Upo hapa kwa muda mfupi sana

Upo hapa kwa muda mfupi sana

Kiroho, kucheza kwa jicho la kulia kunawakilisha kuchochewa kwa nishati ya vitendo, maono ya mbeleni, na ulinzi. Jicho lako kucheza tangu jana ni ishara kwamba nafsi yako ipo macho na inajaribu kuhisi mambo yaliyofichika katika ulimwengu wa roho kabla hayajadhihirika kimwili.
Bado nipo njiapanda ni ishara nzuri au mbaya kaka
 
Binadamu wanashindwa kuishi maisha marefu kuliko miti, kuna miti ilipandwa karne ya 20 ipo mpaka sasa haijachoka. Mfano ni ile miembe ya Unyanyembe Tabora. Sijui ni kwa nini graph grouth ya binadamu ni fupi na hufikia ukomo haraka kuliko miti
 
wanadamu ni mafupi na yenye mahangaiko mengi, na hakuna jipya chini ya jua.

Hapo utaona mambo matatu Mwanadamu, Maisha, na Mahangaiko.

Tumesema hapo juu kuwa maisha ni mafupi sana, kwa uzoefu mdogo utaona kuwa umepitia utoto, baadaye ujana, na huenda kwa sasa wewe ni mzee. Kesho huenda ukawa marehemu.

Somo la Leo jifunze kuishi kwa kutumia ufahamu wako wa ndani, na elewa kuwa kila jambo linalokutokea lilipaswa litokee, na kuna somo fulani unajifunza. Usihukumu wala kulaumu kwa chochote.

Maisha ni mapito. Kila jambo lipo, na litapita.
Asante mkuu,
Na kingine ni kufurahia kazi za mikono Yako/juhudi zako.
Na je uwepo wako duniani umekuwa faida au khasara kwa wengine?
Vipi ukiwa tayari marehemu utakuwa na tofauti Gani na marehemu paka/mbwa?
Na ndio maana wazee walituambia wema hauozi
 
Unaishi miaka 70 au 80 then unakufa for eternity (millions to trillions years and infinite) maisha ya mwanadamu ni mafupi mno, kila muda unaopita haurudi kamwe, tuishi kwa upendo na amani kesho yetu hatuijui

Inasikitisha
 
Unaishi miaka 70 au 80 then unakufa for eternity (millions to trillions years and infinite) maisha ya mwanadamu ni mafupi mno, kila muda unaopita haurudi kamwe, tuishi kwa upendo na amani kesho yetu hatuijui

Inasikitisha
IMG-20260729-WA0061.jpg
 
One day you’ll realize that the people who genuinely loved you never asked you to become someone else just to deserve their love.
 
Maisha haya kweli ni ubatili tu...nakumbuka nimewai tamani kifo kuliko uhai nyakati fulani za magumu yangu...mbele ilikua ni giza tororo.
 
Hili somo murua sana. Nakumbuka wimbo wa kikosi cha mizinga unaitwa 'saa za kazi'. Kuna punch moja inasema "chochote unachofanya kifanye tena kwa uhakika". ni verse ya Hashim D kama sikosei...
 
wanadamu ni mafupi na yenye mahangaiko mengi, na hakuna jipya chini ya jua.

Hapo utaona mambo matatu Mwanadamu, Maisha, na Mahangaiko.

Tumesema hapo juu kuwa maisha ni mafupi sana, kwa uzoefu mdogo utaona kuwa umepitia utoto, baadaye ujana, na huenda kwa sasa wewe ni mzee. Kesho huenda ukawa marehemu. Kumbe upo katika mapito tu.

Hapa jifunze kuishi katika ukamilifu katika kila eneo. Mathalani, unapokuwa kazini, fanya kazi kwa shauku na upendo mkubwa. Kila siku ona kuwa ndiyo mara yako ya kwanza kufanya kazi hiyo.

Unapokuwa katika maeneo ya starehe, mathalani unaangalia mpira, unaangalia movie, unakunywa kinywaji, na kadhalika, fanya hivyo kwa upendo na furaha sana, wala usijilaumu kufanya hivyo, kwa kuwa ndiyo muda wake. Hutaweza kupata wasaa kama huo tena.

Kuna watu ambao huwa wanajilaumu sana kwa maisha yao ya nyuma. Utamwona mtu anajilaumu sana kwa kufuja fedha kutokana na matumizi mabaya ya fedha, mathalani kwa kununua magari ya kifahari na kujenga nyumba za kisasa, badala ya kufanya uwekezaji mkubwa wa mashamba na biashara. Lakini kumbe si kweli kuwa ukiwekeza sana ndiyo utafurahia maisha. Kila jambo lina wakati wake na nafasi yake.

Unapougua sana magonjwa makubwa na kubaki kitandani, tambua ni wakati wako sahihi wa kupata uzoefu huo wa magonjwa. Hivyo unapaswa kuendelea kushukuru sana, na ukishukuru, maana yake utapokea zawadi ya kupona.

Somo la Leo jifunze kuishi kwa kutumia ufahamu wako wa ndani, na elewa kuwa kila jambo linalokutokea lilipaswa litokee, na kuna somo fulani unajifunza. Usihukumu wala kulaumu kwa chochote.

Maisha ni mapito. Kila jambo lipo, na litapita.
Asante sana boss! Huwa tunajisahau sana na kuona kama tunaumiliki ulimwengu huu!
 
Back
Top Bottom