Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Moses Mashalla, Arusha na Boniface Meena, Dar | Mwananchi | Oktoba 06, 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amekitikisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa hatua yake ya kutangaza kuwania urais 2015, baada ya mwasisi wake, Edwin Mtei kumuonya kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

Kauli hiyo ya Mtei imekuja siku chache baada ya mbunge huyo kutangaza kwamba hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.

Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 umekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Alisisitiza kwamba siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini akasema kuwa ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza.

“Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.

Huku akimwagia sifa mbalimbali Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, Mtei alisema kwa upande mwingine, Katiba ya Tanzania kwa sasa, inamnyima Zitto sifa za kuwania urais mwaka 2015 kwa kuwa hadi kufikia mwaka huo atakuwa amefikisha miaka 38, huku Katiba ikielekeza kuwa mgombea urais anatakiwa awe na miaka isiyopungua 40.

Alipoulizwa ya kwamba endapo uchaguzi mkuu ujao utafanyika huku Watanzania wakiwa na Katiba Mpya iliyopunguza umri wa kuwania urais, Mtei alisema endapo mbunge huyo atapambana kuhakikisha umri huo unapunguzwa, basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia.

“Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri.”

Zitto apinga
Akizungumzia kauli hiyo ya Mtei, Zitto alisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

“Namheshimu Mtei kama mmoja wa waasisi na mwenyekiti mwanzilishi wa chama. Chama chetu kimekua na kina uwezo wa kuhimili demokrasia ya ndani,” alisema Zitto akiongeza kuwa miaka 20 tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, nchi inastahili kuimarisha vyama kidemokrasia.

“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.

Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”

Septemba 26, mwaka huu Zitto alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais mwaka 2015, alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliofanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200. Miongoni mwa maswali hayo lilihusu tetesi kwamba anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Katika majibu yake Zitto alisema: “Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge… mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii.

“Nimefanya kazi kubwa katika ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka 10.

“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola.

“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndiyo msimamo wangu. Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.

”
Alipoulizwa kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa Katiba alijibu: “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndiyo maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika Katiba Mpya.”

My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.

Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.

Yaani hilo ndio typical "pepo" la upandikizi wa ki-CCM linavyochemka ndani ya Zitto Kabwe!....Na hapo ndio utapata majibu kuwa kwa nini Zitto hawezi kuaminiwa kupewa madaraka yeyote makubwa ndani ya CHADEMA. Na bila shaka CHADEMA hawatofanya hilo kosa hata siku moja, otherwise itakuwa ndio kiama yake.

Kwa upande wa uongozi wa CHADEMA wameamua kudili naye kwa kutumia hekima, busara na werevu wa kupindukia. Na kwa hilo nausifu safu nzima ya uongozi kwa hilo. Wameamua kumpuuza Zitto kwa staili ya "mwana mjinga na asiye na adabu" na wameonelea iwapo wataamua ku dili naye kwa staili "kula naye sahani moja" itawavuruga zaidi. Lakini dawa ya Zitto inachemka kwani ifikapo 2015 utakuwa wakati mwafaka wa CHADEMA kama chama KUPIMA na KUAMUA hatima ya mahusiano yake na Zitto Kabwe.
 
NI kweli nakubalina na wewe kabisa ni family Kama vile mtoto ni mjumbe wa nec bagamoyo mama ni mjumbe wa nec mtwara na baba ni mwenyekiti wa Chama kwi! Kwi! Kwi! Kwi

Lakini nahisi hayo ayafanyayo Zitto ni kusudi kama ametumwa na kundi la watu kuharibu Chadema baada ya kujaribu njia zote kushindikana. Napata kuyaamini mawazo yangu 75% kama nia yake hiyo anahakika hawezi shinda hivyo huo ni mpango kamili kwa maana Tanzania bado aliyetayari kumkomboa Mtanzania. Ila Tuombe Mungu atutetee TUMECHOKA WATANZANIA MUNGU tunaomba turehemu. Kwani anayoyafanya sasa na tuliyosikia huko nyuma yanathibitisha mashaka kuwa halisia.
 
naufuta mchango wote wa Zitto katika akili yangu.... he does nothing at all... that how nnimeanza kumchukulia toka sasa... anachefua!
 
