Exactly, hiyo maana yake ni "Art" aka sanaa.
maana naona kila mtu anajaribu tu kukumbatia mbuyu.sawa chemichemi ya maji utadhani yamekwisha kumbe yapo zaidi ya uliyochota
Exactly, hiyo maana yake ni "Art" aka sanaa.
Tangu aondoke mamlakani mmefanya nini kusahihisha mnachodhania ni makosa yake? Mbona mambo yanazidi kwenda kombo Tanzania wakati wazungu wanachota maliasili zetu? Mbona sijawasikia Wakenya wakimlalamikia Kenyatta licha ya kwamba aliwapandikizia ukabila na kuchukua ardhi yao? Mbona wenzetu wamesonga mbele? Mtaendelea kulalamika juu ya Nyerere mpaka lini? Tumia akili au show us a better way forward, you moron.kama mambo yakuvunjavunja baraza la mawaziri na sekta zingine yeye ndio muanzishaji mkuu,sasa utasemaje alikuwa kiongozi imara na hasiyeyumba.Hapo tulipo,hisa za nyerere zinahusika{tena sana},halishindwa kuhakikisha uwajibikaji mbele na urafiki nyuma.
Kwanza halileta umaskini,uadui sisi na nchi zingne za africa i.e uganda,kwasababu ya ushkaji wake yeye na OBOTE.
Nyerere nikiongozi aliyekuwa na mapungufu mengi mno,bali watu walikosa pakusemea.Wapi KAMBONA,ABOOD JUMBE,KOLIMBA....
Christopher Kassanga Tumbo was arrested in Kenya in 1963 for opposing the East African Federation proposal. He was returned to Tanganyika and held in detention for four years.
Kuhusu Joseph Kasella Bantu ninachokumbuka mimi ni kuwa alikuwa anampinga Nyerere na aliwekwa ndani kwa kuamrisha mapigano ya watu kuibiana ng'ombe kule Nzega. Bahati mbaya taarifa zake hazijaandikwa, lakini hili nalikumbuka.
Ukweli ni kuwa Nyerere alikuwa hapendi sana kubishiwa kitu. Alikuwa anawaadabisha wale waliompinga kwa kutumia sheria ile ile ya Preventative Detention Act waliyokuwa wanatumia wakoloni. Pamoja na mabaya yake yote Nyerere hakumuua yeyote wala kumuacha mtu aozee detention na wala hakuwa na lukuki ya watu walioswekwa detention.
Nyerere wa Wikipedia atabaki kuwa wa hukohuko. Nyerere wa WATANZANIA, tulieishi naye, tukafanyakazi naye, tukamsoma, tukamsikiliza, akafariki, tukamzika atabaki kama tulivyomwona na kumfahamu.
Tatizo ni kuwa tuna kundi kubwa la jamii ambalo halioni kuwa Nyerere alikuwa ni mkosa na makosa yake yanahitaji kusahihishwa! ni muhimu kwanza Watanzania wakubaliane kuwa alikuwa ni mkosa na makosa yake yalikuwa ni yapi ili baada ya hapo ndio waweze kuendelea, lakini wakati unamwambia mwenzako hili ni kosa yeye anakwambia "baba wa taifa" kasema hivi au hakutaka hivi! hili ujue ni tatizo ambalo linahitajika kufutwa kwanza.Tangu aondoke mamlakani mmefanya nini kusahihisha mnachodhania ni makosa yake? Mbona mambo yanazidi kwenda kombo Tanzania wakati wazungu wanachota maliasili zetu? Mbona sijawasikia Wakenya wakimlalamikia Kenyatta licha ya kwamba aliwapandikizia ukabila na kuchukua ardhi yao? Mbona wenzetu wamesonga mbele? Mtaendelea kulalamika juu ya Nyerere mpaka lini? Tumia akili au show us a better way forward, you moron.
Tumekuwa na viongozi watatu ambao wote ni anti-Nyerere. Mwinyi, Mkapa, na Kikwete. Kipi kimewashinda kufanya, kama waliweza kufuta azimio na kuondoa maadili ya uongozi, kubadilisha sera za Nyerere? Kipi kimemshinda Kikwete kuunga mkono uwepo wa serikali tatu? CUF iliunga mkono serikali tatu lakini nasikia sasa baada ya ndoa yake na CCM wanataka serikali mbili. Alaumiwe Nyerere? Haya, tukishakubali kuwa Nyerere alifanya makosa ndipo tutapiga hatua mbele? Mbona kama vile nchi inarudi nyuma? Nyerere alishauri madini yasichimbwe mpaka Watanzania watakapokuwa na uwezo lakini akina Mkapa/Kikwete wakajiona wajanja wakawapa wazungu mbuga za madini na kuwafukuza raia wetu kwa mtutu wa bunduki. Alaumiwe Nyerere pia? Tumekumbatia ubepari bila kujipanga na leo tunawaona wazungu, eti mnawaita wawekezaji, kuwa wakombozi wetu. Tumlaumu Nyerere hapo? Naweza kuendelea on and on lakini ukweli unawasuta wale waliopo madarakani hivi sasa na ninyi mnaowaunga mkono kwamba uongozi wa sasa umeshindwa na unataka kujificha nyuma ya kisingizio kuwa Nyerere alifanya makosa.Tatizo ni kuwa tuna kundi kubwa la jamii ambalo halioni kuwa Nyerere alikuwa ni mkosa na makosa yake yanahitaji kusahihishwa! ni muhimu kwanza Watanzania wakubaliane kuwa alikuwa ni mkosa na makosa yake yalikuwa ni yapi ili baada ya hapo ndio waweze kuendelea, lakini wakati unamwambia mwenzako hili ni kosa yeye anakwambia "baba wa taifa" kasema hivi au hakutaka hivi! hili ujue ni tatizo ambalo linahitajika kufutwa kwanza.
Mfano mmoja mdogo tu ni suala la Serikali tatu ndani ya muungano, rekodi zinaonyesha kuwa wabunge au bunge ambalo kwa siasa za Tanzania ndilo linalopitisha sheria zao, lilikuwa likielekea kukubali kuanzishwa kwa serikali tatu, lakini Nyerere akaingilia na kutia mkono wake kuwa hili yeye halitaki! na kama sikosei alikuwa tayari aameshastaafu wakati huo! yeye ni nani? Tanzania ni ya kwake?
Sasa kama bunge kweli linakubali kuwa lile lilikuwa ni kosa la Nyerere kwa nini hawalirekebishi na kufuata matakwa ya wawakilishi wa wananchi ya kuwepo serikali tatu katika muungano? watakwambia kwa sababu "baba wa taifa" alikuwa halitaki hili!
Juzi mtumishi wa taasisi ya juu ya kiserikali ndio alitoa mpya na kali pale alipojibu kuwa Nyerere alikitoa kipengele cha dini katika sensa kwa sababu alioteshwa na mungu! huyu ni mwakilishi wa serikali na msomi anasema hivi! hapo ujue kuwa kuna tatizo kubwa jasusi.
Umetolea mfano Kenya na Kenyatta wenzetu wanakubali kimaneno au kivitendo kuwa Kenyatta alikuwa na makosa, isitoshe makosa ya Kenyatta yanaweza kuhesabika, lakini Nyerere?!
Yote hayo yanaangukia kwenye msingi alioucha Nyerere, kumbuka kuwa ni Nyerere au Nyerereism iliyowapatia Tanzania hao viongozi uliowataja.Tumekuwa na viongozi watatu ambao wote ni anti-Nyerere. Mwinyi, Mkapa, na Kikwete. Kipi kimewashinda kufanya, kama waliweza kufuta azimio na kuondoa maadili ya uongozi, kubadilisha sera za Nyerere? Kipi kimemshinda Kikwete kuunga mkono uwepo wa serikali tatu? CUF iliunga mkono serikali tatu lakini nasikia sasa baada ya ndoa yake na CCM wanataka serikali mbili. Alaumiwe Nyerere? Haya, tukishakubali kuwa Nyerere alifanya makosa ndipo tutapiga hatua mbele? Mbona kama vile nchi inarudi nyuma? Nyerere alishauri madini yasichimbwe mpaka Watanzania watakapokuwa na uwezo lakini akina Mkapa/Kikwete wakajiona wajanja wakawapa wazungu mbuga za madini na kuwafukuza raia wetu kwa mtutu wa bunduki. Alaumiwe Nyerere pia? Tumekumbatia ubepari bila kujipanga na leo tunawaona wazungu, eti mnawaita wawekezaji, kuwa wakombozi wetu. Tumlaumu Nyerere hapo? Naweza kuendelea on and on lakini ukweli unawasuta wale waliopo madarakani hivi sasa na ninyi mnaowaunga mkono kwamba uongozi wa sasa umeshindwa na unataka kujificha nyuma ya kisingizio kuwa Nyerere alifanya makosa.
