Zitto juu ya azima hiyo? Tunaweza kuamini Zitto aliandaa tamasha lile kwa lengo hilo kwa vile Bungeni leo amepasua jipu hilo bungeni kwa kutetea?
 
Vogue and hummer? kama kweli zitto umetisha...habari yako kaka, duuuh...sijui tumuamini nani sasa?
 
Hakuna la kushangaza hapa labda wewe ndio unashangaa. Hawa vijana walisha panga siku nyingi na hakuna upumbavu wowote ikiwa ktk mikutano yao wanaamini kabisa rais ajaye lazima awe kijana na wanagombania katiba mpya ishushe umri..Sasa wewe nambie unampitisha kijana gani kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano leo hii?. Kwa nchi kama Tanzania nimeshawasikia viongozi wengi sana wakisema wana uwezo wa kuongoza, sema tu hawa sii maarufu wala haikuwa muhimu kwangu..

Hivyo, hawa vijana waruke wasiruke ndivyo vijana wetu wanavyotuonyesha hawajakomaa kisiasa. Lakini nasema hivi ndivyo wanavyofikiria na inawezekana wamesema yaliyoandikwa maana wanajiandaa kumweka mgombea 2015 kijana.. How? hilo sijui na wala sintopenda kujua lakini wataweza vipi kumweka mgombea kijana pasipo kuanza maandalizi leo au kesho..... Maneno ya Zitto bungeni yanadhihirisha zaidi nia yake na anajua nyuma yake ana support kubwa. Na nimeshasema mtu yeyote anaweza kuweka nia ya kugombea hakuna ubaya. Je, Kuna Mbunge alosimama na kumpinga au kuomba mwogozo? sidhani.. kumbuka Zitto alisema nini kuhusu mzee Thabit Kombo?..
 
Wakati tunaisubiri hiyo Video,(ambayo kiukweli mimi cna imani nayo nahic itakuwa imechakachuliwa,kwanza mbona imekaa muda mrefu,pili kwanini wabunge karibu wote wakanushe,tatu,hv huyo mwandishi wa Mwananchi ndiye pekee, Zitto na Kafulila ndio waliyasikia hayo,wapi waandishi wa Nipashe,wapi TZ daima),nilikuwa nauliza hv,HAKUKUWA NA WANAJF cku hiyo,kwenye hilo TAMASHA ili nao bac tuwasikie,maana wengi ni GREAT THINKER na WAKWELI,kama mpo hebu tusaidieni jamani!
 
Labda ni wewe tu ambaye hujui kuwa dr. Slaa ndiye raisi mtarajiwa wa jmt, kutinga ikulu kupitia tiketi ya chadema, na wananchi hawababaishwi na propaganda, wamekubali kukitosa chama maarufu na kikongwe kuliko vyote nchini kwa ajili ya chadema tarajio kuu la wananchi ni amiri jeshi mkuu kuwa dr. Slaa, usitarajie kuna kapukumeni na ubinafsi binafsi wake (zito) atawakengeusha freedom fighters. Ya zito ni mashuzi, kavimbiwa migebuka yeye na kufulila wake wanaoota kuifanya migebuka kitoweo cha kitaifa kwa mujibu wa tamasha lao la kibaguzi (kigoma)

Usijidanganye kwamba kwa vile aligombea 2010 ndio lazima agombee 2015, mambo yanabadilika ndugu. Huyo Mbowe mwenyewe anautaka huo urais, we subiri uone wanavyotoana macho! Maslahi kaka, siasa ni kazi na kazini kila mtu anataka kupanda cheo.

Kuna mtu anasema "A need once achieved is no longer a motivation", ie all MPs would like to be upgraded to next steps which is probably presidential seat.

Take note, Slaa will not stand for it, keep this and remind me if it happen otherwise.
 
Wakati tunaisubiri hiyo Video,(ambayo kiukweli mimi cna imani nayo nahic itakuwa imechakachuliwa,kwanza mbona imekaa muda mrefu,pili kwanini wabunge karibu wote wakanushe,tatu,hv huyo mwandishi wa Mwananchi ndiye pekee, Zitto na Kafulila ndio waliyasikia hayo,wapi waandishi wa Nipashe,wapi TZ daima),nilikuwa nauliza hv,HAKUKUWA NA WANAJF cku hiyo,kwenye hilo TAMASHA ili nao bac tuwasikie,maana wengi ni GREAT THINKER na WAKWELI,kama mpo hebu tusaidieni jamani!

Kama huwajui wanasiasa subiri hiyo video, itatoka itatamka exactly gazeti lilivyoandika nao watakuja kwa kusema sikumaanisha hivi au vile, na usishangae wakakwambia maneno ya kukanusha walilishwa.
 
Hakuna la kushangaza hapa labda wewe ndio unashangaa. Hawa vijana walisha panga siku nyingi na hakuna upumbavu wowote ikiwa ktk mikutano yao wanaamini kabisa rais ajaye lazima awe kijana na wanagombania katiba mpya ishushe umri..Sasa wewe nambie unampitisha kijana gani kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano leo hii?. Kwa nchi kama Tanzania nimeshawasikia viongozi wengi sana wakisema wana uwezo wa kuongoza, sema tu hawa sii maarufu wala haikuwa muhimu kwangu..

Hivyo, hawa vijana waruke wasiruke ndivyo vijana wetu wanavyotuonyesha hawajakomaa kisiasa. Lakini nasema hivi ndivyo wanavyofikiria na inawezekana wamesema yaliyoandikwa maana wanajiandaa kumweka mgombea 2015 kijana.. How? hilo sijui na wala sintopenda kujua lakini wataweza vipi kumweka mgombea kijana pasipo kuanza maandalizi leo au kesho..... Maneno ya Zitto bungeni yanadhihirisha zaidi nia yake na anajua nyuma yake ana support kubwa. Na nimeshasema mtu yeyote anaweza kuweka nia ya kugombea hakuna ubaya. Je, Kuna Mbunge alosimama na kumpinga au kuomba mwogozo? sidhani.. kumbuka Zitto alisema nini kuhusu mzee Thabit Kombo?..

Mkandala, umeshaona aliyeumwa na nyoka huogopa hata kamba ya kufungia kuni?
 
SAM_4088.JPG
 
Kama huwajui wanasiasa subiri hiyo video, itatoka itatamka exactly gazeti lilivyoandika nao watakuja kwa kusema sikumaanisha hivi au vile, na usishangae wakakwambia maneno ya kukanusha walilishwa.

Unachosema mkuu yawezekana,ingawa credibility ya Mwananchi imepungua hasa kutokana na kumradhi kwa MEMBE,ndio maana nikasema ingekuwa vizuri tupate kundi jingine huru,lililokuwepo tulickie,ndio nikauliza kwani siku hiyto hakukuwa na wanajf kwenye hilo tamasha?
 
Gazeti la Mwanahalisi toleo la leo kila kona habari yake inanyofolewa, lakini kama limekuwa published whats wrong? Bahati mbaya enzi za dot.com too late habari zishasambaa sana tu na nakala nyingi ziko mitaani.

Bahati nzuri wajanja tulishaserve copy.

Blog mbalimbali nako wanaweka limit hiyo?

Gazeti la Mwanahalisi leo hata online limefungiwa nini maana halifunguki. Kazi kweli kweli.
 
Mkandala, umeshaona aliyeumwa na nyoka huogopa hata kamba ya kufungia kuni?
Kweli nimewaona wengi lakini hii sii kazi yao kuwinda nyoka, huenda tu kukata kuni msituni.. Unamkumbuka yule bingwa wa Australia alokufa kwa kuchomwana mkia wa stingrays alivyokuwa akicheza na Nyoka?..basi wapo wenye kiburi kama yule usisahau ndio profession yao sasa.
 
