Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

Mazoea nayo yakizidi ni kero ingawa ni upendo.jaribu kukeep distance kidogo ili muheshiane pamoja na kuset standards zako
 
Jamani mimi mawifi zangu (dada wa mtarajiwa wangu) wananitatiza. Mchumba wangu ni mtoto wa kiume pekee kwa wazazi wake na amebarikiwa madada sita. To be honest nawapenda mawifi zangu na wananipenda pia kwa maneno na matendo ila sasa upendo huu naona unaelekea kuwa mzito sana kwangu.

Mimi ni mwanamke simple sana. Mavazi na Hairstyle na muonekano wangu kwa ujumla ni simple. Sasa mawifi zangu tangu nimetambulishwa kwao wamekuwa ni watu wa kutaka kunibadilisha. Ninaletewa nguo, hereni, viatu na kila aina ya urembo ambao si kama ule ninaopendelea. Weekend lazima mmoja anitafute twende salon, tukifika huko nitalazimishwa mambo ya pedicure, manicure wakati sina mazoea hayo. Yani ni kama wamewekeana zamu, leo huyu kesho huyu. Mara shopping na tukifika huko sipewi uhuru wa kuchagua nivipendavyo bali naambiwa "wifi hii ndo itakupendeza bwana, tena hata kaka atapenda ukivaa hii".

Wiki iliyopita tulienda harusini mimi, mchumba wangu na dada zake wawili. Nikakutana nao mitaa ya Mwenge ili tuongozane kwenda huko. Nilikuwa nimevaa flat shoes na gauni langu la usiku. Jamani wifi zangu walilalamika kwanini nimevaa flat shoes kwa muda kama dakika 20 hadi baby ikabidi aseme mwacheni mke wangu. Leo wifi amenitag instagram kwenye picha ya viatu virefu ananiuliza kama nimevipenda. Sijajibu hadi sasa na najawa na hasira na mashaka kuwa endapo nikiolewa si watakuja kunipangia hadi nightdress za kumvalia mume wangu hawa..

Nifanye nini waniache alone bila kuwa na mtafaruku au wasijisikie vibaya kwani wananipenda na najua wanafanya kwa upendo na nafurahi kupendwa ukweni ila daaaaahhhh!
Mawifi zako wanatumia JF pia?
 
Yawezekana wana pretend kukupenda mtu yeyote akikupenda ikiwa rafiki au yeyote hukupenda kwa jinsi ulivyo they will never ask you to change
 
Be yourself, nilipata danga flani hivyo, dada yake aliwahi kuwa miss, yeye anafikiri urembo ni extension hair, nails, eyebrow na eyelashes. Hivyo vyote sikuviweza, mwisho wa siku alikubali kuwa siwezi kubadilika.
Duu danga=buzi!!!
 
Aisee mawifi weengi hao

Bt ushukuru Mungu wanakupenda

And nilicho ona wanataka uonekane tofauti kidogo.

Yan kuna design ya wif wanayo itaka sasa wanajaribu kukubadirisha

Ishi nao kwa akili sababu wanaweza kukugeuka wote.

Waambie tu or kama huwez mwambie huyo mtarajiwa kuwa yeye ndio anapenda ww uwe hivyo; ili awavunje moyo.

Ndio shida ya kuzaliwa mdada mmoja au mkaka mmoja ktk familia cz wanamuona jicho hilo
 
hahaha
Siku nyingine ukinimenshen hakikisha unanipa samare ya madiskashen...

Yaani nimeacha nyagi yangu nikajua unanipa habari pendwa kumbe mambo ya mawifi,. Narudia tena unimenshen siku JPM akinikumbuka kwenye ufalme wake.

Baada ya kusema hayo napenda kukufahamisha sijakumisi wala nini.

Ukimwona gfsonwin mwambie muda si mrefu ntammisi.
hahahahahhahahahahhhahahahhahahhaha mekumisss kama ngalalimo aseeee!
 
Upo kwenye ulimwengu huu my dear.Missing you so long sijakutana na comment yako.
Nilikua nalea mwaya!
nimekuza no merudi upyaa
naangalia mustakhabal humu daaah,nikiwaona hivi wala chumvi nyingi napata faraja kuwa am still at home!
miss you much much
ukimuona Kaunga Kongosho na kingasti wambie nao nimewamiss sana!
uko poa lakini?
home nini?
haya mwaya!
 
Nilikua nalea mwaya!
nimekuza no merudi upyaa
naangalia mustakhabal humu daaah,nikiwaona hivi wala chumvi nyingi napata faraja kuwa am still at home!
miss you much much
ukimuona Kaunga Kongosho na kingasti wambie nao nimewamiss sana!
uko poa lakini?
home nini?
haya mwaya!
Kongosho kwisha kazi yake, Zombie kamgeuza zomba. King'asti tia maji tia maji na Paw wake, Kaunga kawa "swala tano" ukimgusa tu anakutupia upako.

Hivi Wangoni bado wanapatikana Duniani!!
 
Hiyo familia imejaliwa upendo, mshikamano ndo mana wote wanafanana tabia na mapendeleo,.. Naona hapa wanafurahi kuongeza ndugu wa saba ambae ni wewe,kwa upendo wao hawakumcritisize kaka yao walipoona upo tofauti wanataka kukuweka kama wao,... Its like a new baby is born in their family,wazoee na uwapende pia unavyovipenda vaa, na visivyokuridhsha waambie wifi hiki sijakipenda sitakuwa comfortable na watakuelewa
 
Kaka yao alikupenda jinsi ulivyo na alijua fika kua kuna mabinti wanaojiremba zaidi yako ila alikupenda ww na sio hao wengine. Hao mawifi wanaona ww ni mshamba na kama unawaaibisha ndo maana wanajitahidi kukubadili ili na kaka yao aonekane ana sister duu ila you have to be yourself sababu wao sio waliokupenda ww.
 
Hiyo familia imejaliwa upendo, mshikamano ndo mana wote wanafanana tabia na mapendeleo,.. Naona hapa wanafurahi kuongeza ndugu wa saba ambae ni wewe,kwa upendo wao hawakumcritisize kaka yao walipoona upo tofauti wanataka kukuweka kama wao,... Its like a new baby is born in their family,wazoee na uwapende pia unavyovipenda vaa, na visivyokuridhsha waambie wifi hiki sijakipenda sitakuwa comfortable na watakuelewa
Shukrani sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom