Upotoshaji Wikipedia Juu ya Nyerere?

Upotoshaji Wikipedia Juu ya Nyerere?

Hamna shida nieleze nakusikiliza kuhusu hizo ibada.Kama mtu haelewi si unamwelewesha mkuu wangu?orodhesha hizo ibadq ili twende straight to the point instead of beating around the bushes.

Huo mfano wa Vatican nimekuelewa,lakini sina mfano wa jambo kama hilo lilotokea.Kama limetokea si haki kabisa.Lakini nipatie mfano ili nichanganye na zangu.Je una maanisha kwamba serikali ya JK imezuia msaada kwa waislam kwasbabu hauna maslahi/faida na wakristo?

Naomba niingilie huu mjadala MUshi, hebu nikuulize, kwaini wakristo wa tanzania WANAPIGA KELELE SANA SERIKALI KUINGIA OIC? ukinijibu hilo nadhani utapata jibu hapo juu
 
Hawa walipotelea wapi Tanganyika au Zanzibar? Tanzania bara au Tanzania Visiwani?

NANI ALISABABISHA VIFO VYA WATU HAWA? kabla hawajakabidhiwa Zanzibar inasemekana walikuwa huku Tanzania bara, nani alisababisha vifo vyao?
 
Ama bora waulizeni hawa
  • kambona
  • mapalala
  • kasanga tumbo
  • fundikira
  • bibi titi
  • sheikh takadir
  • zakaria hanspope
  • kassim hanga-huyu alimuonesha jangwani paleeeee......akapelekwa znz asubuhi hajulikani alipo hata kaburi
  • othman sharif nae huyu..alikamatwa hapa dar akaoneshwa hadharani..judgemnt ikapitishwa hapo na nyerere asubuhi karume znz akatekeleza hukuma..nae hajulikani kazikwa wapi
  • mohamed shamtee...aliekuwa waziri mkuu wa znz kabla ya mapinduzi...kapinduliwa znz..kafia jela za tanganyika
  • mamia ya waliopoteza maisha yao kuhamishwa kwa nguvu kwenda 'gezaulole"
  • unyanganyi wa nyumba za watu binafsi hata kama ulikua na mkopo\
  • unyanganyi wa mashamba ya watu binafsi
  • unyanganyi wa mashule ya binafsi na taasisi za dini
  • kuhusu propaganga ya uhujumu wa uchumi watu walinyanganywa pesa na mali zao na wengine kutiwa ndani...wengine kweli walipoteza maisha...lengo ni kupoteza mawazo ya watu...kwamba hajashindwa kuendesha nchi na uchumi ila kuna wachache ndio wanahujumu
  • vita vya uganda ..lengo kumrudisha rafiki yake obote....ni nyerere ndie aliemshawishi obote aende Singapore kuhudhuria mkutano wa commonwealth na huku Amin akampindua..hivyo alitaka kumrejesha
  • mamia watiwa ndani wakati alipomwachisha jumbe urais wa znz
  • alipeleka wa tz biafra kufa katika vita kwa hisia za ukatoliki
  • 1982 vijana walio choka na utawala wake waliteka ndege ya ATC kumlazimisha kujiuzulu kutokana na kushindwa kuendesha nchi....walipewa hifadhi huko London.....
kwa vijana wengi hawajui haya..wao wanao soma zaidi propaganda....

HAlafu ndio aitwe mtakatifu, umesahau kumention wazee wa Kariakoo walotiwa ndani miaka ya 1967/68 LAA'NA BABU YULE !!!! wamemkaribisha halafu amewatia ndani ALLAh AWAREHEMU WAZEE WETU
 
Enzi hizo mapinduzi yalikuwa nje nje, viongozi wa kiafrika walitumiwa sana na mabeberu kuangusha tawala za viongozi waliokuwa wanaonekana hawataki kuendeleza unyonywaji wa nchi zao. Siku hizi hakuna mapinduzi kama ya enzi zile kwa sababu viongozi wengi ni vibaraka vya wanyonyaji, wanatumika kuwakandamiza wananchi wao na hata kuwa peleka mabwepande wale wote wanaowapinga.

NYERERE alifanya maamuzi magumu kwa nia njema na faida ya Taifa, sio hawa wa sasa wanao cheka na mafisadi wenzao. Tungepata Hu Ji Tao nchi hii ili tunyonge wezi wa taifa hadharani. Tukipoteza watu kumi tukaokoa maelfu elfu hakuna dhambi!
 
NANI ALISABABISHA VIFO VYA WATU HAWA? kabla hawajakabidhiwa Zanzibar inasemekana walikuwa huku Tanzania bara, nani alisababisha vifo vyao?
Hivi mkuu OIC stands for Organization Of Islamic Countries"?tuanzie hapo...
 
Hamna shida nieleze nakusikiliza kuhusu hizo ibada.Kama mtu haelewi si unamwelewesha mkuu wangu?orodhesha hizo ibada ili twende straight to the point instead of beating around the bushes.

Huo mfano wa Vatican nimekuelewa,lakini sina mfano wa jambo kama hilo lilotokea.Kama limetokea si haki kabisa.Lakini nipatie mfano ili nichanganye na zangu.Je una maanisha kwamba serikali ya JK imezuia msaada kwa waislam kwasbabu hauna maslahi/faida na wakristo?
Unaona sasa hujanijibu isipokuwa umezungusha.. Swali rahisi kabisa nimekuuliza lakini umetafuta njia ya kutokea. Mkuu wangu swala lolote linalohusu mahusiano baina ya wakristu wakatoliki na vatican sisi Waislaam , Protestant au Pentakosti hatutakiwi kuingilia ibada yao na serikali inatakiwa kuwalinda wakatoliki ktk ibada yao... Vivyo hivyo kwa dini na madhehebu mengine yote Unless ibada hiyo itakiuka Uhuru waliopewa kikatiba na ama kuingilia uhuru wa watu wengine.. Je unajua ya kwamba ni kazi kubwa sana kwa Msikiti kujengwa hata kijijini (kupewa Kibali) kuliko kanisa kujengwa mjini tena katikati ya residential areas? Wakristu na sio serikali watataka kujua fedha zimetoka wapi, nani kazitoa na tuna mahusiano gani lakini haiwi hivyo upande wa pili. OIC, Mahakama ya kadhi, serikali kutuwekea kadhi mkuu, Bakwata yaani mbona mengi sana na tunarudi kule kule....
 
Hivi mkuu OIC stands for Organization Of Islamic Countries"?tuanzie hapo...
jmushi1 what a name stand for does not count isipokuwa what they wonna do. Anyway, maana yake haswa ni Organisation of Islamic Cooperation sijui unataka kujua nini zaidi? Hivi Jmushi akitaka kujenga msikiti kama alivyofanya Nyerere (mkristu) waislaam wanatakiwa kuuliza jina la Mushi lina maana gani?
 
Ndugu yangu, tumia akili kidogo. Ian Smith was not an angel. He was on the opposite side of Nyerere. For him, an evil man, to call the other person, of a different persuasion evil, means that Nyerere was no evil. Ni kama vile shetani akuite wewe shetani, kwa sababu hakubaliani na msimamo wako. Sasa hapo shetani ni nani?

Jasusi,

..nakwambia mtandao una kazi huu??

..yaani mtu anakuja hapa anam-quote Ian Smith!?

..Ian Smith aliyetuma madege kwenda kushambulia kambi za wakimbizi with napalm bombs?
 
jmushi1 what a name stand for does not count isipokuwa what they wonna do. Anyway, maana yake haswa ni Organisation of Islamic Cooperation sijui unataka kujua nini zaidi? Hivi Jmushi akitaka kujenga msikiti kama alivyofanya Nyerere (mkristu) waislaam wanatakiwa kuuliza jina la Mushi lina maana gani?

Mkuu wangu uelewa wa wananchi ni wataofauti kabisa.Kama unajuwa uelewa wetu ni shida,basi hutapata shida kuona watu wa imani nyingine wakitilia mashaka kwasababu tu ya jina la OIC.Hilo la Cooperation nimejuwa leo,tuendelee kuelemishana.Mwanzoni nilidhani hiyo "c" stands for countries.

Mifano mingine ulonipa sijakupata labda uende straight to the point kwamba nani alizuia nini na kwanini,na mimi niweke input yangu kama Mtanzania.
 
NANI ALISABABISHA VIFO VYA WATU HAWA? kabla hawajakabidhiwa Zanzibar inasemekana walikuwa huku Tanzania bara, nani alisababisha vifo vyao?
Unauliza jibu? Kwani Zanzibar si watu? Walikabidhiwa kwa Wazanzibari wenzao ambao walisababisha vifo vyao.
 
Mtakatifu wanini? kufunga watu magerezani, kuua au kusababisha vifo kama vya Hanga ? kuwaweka watu wake kwenye folen ya kugombea sukari robo kilo, kuwafanya watu wavae MAKATAMBUGA , viatu vya matairi, kusababisha rushwa tanzania tuliyo nayo leo hii kwa kuwabana watu wasiendelee kwa kutuletea ujamaa na kujitegemea? kwa lipi hasa mtu huyu aitwe mwenye heri, angekuwa mwenye heri mwanawe mtiifu angemfanyia aliyomfanyia??? MY FOOT !
Katika dini yetu Paulo ni mtakatifu. Lakini aliua wafuasi wa Yesu mpaka alipopofushwa na mwanga na akabadilika kuwa mtetezi mkubwa wa Yesu. Waliofungwa magerezani wakati wa Nyerere hawakuwa na hatia? Ulitaka awapongeze na kuwatuza kwa kuvunja sheria? Your foot for real!
 
NANI ALISABABISHA VIFO VYA WATU HAWA? kabla hawajakabidhiwa Zanzibar inasemekana walikuwa huku Tanzania bara, nani alisababisha vifo vyao?

Swali juu ya swali sasa inasaidia nini? Mi sijui nani aliyehusika na wapi walipopotelea watu unaowasema.
 
Mkuu wangu uelewa wa wananchi ni wataofauti kabisa.Kama unajuwa uelewa wetu ni shida,basi hutapata shida kuona watu wa imani nyingine wakitilia mashaka kwasababu tu ya jina la OIC.Hilo la Cooperation nimejuwa leo,tuendelee kuelemishana.Mwanzoni nilidhani hiyo "c" stands for countries.

Mifano mingine ulonipa sijakupata labda uende straight to the point kwamba nani alizuia nini na kwanini,na mimi niweke input yangu kama Mtanzania.
jmushi1, mkuu wangu hata ingekuwa Countries bado hii ni ibada ya waislaam (kwa yale wanayotaka kuyafanya) kama vile Vatican wavyo saidia wakristu ktk nchi mbalimbali pasipo kupitia ubalozi wake. Ujenzi wa kmakanisa na shule unafanywa na Vatican sio serikali ya Vatican na Waislaam hawawezi kulalamika ama kutaka kujua neno Vatican lina maana gani na inawakilisha watu gani..Hii kweli tutafika?

Halafu kama nilivyosema, muda wote huu sisi waislaam tunatumia kuwafahamisha nyie (wakristu) wakati sii hoja yenu, wala hatukutakiwa kuwafahamisha maana hamtaelewa ibada zetu isipokuwa serikali ndio inatakiwa kulinda uhuru tulokuwa nao, Sasa jiulize kwa nini mnataka kuelewa ibada za waislaam kwanza? Je mna mashaka gani na Waislaam wa Tanzania ambao hawaulizi lolote kutoka Vatican hata pale Pope anapopewa heshima za Kitaifa! Hizi hizi tabia za wakristu kufuatilia kila la Waislam na serikali nyuma yao ndio maana tunasema kuna mfumo kristu maana kila chenu kinapitishwa bila kuhojiwa lakini sio cha Waislaam lazima wapate opinion kutoka kwenu. Why can't we just trust each other? au kuna historia ya waislaam kutumia vibaya fursa hizi?
 
mkuu kama ikiwa "nchi", kwa uelewa wa watanzania wengi ambao hawashei imani hiyo,lazima kutakuwa na "raised eyebrows"Na serikali haiwezi kujiingiza kwenye miungano inayohusiana na dini.Na wasiokuwa na dini si watanzania?
Niambie ni muungano gani tulionao na jumuiya ya mataifa ya kikristo na serikali yetu?ni kwasababu kama Taifa tumekuwa na tabia ya kutokujishughulisha kufikiri na kupambanua tunabugia tu.Mkuu wangu mimi nisikufiche mimi ni mwafrika mtanzania period.Ningekuwa kwenye nafasi ya kuangalia na kuchagua ni nani tuungane naye nk.Nitayafanyia uchunguzi madhumuni yao.Kama hayo mataifa ya kiislam yanataka kuwasaidia ndugu zao waislam ni lazima waiingize nchi nzima ama serikali?na maddhumuni yake ni nini?Daima mimi ni mtanzania na kamwe sitoyumbishwa na imani tulizoletwa,be it ukristo ama usilam.
 
Unaona sasa hujanijibu isipokuwa umezungusha.. Swali rahisi kabisa nimekuuliza lakini umetafuta njia ya kutokea. Mkuu wangu swala lolote linalohusu mahusiano baina ya wakristu wakatoliki na vatican sisi Waislaam , Protestant au Pentakosti hatutakiwi kuingilia ibada yao na serikali inatakiwa kuwalinda wakatoliki ktk ibada yao... Vivyo hivyo kwa dini na madhehebu mengine yote Unless ibada hiyo itakiuka Uhuru waliopewa kikatiba na ama kuingilia uhuru wa watu wengine.. Je unajua ya kwamba ni kazi kubwa sana kwa Msikiti kujengwa hata kijijini (kupewa Kibali) kuliko kanisa kujengwa mjini tena katikati ya residential areas? Wakristu na sio serikali watataka kujua fedha zimetoka wapi, nani kazitoa na tuna mahusiano gani lakini haiwi hivyo upande wa pili. OIC, Mahakama ya kadhi, serikali kutuwekea kadhi mkuu, Bakwata yaani mbona mengi sana na tunarudi kule kule....
mkuu hapo kwenye misikiti kunyimwa vibali una uhakika napo mkuu?Maana naona unazungumzia kama ni tatizo sugu.Na kama hilo likiwa tatizo,je ni sheria gani inayokataza kujenga msikiti Tanzania?Kama kuna viongozi individuals ambao kwa utashi wao kinyume na sheria za nchi wamefanya hivyo,then kuna hatua za kuchukua dhidi yao.Mkuu wangu si misikiti tu,we unajuwa jinsi ambavyo wananchi wote kwa ujumla wanateseka na matendo ya viongozi ya unyanyasaji.Ebu niambie mkuu wangu kwenye taifa la rushwa kama letu,unataka kuniambia pesa ikitembezwa hayo hayafanikishwi?tuongelee reality ya taifa letu bila politics za dini.Hakuna kitu kinashinda pesa kwa viongozi na serikali be it musilam ama mkristo.Sheria zinavunjwa left right.
 
Mi nadhani ukifuatilia baadhi ya wachangiaji utagundua kuwa wana chuki na UPINZANI, UKRISTO na NYERERE nadhani katikati hapa pana shida ilitokea. nadhani mtu aliye smart anajua jinsi ya kuishi na watu mbalimbali na hugeuza changamoto zote kuwa fursa. Africa bado tunadhaurika bila kujitegemea hata tujiunge na organisation gani katu hatuwezi kuwa kama wao. let us love our countries and be proud of whonwe are unless tunarudi utumwani.
 
zomba nimeamini kuwa upeo wa wengi hapa Jf ni mdogo sana....
Fatilia utaona zaidi ya watu 20 wananikosoa Kiswahili changu.....kisa nini???? nimewaudhi
kwenye jina la Nyerere nimeandika Nyelele......hawahoji kwa nini nimeandika uongo kuwa Mwalimu aliimarisha elimu na kulikuwa na neema ya chakula, kaazi kweli kweli

Nimekusoma Boflo na niliona ile stihizai uliowafanyia na nikajuwa wengi wataingia kichwa nikakaa pembeni natazama unavyowarundika.

Nyelele huwa hawaachi kufanya makosa na kuandika Nyerere lakini hawakosei kuandika Safali na Omali arisema.
 
Mi nadhani ukifuatilia baadhi ya wachangiaji utagundua kuwa wana chuki na UPINZANI, UKRISTO na NYERERE nadhani katikati hapa pana shida ilitokea. nadhani mtu aliye smart anajua jinsi ya kuishi na watu mbalimbali na hugeuza changamoto zote kuwa fursa. Africa bado tunadhaurika bila kujitegemea hata tujiunge na organisation gani katu hatuwezi kuwa kama wao. let us love our countries and be proud of whonwe are unless tunarudi utumwani.

Ni nini alichozuliwa ambacho si cha kweli? Jee, Nyerere hakuweka hiyo sheria ya "detention" na kawaweka watu ndani kwa maelfu kwa hiyo sheria na wengine hawajulikani mpaka leo wako wapi toka waliporundikwa "detention". Au ni kipi unachokiona wewe kuwa hiki Nyerere anazuliwa?
 
ulikuwepo wakati huo?

Nashkuru Mungu nilikuwepo wakati nchi hii bado ipo chini ya Umoja wa Mataifa na inatawaliwa na Malkia wa Uingereza. Nilikuwepo kabla Nyerere hajawa Waziri Mkuu, na kabla hajawa Rais, nimeanza kusoma kabla ya hii nchi kuwa Tanzania, nimeziona neema na matatizo yaliokuwepo kabla ya kupewa madaraka nimeona neema tulizobaki nazo baada ya kupewa madaraka, nimeona jinsi Nyerere alivyo "abuse" madaraka na kuwa dikteta, nimeona jinsi Tanganyika ilivyotolewa kwenye neema na kuwa maskini wa mwisho duniani (mpaka nikaikimbia nchi), nimeona mabadiliko baada ya kuondoka Nyerere, katika uongozi wa Mwinyi, nimeona uongozi wa Nkapa na Nashkuru sasa nauishi uongozi wa Kikwete.

Namshukuru Mungu kuniweka hai na kushuhudia, kula na kunya katika awamu tano za uongozi wa nchi hii: Malkia, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete.

Wewe umeanza kuwepo na kujijuwa kuwa upo kuanzia awamu ya nani?
 
Back
Top Bottom