Nilijizuia kwa muda mrefu kuingia kwenye mjadala huu kwa kuwa nilihisi hauna tija. Kwangu ulionekana kama mjadala uliotengenezwa kuchukua nafasi ya maswala muhimu yaliyokuwa yanajadiliwa humu mtandaoni. Binafsi namheshimu Zitto na naafikiana naye kuwa anao uwezo wa uongozi na haki ya kugombea. Pengine hofu yangu ni namna anavyoutaka huo Uraisi. Mimi nahisi ameanza vibaya. Kwa kuwa nafasi anayoitafuta ni ya kitaifa angejikita kwenye ajenda za kitaifa zaidi na kuacha kuonekana kama anayetetea vikundi vya watu wachache waliosahauliwa (mathalani watokao pembezoni mwa nchi - e.g. Kigoma, Waislamu na Vijana). Anaweza asiwe ametamka hayo matatu lakini ushahidi wa kimazingira ndivyo unavyoonyesha. Kwa kadri muda unavyopita hoja hizo zinaweza zisiwe na nguvu kabisa. Watanzania wana uzoefu wa watu waliokuja na hoja kama hizo na wakaaminiwa kupewa nafasi ya Uraisi na wakashindwa vibaya kutimiza matarajio ya wapiga kura.
Lakini ningependa Zito unijuze jambo moja linalonitatanisha. Unafikiria kugombea Uraisi kwa vile unadhani ‘chama chako’ cha CHADEMA hakina mtu bora zaidi yako anayeweza kukubalika kwenye nafasi ya Uraisi kwenye uchaguzi ujao? Kama una jambo unalolifahamu juu ya kutofaa kwa aliyekiletea ushindi mnono ‘chama chako’ uchaguzi uliopita huu ungekuwa wakati mzuri wa kutujuza. Kwa sababu mimi kwa ujinga wangu nilidhani ushindi mkubwa wa Chadema katika nafasi ya raisi uchaguzi uliopita ulitokana na mvuto na uwezo binafsi wa Dr Slaa katika kupanga hoja na kumdhibiti mpinzani wake mkuu kutoka CCM. Katika kufanya tathmini ya uchaguzi katika vikao vyenu vya ndani hamkulibaini hilo? Wewe Zito binafsi unakubaliana na dhana hiyo? Huoni kwa kumweka pembeni mtu kama huyu unaweza kuporomosha idadi ya kura za uraisi za chama chako uchaguzi ujao? Kwani nafasi bora kwako ni uraisi tu? Mimi binafsi natambua uwezo wako mkubwa na wala si wazo baya kufikiria kugombea nafasi kubwa kama hiyo. Lakini kwa namna unavyoutaka uraisi kwanza unahatarisha mshikamano wa chama chako, pili unawaweka njiapanda baadhi ya wale waliokuona kuwa ni jembe la kutegemewa kuuondoa ufedhuli unaofanywa na chama kisichotaka kujirekebisha kilichoko madarakani, na tatu unaviza vuguvugu la mabadiliko lililokuwa limeanza kushika kasi lililoanzishwa na ‘chama chako’. kama ulivyosema mwenyewe uraisi utakuja kwa wakati wake. Hakuna haja ya kuuharakisha. Usipokee kila ushauri. Kuna watu wanataka kutumia umaarufu wako kubeba hoja zao. Nakutakia kila la heri
 
Kweli nimewaona wengi lakini hii sii kazi yao kuwinda nyoka, huenda tu kukata kuni msituni.. Unamkumbuka yule bingwa wa Australia alokufa kwa kuchomwana mkia wa stingrays alivyokuwa akicheza na Nyoka?..basi wapo wenye kiburi kama yule usisahau ndio profession yao sasa.
Mkuu kmsingi sipingi ZITTO kuutaka urais,Lakini naomba unijibu kama ana nia nzuri kwann hashiriki katika ujenzi wa CHADEMA? Huon hapa kuna mashaka mkuu?
 
Hili sio kosa lka Ziutto ni kosa la kimfumo la chama kuwa na viongozi wa chama ambao pia ni Wabunge, mawaziri kivuli na halafu pia sijui ni majumbe wa mabaraza ya bunge..Hawa watu miungu?.. kusema kweli niliyasema haya long timme hapa JF mkaniijia juu kwa sababu nimemsema Mnyika japokuwa sikuwa na maana mbaya.

Muundo wa Chadema ktk uongozi ngazi ya chama sii mzuri na kushinda kwa wabunge wetu wengi hadi kushika nafasi ya Upinzani imekuwa mzigo ambao viongozi wote hawauwezi.. Sii Zitto, Mbowe wala Mnyika wote wame elemewa, mimi naona vijana wa Bavicha wasiokuwa wabunge wanaifanya kazi zaidi kuliko uongozi wa juu - Utanisamehe ni mtazamo wangu.
 
Nimekuelewa mkuu,Shauri japo kwa kifupi wafanye nini,kwan muda uliobaki ni mchache na maeneo ya vijijini bado ha2oni nguvu ya CHADEMA na huku ndio mtaji mkubwa wa kura ulipo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom