Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

Wadada mma visa, mawifi wakiwachukia kwenu kero wakiwapenda kwenu kero, sasa mnataka wafanyaje??
 
Jamani mimi mawifi zangu (dada wa mtarajiwa wangu) wananitatiza. Mchumba wangu ni mtoto wa kiume pekee kwa wazazi wake na amebarikiwa madada sita. To be honest nawapenda mawifi zangu na wananipenda pia kwa maneno na matendo ila sasa upendo huu naona unaelekea kuwa mzito sana kwangu.

Mimi ni mwanamke simple sana. Mavazi na Hairstyle na muonekano wangu kwa ujumla ni simple. Sasa mawifi zangu tangu nimetambulishwa kwao wamekuwa ni watu wa kutaka kunibadilisha. Ninaletewa nguo, hereni, viatu na kila aina ya urembo ambao si kama ule ninaopendelea. Weekend lazima mmoja anitafute twende salon, tukifika huko nitalazimishwa mambo ya pedicure, manicure wakati sina mazoea hayo. Yani ni kama wamewekeana zamu, leo huyu kesho huyu. Mara shopping na tukifika huko sipewi uhuru wa kuchagua nivipendavyo bali naambiwa "wifi hii ndo itakupendeza bwana, tena hata kaka atapenda ukivaa hii".

Wiki iliyopita tulienda harusini mimi, mchumba wangu na dada zake wawili. Nikakutana nao mitaa ya Mwenge ili tuongozane kwenda huko. Nilikuwa nimevaa flat shoes na gauni langu la usiku. Jamani wifi zangu walilalamika kwanini nimevaa flat shoes kwa muda kama dakika 20 hadi baby ikabidi aseme mwacheni mke wangu. Leo wifi amenitag instagram kwenye picha ya viatu virefu ananiuliza kama nimevipenda. Sijajibu hadi sasa na najawa na hasira na mashaka kuwa endapo nikiolewa si watakuja kunipangia hadi nightdress za kumvalia mume wangu hawa..

Nifanye nini waniache alone bila kuwa na mtafaruku au wasijisikie vibaya kwani wananipenda na najua wanafanya kwa upendo na nafurahi kupendwa ukweni ila daaaaahhhh!

subiri kwanza uolewe ndio utajua unapendwa ama la, kwa sasa tulia tuliiiiiii. mm naona hapo mbeleni kuna moto mwingi usio uweza na kwa jinsi ulivyojionesha hapa unatakiwa ukaze kwelikweli. Hao wifi zako the way wanavyokupenda ujue na ukichukiwa ni spidi hiyohiyo. reversible reaction
 
hongera mama

umefanikiwa kutujaza wivu
sie wenye mawifi hawana hela

na mawifi dada binamu kutwa kupigana vikumbo kisa kaka yao kinyama cha hamu...
Hahahaha...pole shogaangu....
 
subiri kwanza uolewe ndio utajua unapendwa ama la, kwa sasa tulia tuliiiiiii. mm naona hapo mbeleni kuna moto mwingi usio uweza na kwa jinsi ulivyojionesha hapa unatakiwa ukaze kwelikweli. Hao wifi zako the way wanavyokupenda ujue na ukichukiwa ni spidi hiyohiyo. reversible reaction
I pray wasije kunichukia mkuu
 
Duuh mawifi zako wanakupenda sana, sijui coz ndo wifi mmoja tu waliyenaye!! Maana mabinti wengi ndo huwa wanajitahidi kweli kuwa-win mawifi zao, sio kwa yeye kuwanunulia mizawadi. (Unapalilia ndoa kwa mawifi teh)

