Updates za yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA

Updates za yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA

Hii ni aibu kama kama iliyolipata jeshi la Polisi Uganda wakati Besgye alipoanzisha harakati za "walk to work" na polisi wakaanza kuwakamata watu wanaojitembelea kwenda kazini kwa miguu badala ya kupanda town bus. Utakamataje mtu anayetembea barabarani bila bango wala fujo? Kweli maccm yamechoka.
 
Piga wahuni hao!
Leo ndiyo nimejua kuwa msalani ni mtoto ambaye hata ungo haja vunja, unashabikia ujinga? Haujui watu wakikomaa hapata kalika? Cha msingi watu wasiandamane,wadai haki mahakamani kama hakuna basi tusubiri hiyo katiba ya chama tawala tuipige chini.
 
Hakuna mabadiliko isiyokuwa na gharama. Polisi waelewe kuwa wanapoamrishwa na wakuu wao kupiga mabomu kabla hawajafanya hivyo wachanganye na akili zao. Nchi hii ni lazima ibadilike. Mabadiliko mi lazima. Haki haiombwi bali inadaiwa. Tutaendelea kudai mpaka dakika ya mwisho. HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
 
Mbona Diamond alipotoka sijui wapi uko alipokelewa Dar?

Mbona maccm huwa wanawatambulisha viongozi wao na hata rais baada ya kuchaguliwa?
 
Maandamano siyo kitu kizuri, wafikirie kutaka haki mahakamani na kama hakuna haki tuisubiri hiyo katiba ya chama tawala tuipige chini, kuanndamana no.

Mkuu ni bora hayo maandamano ya amani yaendelee mpaka haki ipatikane. Unajua haya mambo kwa nchi zingine ndio yanayoingiza watu msituni au hujuma za kigaidi kama kulipua ofisi za umma, vtuo vya polisi na sehemu nyingine nyeti kwa vile haki yao ya kuandamana inazuiwa kwa kutumia mabavu.
 
Leo ndiyo nimejua kuwa msalani ni mtoto ambaye hata ungo haja vunja, unashabikia ujinga? Haujui watu wakikomaa hapata kalika? Cha msingi watu wasiandamane,wadai haki mahakamani kama hakuna basi tusubiri hiyo katiba ya chama tawala tuipige chini.

Suala la kutii sheria bila shuruti liko wazi kabisa. Kama hamtaki kufuata. Mpigwe tu!
 
Pamoja na kwamba Polisi wamezuia maandamano lakini CHADEMA Dodoma wapo barabarani Tayari. Tujuzane sehemu nyingine ambapo maandamano yamefanyika.
attachment.php

Upande wa pili Polisi wamejiandaa vilivyo


Jeshi la polisi limeimalisha ulinzi katika maeneo yote ambayo yalitajwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiyo watapitia wakiandamana kwenda kwenda Bungeni kuanzia saa 4 asubuhi ya leo.


Polisi wakiwa wamefunga kamba kati barabara ya mzunguko ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na chuo cha biashara CBE kwaajili ya kuwazuia waandamanaji hao waliopanga kwenda Bungeni.
4.jpg

Picha kwa hisani ya John Banda

Upates:
Waliomsindikiza Mbowe Polisi wamefukuzwa kwa mabomu sasa wanapambana na polisi walio na virungu pamoja na Mbwa
 

Attachments

  • maandamano.jpg
    maandamano.jpg
    67.1 KB · Views: 4,208
Makamanda mwemweleeeeeee peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
P olisi wafanya maandamano inchi nzima kufikisha ujumbe wa CHADEMA kwa wanainchi.


Kumbe polisi wananguo nzuri za sare zao huwa wameziweka tu majumbani, nimefanya mawasiliano nchi nzima nimeambiwa jeshi la polisi liko stand bay , liko barabarani likifanya doria kudhibiti maandamano ya wafuasi wa CHADEMA ambao wangeandamana leo.


Ofisi zote za CHADEMA zimezingirwa na magari ya ngarandinga ya FFU wakiwa wamavalia sare zao safi teyari kukabiliana na lolote litakalotokea. Ofisi za CHADEMA Mtwara maeneo ya chikongora karibu na soko kuu zimezingirwa, Masasi maeneo ya uwanja wa fisi kuna polisi kibao, Kasulu ofisi za CHADEMA ziko Kigoma Kibondo road karibu na nyumba ya Gorofa ya Ndituye zimezingirwa ,Tanga ofisi za CHADEMA ziko mabanda ya papa zimezingirwa. Mpwapwa ofisi za CHADEMA ziko maeneo ya stand ya zamani zimezingirwa. Dodoma maeneo yote ya barabara inayochepuka toka barabara kuu itokayo Dar kwanda maeneo ya ukumbi wa bunge kuanzia CBE wapo polisi na magari yao, mbwa na farasi ,hapapitiki wamefunga njia, kwenye ofisi za CHADEMA mkoa karibu na FOTS kuna gari za ngarandinga zipatazo 10. Kigoma maeneo yote ya Mwanga, mnarani hadi Ujiji ni polisi tupu.


Wanainchi wanajiuliza kuna nini leo? Wanajibiwa na wenzao kwamba Polisi wanazuia maandamano ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA wanaotarajia kuandamana kupinga bunge la katiba kuendelea kufuja hela za walipa kodi bure.


Kwa mwenendo huu wa polisi wamekisaidia chama cha CHADEMA kufikisha ujumbe wa CHADEMA kwa wanainchi bila wao kujua, kwa maneno mengine Polisi ndiyo imefanya maandamano ambayo yangefanywa na CHADEMA kupinga matumizi ya ovyo ya raslimali za wanainchi yanayofanywa na bunge la katiba.
Ama kweli Polisi watu uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, wanafanya kazi kubwa namna hii ya CHADEMA bila wao kujua.

 
Watawala wana hofu karibia wajinyee!!magamba wamechoka hakika.
 
Back
Top Bottom