P olisi wafanya maandamano inchi nzima kufikisha ujumbe wa CHADEMA kwa wanainchi.
Kumbe polisi wananguo nzuri za sare zao huwa wameziweka tu majumbani, nimefanya mawasiliano nchi nzima nimeambiwa jeshi la polisi liko stand bay , liko barabarani likifanya doria kudhibiti maandamano ya wafuasi wa CHADEMA ambao wangeandamana leo.
Ofisi zote za CHADEMA zimezingirwa na magari ya ngarandinga ya FFU wakiwa wamavalia sare zao safi teyari kukabiliana na lolote litakalotokea. Ofisi za CHADEMA Mtwara maeneo ya chikongora karibu na soko kuu zimezingirwa, Masasi maeneo ya uwanja wa fisi kuna polisi kibao, Kasulu ofisi za CHADEMA ziko Kigoma Kibondo road karibu na nyumba ya Gorofa ya Ndituye zimezingirwa ,Tanga ofisi za CHADEMA ziko mabanda ya papa zimezingirwa. Mpwapwa ofisi za CHADEMA ziko maeneo ya stand ya zamani zimezingirwa. Dodoma maeneo yote ya barabara inayochepuka toka barabara kuu itokayo Dar kwanda maeneo ya ukumbi wa bunge kuanzia CBE wapo polisi na magari yao, mbwa na farasi ,hapapitiki wamefunga njia, kwenye ofisi za CHADEMA mkoa karibu na FOTS kuna gari za ngarandinga zipatazo 10. Kigoma maeneo yote ya Mwanga, mnarani hadi Ujiji ni polisi tupu.
Wanainchi wanajiuliza kuna nini leo? Wanajibiwa na wenzao kwamba Polisi wanazuia maandamano ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA wanaotarajia kuandamana kupinga bunge la katiba kuendelea kufuja hela za walipa kodi bure.
Kwa mwenendo huu wa polisi wamekisaidia chama cha CHADEMA kufikisha ujumbe wa CHADEMA kwa wanainchi bila wao kujua, kwa maneno mengine Polisi ndiyo imefanya maandamano ambayo yangefanywa na CHADEMA kupinga matumizi ya ovyo ya raslimali za wanainchi yanayofanywa na bunge la katiba.
Ama kweli Polisi watu uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, wanafanya kazi kubwa namna hii ya CHADEMA bila wao kujua.