Sideeq,Yote hayo yanaangukia kwenye msingi alioucha Nyerere, kumbuka kuwa ni Nyerere au Nyerereism iliyowapatia Tanzania hao viongozi uliowataja.
Narudia tena ni muhimu kwa Watanzania wakubali kuwa Nyerere alikuwa ni mkosa ili waweze kuendelea, lakini wakibakia kuwa Mwalimu kasema, Mwalimu hakutaka, Mwalimu kaoteshwa basi ujue kuwa hakuna maendeleo yoyote yatakayo patikana.
Sawa lakini inaonyesha kuwa ingawa umeiondoka CCM lakini hujauondoka Unyerere (hutaki kukubali kuwa alikuwa ni mkosa, zaidi ya kutaka kuonyesha kuwa alikuwa na makosa madogomadogo hapa na pale), kama ningekuwa mimi ni CHADEMA ningekuwa mwangalifu sana na watu wa aina yako.Sideeq,
Mimi ni fan mkubwa wa Nyerere. Lakini sasa hivi nimejiunga na Chadema kwa sababu naamini wana vision ya way forward. Chadema hatukai tunalalamika kuwa Nyerere alifanya hivi alifanya vile. Tunatambua mchango wake kwa taifa na hata pale alipoteleza. Lakini tuna vision ya kuliondoa taifa letu kwenye ufisadi uliokithiri. Tuna vision ya kumrudishia Mtanzania fahari na matumaini nyumbani kwake. Tuna vision ya kuona Mtanzania anafaidika na maliasili zake na si mzungu au mwarabu. Tuna vision ya kuona hospitali zetu zinatoa tiba nzuri kwa kila mtanzania na shule zetu zinapata nafasi ya kutoa elimu bora kwa kila mtanzania bila kujali katoka familia ya nani. Ninyi endeleeni kulalamika kuwa Nyerere alitufanyia hiki alitufanyia kile, sisi tunachanja mbuga kutafuta Tanzania bora kwa kutaka vizazi vyetu na vile vijavyo.
Sawa lakini inaonyesha kuwa ingawa umeiondoka CCM lakini hujauondoka Unyerere (hutaki kukubali kuwa alikuwa ni mkosa, zaidi ya kutaka kuonyesha kuwa alikuwa na makosa madogomadogo hapa na pale), kama ningekuwa mimi ni CHADEMA ningekuwa mwangalifu sana na watu wa aina yako.
Ameondoka mamlakani literacy rate ikiwa 85%. One of the best in Africa. Leo nasikitika kusikia watoto wanaomaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika. Mama yangu mzazi kajifunza elimu ya ngumbaro enzi za uhuru na kufikia wakati mauti inampata aliweza kusoma Biblia na kuandika mwenyewe. Leo kuna genge la anti-Nyerereist wanakuja na ngonjera za ajabu.Nakereka sana mnavyomjadil nyerere vibaya. Hv nyerere si alitoa elimu ya bure kwa baba zenu?na kulikuwa hamna shule za st w2 wote walisoma shle za serikal na elimu ilikuwa bora kuliko sasa. For me Nyerere ni mtu ambaye ametufanya tuish bila udin,ukabila wala rang. Naamin kila mtu anamapungufu yake lkn nahs mnamkosea sana mungu kwa kumsema Nyerere vibaya.
Mtakatifu Nyerere... Hizi nyimbo mkawaimbie watoto wa chekechea...Nyerere the Saint, the Holy father, Baba wa Taifa blah blah ...
jmushi1, Mkuu wangu sasa nadhani unataka kudadisi zaidi ya kutaka kufahamu kwa sababu tayari umeshaweka majibu kichwani.mkuu hapo kwenye misikiti kunyimwa vibali una uhakika napo mkuu?Maana naona unazungumzia kama ni tatizo sugu.Na kama hilo likiwa tatizo,je ni sheria gani inayokataza kujenga msikiti Tanzania?Kama kuna viongozi individuals ambao kwa utashi wao kinyume na sheria za nchi wamefanya hivyo,then kuna hatua za kuchukua dhidi yao.Mkuu wangu si misikiti tu,we unajuwa jinsi ambavyo wananchi wote kwa ujumla wanateseka na matendo ya viongozi ya unyanyasaji.Ebu niambie mkuu wangu kwenye taifa la rushwa kama letu,unataka kuniambia pesa ikitembezwa hayo hayafanikishwi?tuongelee reality ya taifa letu bila politics za dini.Hakuna kitu kinashinda pesa kwa viongozi na serikali be it musilam ama mkristo.Sheria zinavunjwa left right.
mkuu "wengine" pamoja na mimi tunakuelewa kwenye mambo mengi tu.Na kama nimeshindwa kukuelewa hapa,haina maana kwamba sikuelewi mara zote.jmushi1, Mkuu wangu sasa nadhani unataka kudadisi zaidi ya kutaka kufahamu kwa sababu tayari umeshaweka majibu kichwani.
Unapomkatalia mtu jambo lolote kinyume cha sheria ndio sababu ya kuwepo madai ya Mfumo Kristu.. Tunasema, Tanzania kuna Ufisadi hakuna mahala kisheria kunaporuhusu Ufisadi lakini imekuwa sehemu ya maisha yetu na hivyo wanyonge wanapolalamikia uongozi huwezi kuwauliza tena wao maswali bali unatazama malalamishi yao na jinsi gani utaweza kuzuia badala ya kuwaambia wao waliomba tender wakanyimwa?.
Labda nikurudishe ktk muafaka wa MoU inakuwaje wakristu walirudishiwa shule zao na hata kuwa sehemu ya mipango ya maendeleo ya elimu na Afya nchini wakanyimwa nafasi hiyo Waislaam na dini nyinginezo. Halafu mkiulizwa mtasema kwani waislaam mliomba mkanyimwa wakati toka mwanzo ilikuwa kinyume cha katiba na sheria. Viongozi wote wanakuwa hivyo walivyo kutokana na mfumo mbaya wa uongozi na utekelezaji ama laa yasingetokea. Majibu kama haya tunayasikia kwa kina Mkapa na uongozi wote ulofuatia ni udadisi na dharau kwa aina fulani.. CDM wanalalamikia mfumo wa uchaguzi, ufisadi mkubwa lakini ukisikia maneno ya wana CCM unashindwa kuelewa kama kweli tunatafuta kupata mfumo bora ama ni uhuni tu unatakiwa maana maswali yao ni kama yako hutaki kufahamishwa ila unayo majibu kichwani kama Nape Mnauye. Nimechoka mkuu wangu nadhani wengine wanmenielewa vizuri zaidi na ndio sababu ya kuwepo hapa JF..
Ukiritimba, ubwana, umimi wote huu hutokana na system iliyopo hivuyo kama waislaam wanalalamika sioni sababu ya wewe kuendelea kutetea mfumo uliopo ambao wewe kwa mtazamo wako pia unaulalamikia. Na mwisho wa mjadala huu nadhani umeonyesha wazi jinsi gani wanavyokwamba kutokana na watu kama nyie mnaotaka sana kutafuta mchawi wakati vitu viko wazi kabisa..Na binafsi yangu sijawahi kuhoji wla mkuuliza mipango yyote ya maendeleo ya wakristu isipokuwa pale inapowakwaza waislaam kama vile muafaka wa MoU lakini maajabu ya Mungu nyie wenyewe pamoja na kuona ukiukaji wa Katiba lakini bado ni watetezi wakubwa wa kanisa.
Ili nyumba iwe imara inabidi iwe na msingi mzuri...
Mwanzilishi wa Taifa letu ni nani??
Yeye ndiye aliyetuwekea misingi ya Taifa letu...
[h=1]You can fool all the people some of the time and some of the people all the time but you cannot fool all the people all the time[/h]
Narudia tena ni muhimu kwa Watanzania wakubali kuwa Nyerere alikuwa ni mkosa ili waweze kuendelea, lakini wakibakia kuwa Mwalimu kasema, Mwalimu hakutaka, Mwalimu kaoteshwa basi ujue kuwa hakuna maendeleo yoyote yatakayo patikana.
ukweli unauma.....
Nyelele arikuwa mtu mzuli sana, wakati wa Nyelele aliimalisha sana hari ya watu wake kierimu na rishe bola, vyakura kama mahalage
mchere, sukali, virikuwa vikipatikana kira kona ya Jamhuli ya Tanzania