Nimewaza tu hao mawifi zako wangekuwa na ghubu mbona ungesurrender mapema, mtu sita uwiii. Anyway unaweza tu kuongea nao kwa upole waambie kuwa umezoea kuwa tu simple mwenyewe, so hupendelei vikorombwezo vingi, slowly tu watakuelewa. Na wakati mwingine ukiona kuna ratiba ambazo watakuhitaji kwa kitu fulani na haupo willing, basi tafuta karatiba kengine ili mpishane. Yes mnapendana but freedom au choices za mtu ziheshimiwe pia, hupendi kitu fulani basi wakuelewe tu. Hongera mwaego, angalau leo umeleta story nzuri za mawifi
HAHAHA Huyo binti ana bahati kupata mawifi wa namna hiyo halafu kuna jambo haliweki wazi hasa aliposema yeye yuko "simple" pengine huo usimple watu wana mtazama kama yuko rough sana hasa mawifi zake hivyo wana jaribu kumuweka kwenye mstari.
sasa mshaurini achague jinsi ya kwenda nao sawa wasione kama ana wareject au achague kuanzisha vita ambayo baadae atashindwa.
Kama mawifi zake wanampenda hivi sidhani kama anaweza kushindwa kukaa nao kirafiki na wakaongea tuu kuwa haya nimeshindwa haya nayaweza lakini akianza kuwakimbia na kudindia lazima ataumia yeye.
Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume yuko tayari kupoteza ndugu au furaha ya ndugu kwaajili ya mwanamke.

Si bora yeye ana mawifi sita mimi akanana ana mawifi zaidi ya tisa...
 
Kwa uoga huo inabidi uzoee tu, kubali yote.
Ila kama unataka mabadiliko na future ya ndoa yako fanya marekebisho kuhusu mienendo yako.
Inaonyesha si Mtu mwenye msimamo katika masuala yako pengine ndiyo maana imekuwa rahisi
kutaka kukuweka wao wanavyoona inafaa.

Umeshawahi kujiuliza ex wa Mchumba wako alikuwa ni Mtu wa aina gani?
Unazijua "variety" za Mchumba wako? Life style ya familia ya Mchumba wako?
mabadiliko hayaji bila maumivu akitaka mabadiliko anatkiwa kuwa makini sana kwenye hili maana anaweza akajikuta ametangaza vita ambayo niwazi hatoiweza.
 
I pray wasije kunichukia mkuu

muombe MUNGU sana, mawifi wanakuwa wachungu sana katika ndoa za watu wengi, sio mjini wala vijijini. na mtihano mkubwa kwako ni kwamba wana kaka 1 utu amabaye ndo huyo mumeo mtarajiwa. Alafu wewe hujaolewa kwenye harusi za watu unafwata nini?? Ukija kupigwa kibuti maumivu yake yachanachana hadi nywele zako. Kaa nyumbani utulie kiherehere chako sio kizuri hata kidogo.
 
HAHAHA Huyo binti ana bahati kupata mawifi wa namna hiyo halafu kuna jambo haliweki wazi hasa aliposema yeye yuko "simple" pengine huo usimple watu wana mtazama kama yuko rough sana hasa mawifi zake hivyo wana jaribu kumuweka kwenye mstari.
sasa mshaurini achague jinsi ya kwenda nao sawa wasione kama ana wareject au achague kuanzisha vita ambayo baadae atashindwa.
Kama mawifi zake wanampenda hivi sidhani kama anaweza kushindwa kukaa nao kirafiki na wakaongea tuu kuwa haya nimeshindwa haya nayaweza lakini akianza kuwakimbia na kudindia lazima ataumia yeye.
Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume yuko tayari kupoteza ndugu au furaha ya ndugu kwaajili ya mwanamke.

Si bora yeye ana mawifi sita mimi akanana ana mawifi zaidi ya tisa...
Asante kwa ushauri mzuri
 
muombe MUNGU sana, mawifi wanakuwa wachungu sana katika ndoa za watu wengi, sio mjini wala vijijini. na mtihano mkubwa kwako ni kwamba wana kaka 1 utu amabaye ndo huyo mumeo mtarajiwa. Alafu wewe hujaolewa kwenye harusi za watu unafwata nini?? Ukija kupigwa kibuti maumivu yake yachanachana hadi nywele zako. Kaa nyumbani utulie kiherehere chako sio kizuri hata kidogo.
Kiherehere tena...This is my official fiancee, harusi early september hivyo mimi tayari ni part ya familia. Na sioni tatizo mimi kwenda harusini kama plus one wa mchumba wangu. Ni katika kujuana vizuri zaidi.
 
*NANI KAKUZUIA KUJIPAMBA, EBU JIPAMBE DADA... JIPAMBE UWE MREMBO ZAIDI*

Leo nataka kuwatia moyo wanawake kwa habari ya kujipamba, jipambe ili mpendeze mwaya.......

Najua zipo saloon nyingi zenye hadhi mbalimbali na zina wataalamu wa viwango tofauti tofauti lakini nimegundua saloon moja haihitaji gharama kubwa sana kama unataka kupambwa.

Nilikuwa napita mahali nikaiona, nikasema lazima niwashauri wanawake waende hiyo saloon wakajipambe na haipo mbali. Unakubalije kukaa bila kujipamba na wakati umeruhusiwa?

Mwanzoni nilipoiona hii saloon nilishtuka nikaambiwa, usishtuke .........nikauliza kwanini? Nikaambiwa...... _*Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwatii waume zao*_1Pet 3:5

Nikauliza walitumia mapambo gani hao wanawake wa zamani? Akasema; _*Wanawake wa zamani walijipamba kwa mapambo yasiyoharibika yaani roho ya upole na ya utulivu*_ 1Pet 3:4 Nikasema.... Kumbe kuwa na roho ya upole ni pambo! Kumbe roho ya utulivu ni pambo!

Mapambo adimu sana haya kwa wanawake wengi siku za leo. Mapambo haya hayapatikani saloon za kawaida bali ndani ya Bible pekee.
Dah !!!I love it !

Ili kujua mtu ana roho ya utulivu ni pale yanapotokea mazingira ya tafrani, misukosuko. Ukiona mwanamke unatokea msukosuko kidogo tu kwenye ndoa yake, halafu anaenda kumtangaza mumewe nje vibaya, ukiona hivi ujue huyu hajapambwa huyu. Unatembea barabarani kumbe unanuka, udhaifu wako wote umeshatolewa nje na hujui.

Na ili kujua mwanamke ana roho ya upole ni pale mazingira yanapokuwa ya fujo, kelele na vimbwanga. Ukiona mwanamke mkali kiasi kwamba mume hajisikii kuwahi nyumbani ujue huyu mwanamke kakosa pambo huyu.

Wanawake jipambeni kwa mapambo hayo jamani, ni mapambo yasiyoharibika yanadumu, hata ukinyeshewa mvua hayabanduki, wanaume/waume zenu wanatamani kuwaona wake zao wakijipamba kwa mapambo hayo.

Lipsticks, Brazilian Hair, Expensive shoes, Expensive dresses, Manicure, Pedicure, Mascara, Eyeshadows....etc haya yanaharibika, hayafai kwa binti za Mungu. Jipambe kwa roho ya upole na utulivu ili uwe mrembo rohoni binti ya MUNGU.

*MUNGU KWANZA!!!*
 
Kiherehere tena...This is my official fiancee, harusi early september hivyo mimi tayari ni part ya familia. Na sioni tatizo mimi kwenda harusini kama plus one wa mchumba wangu. Ni katika kujuana vizuri zaidi.
 
hongera kwa mawifi wengi na wenye upendo
waeleze upendacho na usichopenda
Nimekuwa nikishangazwa na comment za huu uzi eti mawifi sita ni wengi...!
 
Waambie kisilencer
ANZA KUWANUNULIA UNAVYOPENDA!
ANZA KUWATAMBULISHA AINA YAKO YA MAISHA
ANZA KUZUNGUMZA KUHUSU INTEREST ZAKO
ANZA KUSHARE NAO HOBBIES
RECOMEND OUTINGS,WHERE TO EAT WHERE TO SHOP WHOTO CALL UKITAKA VISIMPLE!
story za aina hiyo!
waonyeshe picha zako mkiwa na kaka yao akiwa very happy!
GIVE THEM UR LIFE PROFILE WATAJIUDJUST NAWE UTAJIUDJUST KIDOOOOGO MTAPATA BOOOOONGE LA BLEND!
pengine wao aina yao ya kuonyesha kupenda ni kununua vitu vya thamani!
waonyeshe kuwa mtu anaweza kukupenda na kukuonyesha anakupenda even by spending a quality time with u!
MTAJIFUNZA PAMOJA !
HALAFU MAISHA YATAKUWA POOOOOOOOA!
sio mbaya kihivyo as wangekuwa the opp wa hivyo walivyo,SITA,eenenehhehehehhe MAJI UNGEITA MMA!
Asprin Kaizer na platozoom kama dada zenu wako hivi muwambiage na nyie!
chaaaa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom