Kufuatia sekeseke ya Jana mkoani Mtwara, Polisi leo wameamua kufanya revenge kwa kuvamia makazi ya raia pamoja na kuvunja maduka, kuiba na kuchoma moto mali za raia. Polisi wanachokifanya ni kuleta ubabe kwa raia kwa vile jana baadhi waliuawa
Polisi wameonekana wakiingia kwenye majumba ya watu na kama wakimkuta mke au watoto wanawapakipigo na kuwalazimisha wataje mkuu wa kaya alipo na asipotaja kipigo kinaendelea. Aidha, kila kijana anayezurula barabarani ni kwamba anakamatwa na kuwahishwa gerezani! Kwa utaratibu huu, tunaweza sema kuwa jeshi la polisi limepoteza sifa ya kusimamia usalama wa raia na mali zao na limekuwa chombo cha wizi na kutesa raia kinyume kabisa na majukumu yao.
Napata shida kufahamu kuwa haya yote yanafanywa kwa faida ya raia au nani hasa? Sidhan kama nguvu hizi zinazotumiwa sasa hivi zinalenga kumnufaisha mtanzania kwa namna yoyote ile. Na wala sidhan kama hilo bomba lisipofika Bagamoyo Tanzania itafirisika kiuchumi zaidi ya tulivyofilisika sasa hvi.
Chonde Serikali ya CCM mnachofanya sasa hivi ni vurugu na ukatili kwa raia wenu, tena raia ambao 2015 mtataka kupanda majukwaani kuwaomba kura zao. Inafaa mtumie akili ya kawaida tu kujua kuwa, dhurma kamwe haitashinda. Na uongozi dharimu huondoka kwa aibu.