Unadhan Kamati kuu itampinga mtei wakat mkwe wao? huyo mzee hana lolote anataka mwanae akae ikulu sasa anaona zito ndo kikwazo chama cha familia na serikal mnataka ya family...pumzka we mzee mda wa vijana huu...zito kamua baba
Husiwe na mawazo mgando kama umezaliwa baada ya kifo cha Mwl Nyerere (R.I.P) unaweza kutamka maneno hayo, kumbuka wakati Mwl alipokuwa hai CCM angalau kulikuwa na nidhamu kidogo kwa sababu mambo mengi ya hovyo yule mzee alikuwa anakemea kutokana na hekima zake na waliokuwa na heshima katika chama walimsikiliza na kumtii na mambo yakaenda vizuri, kwa hiyo kauli ya Mzee Mtei haitakiwi kudharauliwa yule mzee anaheshima yake katika chama. na unatakiwa ukumbuke CCM imefika hapa ilipo baada ya kudharau nasaha na maelekezo kutoka kwa wazee waliopo hai na bahati mbaya baada ya kupoteza wengine kusababishiwa umauti.
 
alisema Zitto.

***Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... "Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu***

Haya maneno aliyotamka ZZK yana ukweli ndani yake au ni kutamka tu kwa Nadhalia ili tumuelewe kasema lakini ndani ya moyo wake hataweza kutekeleza kivitendo kwani sio muadilifu hana umoja kwani hameshindwa hata kuwa na umoja na viongozi wake ataweza kuwaunganisha watanzania, uwezo upi alionao kazi yake ni kufichua ubadhirifu wa serikali ya CCM ili ajipatie umaarufu na fedha lakini result 0 - 10%.
 
Hili neno "CHADEMA hakuna makundi" sijui ni kwanini linang'ang'aniwa sana na wajenga hoja wanaoamini kuwa ni wao pekee wanaitetea CHADEMA. Au wao hudhani makundi maana yake ni "wavunja chama"? Makundi kwenye vyama ni lazima ni kama vile maji kwa samaki!!

Mkuu kuna watu hawataki kusikia kwamba CDM kuna makundi. Hakuna kusanyiko la watu lisilokuwa na makundi. Hata familia ina makundi itakuwa chama cha siasa?
 
Watu wengine wakishapata umaarufu kidogo na kusifiwa na watu mbalimabli, basi wanajidanganya kuwa wanaweza kufanya kila kitu. Urais sio kitu cha kukimbilia. Kwa mtu makini natafikiria mara mbili kabla hajatoa tamko lolote kuhusiana na nia yake kutaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Nchi hii imejaa wasiasa uchwara ambao wanafikiria urais tu na kusahau matatizo ya msingi ya wananchi. YOU CAN BE A HERO WITHOUT EVEN BEING A PRESIDENT OF A COUNTRY. Jifunzeni kwa watu kama askofu Demond Tutu. Kwani kuwatumikia watu na kuleta mabadiliko mpaka uwe rais wa nchi?
 
Zito anajidanganya sana,aache kuropoka,anakuwa kama hajaenda shule!,subiri muda ufike utangaze nia yako,sasa hivi jenga chama kwanza.

Nia ya huyu jamaa wala sio huo urais kitu anachotaka ni kukivuruga chama
 
mtei atoe tamko lingine, kuna katibu wa bavicha tanga katangaza nia ya urais.
Nafasi ya mkwe wake mbowe inazidi kuwa hatarini.
 
Mwanamume huwa na kauli 1 tu.

kauli gani?
Ile ilikuwa maalum kwaajili ya zitto tu.
Au hawa wengine hawaogopi?
Haoni wanamvurugia mkwe wake mipango ya kuingia magogoni?
 
Wema kamshindwa ataiweza CHADEMA,poleni na njaa za madaraka.Sasa si muda wa kuteua mgombea urais tulien mbona mna haraka kama mmebanwa na tumbo la kuhara!
Mbona Dr ameshindwa kumfuga Rose Timamu,believe me kama hatogombea au akishindwa urais Josephine nae atatembea.
 
Mnafiki ni wewe namba moja.Mbona wewe umejificha na ID feki ya TUKO.Wewe ndiye mchochezi namba moja unayetaka tukiona mtu anavuruga chama tuogope kusema pole sana.Kama wewe sio mnafiki ungeanza kusema wewe ni nani? Kutumia majina halisi si hoja BTW unaweza kutumia majina halisi huku ukiwa na ID feki hata kumi.Huenda wewe ni mmoja wao na ninabishana na mtu mwenye ID hata kumi.
Usidhani kila mtu anayetetea ustaarabu ndani ya chama amepewa vijivyeo hapo CDM na wala usidhani kila mtu ana njaa kama ulivyo.
Unataka kunifundisha namna ya kutoa maoni hapa JF.Pole sana na umekosea sana.
Watu tuna uchungu na demokrasia na tunachelea kuona watu wachache wakigeuza demokrasia kuleta fujo.
Kwanini usimshauri huyo kipenzi wako asiwe mstaarabu kwa maslahi ya chama? Kwanini asiwe kama Mnyika au January Makamba? Kwani akifuata ushauri wa wazee wake ndani ya chama huo mwaka 2015 haitafika? Lazima sisi wengine tumwambie NO punguza spidi,jenga chama kama wenzako,tulia kama wenzako halafu kipenga kikipulizwa chukua fomu.Hapa kuna kosa gani? Hapa kashambuliwa au kaambiwa ukweli?
Ninakushangaa wewe TUKO unayeona swahiba wako kaonewa kwa kufundishwa ustahimilivu wa kisiasa.
Narudia tena kukuonya usitake kuchagulia watu cha kujadili hapa JF.Hakuna sheria yoyote iliyovunjwa,LAU kama kuna sheria nimevunja nishtaki kwa MODS wanifungie kwa sababu umeonyesha wewe ni dikteta mkubwa usiyependa kuona Swahiba wako akiguswa.Mtu mnafiki na mzandiki anajulikana tu kwa maneno yake kama wewe unayeshambulia mleta mada badala ya kujadili mada yenyewe.Huo ni uwendawazimu!
Samwel Sitta alisema mwanasiasa ni lazima uwe na ngozi ngumu sasa kama mnalalamika hivi kwa kuhoji tu matendo yenu kwa nia njema je,tukiwapa Urais mtaweza?

Tumia japo 10% ya akili yako dogo kabla ya kububujikwa mapovu. Ukisoma contents za posts zangu (nyingi nimeandika kwa kiswahili), hakuna mahali ambapo nimesema namuunga mkono Zitto wala kauli zake. Msimamo wangu dhidi yenu wachache mnaoutumia kauli za Zitto kumfarakanisha na sisi wanachama. CDM imekuwepo tangu wewe unavalishwa nepi, haijawahi kuvurugwa na chochote wala yeyote, sembuse kauli za Zitto?!!! Nakuuliza tena, Mbowe, Slaa, Said Arfi, Lissu, Mnyika na wengine wamezisikia kauli za Zitto but wamakaa kimya, kama zingekuwa kauli za kuvuruga chama, unadhani chama kingeshindwa kumnyamazisha? Tumeshanyamazisha wangapi, tushindwe kumnyamazisha Zitto, kama anahatarisha maslahi ya chama?.
Zitto katumia haki yake kikatiba kutoa maoni yake kuwa ataomba kugombea uraisi 2015 kupitia CDM, nini cha ajaaabu hapo kukuto mapovu? Katibu wa BAVICHA Tanga nae kasema atagombea uraisi 2015, kwa nini ulalamike? Let them express their wills and we, members will rule by our wills..
Mbona ni akili ndogo sana inahitajika hapa kufanya 'political tolerance' Molemo ?
 
Last edited by a moderator:

Umeonyesha wazi upeo wako ni Negative.Siku zote mtu mjinga hujadili mtoa mada na si mada yenyewe.Kama huyo jamaa yako asingekuwa amesababisha chochote kungekuwa na mjadala unaoendelea sasa hivi kwenye media? Au hiyo habari ya mwananchi niliandika mimi?
Kuonyesha upeo wako ulivyo mdogo unasema sisi wengine tusishtuke na kuonya hii hali eti mpaka Mbowe,Slaa,Arfi na wengine waseme.Sasa nikuulize unadhani kauli ya Mzee Mtei haina maana yoyote? Umenikejeli eti wakati CDM inaanzishwa mimi nilikuwa sijavalishwa nepi kweli mjinga hana rangi kwenye uso.Sasa huyo Mtei si ndiye Mwasisi wa hiyo CDM mnayemkejeli na kumtukana kwenye mitandao leo? Angekuwa na tabia kama hiyo yenu mliyo nayo leo kweli CDM ingekuwepo?
Bado nasimama kwenye msimamo wangu kwamba DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
 
Last edited by a moderator:
Nia ya huyu jamaa wala sio huo urais kitu anachotaka ni kukivuruga chama
Chama akiwez kuvurugika kwa Zitto kutanga nia ya kugombea Urais coz Mtei amesema chama kinataratibu zake na kama atakosa Sifa nakula za awali si anaendelea kuwa mwanachama shida ipo wapi?Ila kusema nia yake si mapema ila wana kigoma watafute atakaye wafaaaa
 
Umeonyesha wazi upeo wako ni Negative.Siku zote mtu mjinga hujadili mtoa mada na si mada yenyewe.Kama huyo jamaa yako asingekuwa amesababisha chochote kungekuwa na mjadala unaoendelea sasa hivi kwenye media? Au hiyo habari ya mwananchi niliandika mimi?
Kuonyesha upeo wako ulivyo mdogo unasema sisi wengine tusishtuke na kuonya hii hali eti mpaka Mbowe,Slaa,Arfi na wengine waseme.Sasa nikuulize unadhani kauli ya Mzee Mtei haina maana yoyote? Umenikejeli eti wakati CDM inaanzishwa mimi nilikuwa sijavalishwa nepi kweli mjinga hana rangi kwenye uso.Sasa huyo Mtei si ndiye Mwasisi wa hiyo CDM mnayemkejeli na kumtukana kwenye mitandao leo? Angekuwa na tabia kama hiyo yenu mliyo nayo leo kweli CDM ingekuwepo?
Bado nasimama kwenye msimamo wangu kwamba DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
Nidhamu gani ww unataka?Na demokrasia ina mruhusu kugombea urais,inachotakiwa cc kama CDM tuangalie kijana anasifa za kupeperusha bendera yetu ya kugombea urais 2015?
 
Umeonyesha wazi upeo wako ni Negative.Siku zote mtu mjinga hujadili mtoa mada na si mada yenyewe.Kama huyo jamaa yako asingekuwa amesababisha chochote kungekuwa na mjadala unaoendelea sasa hivi kwenye media? Au hiyo habari ya mwananchi niliandika mimi?
Kuonyesha upeo wako ulivyo mdogo unasema sisi wengine tusishtuke na kuonya hii hali eti mpaka Mbowe,Slaa,Arfi na wengine waseme.Sasa nikuulize unadhani kauli ya Mzee Mtei haina maana yoyote? Umenikejeli eti wakati CDM inaanzishwa mimi nilikuwa sijavalishwa nepi kweli mjinga hana rangi kwenye uso.Sasa huyo Mtei si ndiye Mwasisi wa hiyo CDM mnayemkejeli na kumtukana kwenye mitandao leo? Angekuwa na tabia kama hiyo yenu mliyo nayo leo kweli CDM ingekuwepo?
Bado nasimama kwenye msimamo wangu kwamba DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.

Kama kweli una nia njema katika kauli zako, rudisha ile summary ya topic uliyopost mwanzo kabisa kabla ya kuiondoa na kuacha habari ya gazeti peke yake.
Mtei kaongea vizuri sana, kidiplomasia, na kwa hekima kubwa aliposema "Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri."
Kwa sababu unazojua wewe, mwanzoni ulikuwa umesema eti Mtei kasema kama Zitto atapambana kufanya marekebisho ya katiba yaondoe kipengele cha umri "atakuwa mbinafsi na mwenye uroho wa madaraka". Usidhani kwamba mzee Mtei hakujua kutumia maneno ya hivyo, bali alitumia akili kuhakikisha maoni yake hayamu'attack' Zitto. Kuna tofauti kubwa sana kati ya maneno "itaonekana kuwa" na "atakuwa' kwenye context ya diplomaisia. Mzee Mtei hakuongelea kuwa Zitto atakuwa mroho wa madaraka...

Pili, gazeti limeandika ..."Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga"... Kwa sababu unazojua wewe ukaandika eti; ...Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara lakini kijana huyo amekuwa "mkaidi na asiyesikia"...

Narudia tena, mimi siungi mkono kauli za Zitto kutangaza nia kugombea uraisi. Hata hivyo bado namwona Zitto kuwa ni capable and potential leader wa CDM na nchi, sasa na baadae, kama ilivyo kwa Slaa na Mbowe. Kauli zake hizi ambazo hajazitoa kwa nia mbaya, zisitumiwe na maadui wake kisiasa wachache, kutuvuruga CDM kwa kutufarakanisha na viongozi wetu na kusema eti CDM kuna makundi.
Kwa heri Molemo, na sitakujibu tena.
 
Last edited by a moderator:
Mshauri mkuu wa chadema ndugu, Kitila Mkumbo alitembelea Uingereza katika miji ya London na Readings kuanzia tarehe 5 Machi na 6 Machi 2012 na kuondoka tarehe 10 Machi, 2012. Miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kati ya Freeman Mbowe na Dk. Slaa.Mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo. Wanaomuunga mkono Dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko Mbowe lakini pia kwamba Dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo Dk. Slaa anaweza kuwa Rais ajaye. Kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa Mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao. My take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015.Source: Nilikuwa Uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu Kitila. HUU UZI UNAUKUMBUKA????
Kwa tamaa hii ya akina Zitto na Mbowe nina imani CCM itarudi madarakani. Nawashauri wanachadema wakae chini na kufikiri hivi Mbowe na Dr. Slaa nani anapendwa na wananchi wengi. Tusijidanganye mvuto wa wananchi kwa sasa ni kwa kazi anayoifanya Dr Slaa. Mkiamua kumuaweka pembenni jua mnatwanga maji kwenye kinu. Urais agombee Dr. Slaa na si vinginevyo
 
Kama kweli una nia njema katika kauli zako, rudisha ile summary ya topic uliyopost mwanzo kabisa kabla ya kuiondoa na kuacha habari ya gazeti peke yake.
Mtei kaongea vizuri sana, kidiplomasia, na kwa hekima kubwa aliposema “Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri.”
Kwa sababu unazojua wewe, mwanzoni ulikuwa umesema eti Mtei kasema kama Zitto atapambana kufanya marekebisho ya katiba yaondoe kipengele cha umri "atakuwa mbinafsi na mwenye uroho wa madaraka". Usidhani kwamba mzee Mtei hakujua kutumia maneno ya hivyo, bali alitumia akili kuhakikisha maoni yake hayamu'attack' Zitto. Kuna tofauti kubwa sana kati ya maneno "itaonekana kuwa" na "atakuwa' kwenye context ya diplomaisia. Mzee Mtei hakuongelea kuwa Zitto atakuwa mroho wa madaraka...

Pili, gazeti limeandika ..."Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga"... Kwa sababu unazojua wewe ukaandika eti; ...Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara lakini kijana huyo amekuwa "mkaidi na asiyesikia"...

Narudia tena, mimi siungi mkono kauli za Zitto kutangaza nia kugombea uraisi. Hata hivyo bado namwona Zitto kuwa ni capable and potential leader wa CDM na nchi, sasa na baadae, kama ilivyo kwa Slaa na Mbowe. Kauli zake hizi ambazo hajazitoa kwa nia mbaya, zisitumiwe na maadui wake kisiasa wachache, kutuvuruga CDM kwa kutufarakanisha na viongozi wetu na kusema eti CDM kuna makundi.
Kwa heri Molemo, na sitakujibu tena.

Afadhali sasa akili yako imerudi na umejadili hoja badala ya mleta hoja.Hivyo ndivyo GT anapaswa kuwa.Kwa vyovyote vile unaweza kubadili maneno kwa namna yeyote unayotaka kusema ili tu kulainisha maneno lakini jibu moja liko very clear kwamba Mwasisi wa chama Edwin Mtei hajauma maneno na amepeleka ujumbe sawia hata kama ni mchungu kwamba Huu ni wakati wa kujenga chama na si wakati wa kugawa wanachama.Na kwa kauli ya kifasihi ni wazi Mzee wetu Mtei hayuko mbali na kauli yangu kwamba DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom