Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Updates: Yanayojiri Mtwara - hali bado tete (Mei 23/24, 2013)

Waziri mkuu alishaongea na wanamtwara, kama hakuna aliyeelewa ni bora nguvu itumike kuliko kuacha mali zikaendelea kuchomwa moto na kuharibiwa na kuhatarisha amani ya mtwara na baadae tanzania. tuna vyombo vya dola kwa ajili ya kulinda amani acha vifanye kazi yake kwa wale wanaotaka kuiharibu.

Acha kutumia masaburi kufikiri. Matumizi ya nguvu katika suala hili sio approach sahihi hata kidogo. Ubabe unaweza kufanya kazi kwa muda lakini kumbuka hii sio one time project, ni project endelevu ambayo bila kuwashirikisha wananchi, wataihujumu huko mbele.

Tiba
 
Nawapongeza watanzania wenzangu wa mtwara, najua wengi mnashangaa lakini watanzania hawa, maskini waliokosa matumaini kwa kipindi kirefu nawapa pongezi kwa uzalendo mkubwa wanaoendelea kuuonyesha.
Wana mtwara wanastahiri pongezi, na si kwa misingi ya uchochezi, bali kwa namana wanavyotaka kujipambanua kutoka katika historia mbovu ya "tutajua baadae". Wanamtwara wanatambua, na wameshuhudia migodi ya madini ilipoanza kanda ya ziwa,..walisikia jinsi viongozi walivyojitapa majukwaani namna madini hayo yatavyowasaidia watu wa kanda ya ziwa..wanazifahamu ahadi zilivotolewa na serikali mwanzoni miaka ya 1990's kwa wakazi wa kanda ya ziwa. na sasa wanatambua jinsi wana kanda ya ziwa wanavyotaabika kutokana na migodi hiyo, wanavyo uwawa kwa kemikali, wao na mifugo yao, wanavyodhalilishwa na makabulu na jinsi walivyotelekezwa na serikali yao sikivu.

Wana Mtwara wanajua kua ikulu kwa awamu mbili zilizopita imekarabatiwa kwa takribani Tsh billion 67, huku tukiwa na CIT- SCAN moja tu muhimbili tena mbovu. Wanajua kuwa DOWANS ilikua kampuni hewa ya umeme, tena iliyotuingizia hasara ya zaidi ya billion 600, hawataki kuamini kirahisi kuwa hicho kitua cha dar si dowans nyingine.. wanajua kuwa wahusika wa dowans wamesamehewa. Wana mtwara wanajua kashfa zote za mabillioni ya pesa dhidi ya serikali ambazo wewe mwana JF unazifaham.

Kwa Tabu na umaskini waliopitia wana mtwara tangu uhuru, Tumaini lao kwa sasa ni Gesi..na Kwa jinsi serikali hii ilivyo hodari wa kuuza rasilimali zetu kwa kupitia mikataba mibovu mibovu. Watanzania hawa wanakataa kuamini ahadi na wanataka tumaini lao libakie nyumbani. Hawataki hadithi ya "majuto ni mjukuu" kama ndugu zao wa Kanda ya ziwa.Hawataki kuingia kwenye vitabu vya historia kama mangungo wa msovero.

Wakati wa Chief Mkwawa, kuna baadhi ya ndugu zetu watanganyika waliungana na wakoloni na kumuita gaidi, mbinafsi, hapendi maendeleo na mchochezi.Lakini leo hii ni shujaa aliyekataa kuamini ahadi mbovu za kikoloni na utawala wao dhalimu. Wana mtwara wanataka kuingia katika historia kama mashujaa waliochoka ufisadi, ahadi za uongo, mikataba ya kinyonyaji na udhalimu wa viongozi. Baada ya miaka ishirini ijayo kizazi hiki cha mtwara kitarekodiwa kama kizazi pekee kilichokataa dulu za kidanganyifu za ukoloni mamboleo ndani ya tanzania. Kwa kakika WAJUKUU ZAKO WEWE NA MIMI watatushangaa sana kwa namna tulivyo DOCILE na kushindwa kuuunga mkono ushujaa huu wa ndugu zetu watanzania wa Mtwara. I COMMEND MTWARA'S PATRIOTS


Tafakuri hii hailengi kuleta uchochezi
 
Polisi wenyewe njaa kali, wanatumia fursa hiyo kujipatia nawao chochote, Nchi hii raha tupu kila mtu anamnyonga mnyonge wake. Kazi kweli kweli!!!!
 
Hii hali sio ya kushabikia, Vichwa vichache vyenye Busara Viende Mtwara kutafuta suluhisho. Hii ni sawa na kujamba ndani ya maji ushuzi utanuka tu.

Tumbo kutangulia mbele si hoja hata makalio nayo yana umuhimu wake!

Nahisi km Kina -MCHUMIA TUMBO wametangulia mbele, na Kina -MAKALIO wako nyuma, ingawa wote safari moja.

Hili ni jambo la mazungumzo na maelewano na linawezekana km BUSARA itatawala kuliko UBABE.
Nawasilisha
 
Hakuna siku katika karne hii kwa gharama za umeme kushuka katika TZ! Je, madeni ya Dowans, richmond, iptl na mengine yamemalizwa kulipwa?
 
Tunafahamu sana watu kama nyie lazima mtaanza kufaya uchochezi
Huo ni ndio uchochezi wenyewe, polisi fanyeni kazi yenu ya kuhakikisha hali ya amani na usalama inaendelea huko mtwara watu wanawaponda lakini kazi yenu inaonekana. ukiona mtu anavichukia vyombo vya dola ujue huyo ni mmoja wa wahalifu.

Hapa hakuna uchochezi, naeleza hali halisi ya kinachofanyika kwa taarifa yako habari hizi sisimuliwi na mtu, ndg yangu yuko Ligula hospt yeye ana hardware na kama unavojuwa nondo huwa zinawekwa nje so alikuwa akizilinda ili wale waliokuwa wakifanya vurugu wasije kuzipitia ndipo walipomkuta polisi wakamjeruhi vibaya na kumnyang'anya kila kitu kutoka mfukoni mwake zikiwemo Tshs laki sita na simu ya mkononi.
Wewe hauko eneo la tukio usilete ushabiki wako wa kisiasa hapa, tangu mmekremishwa hilo neno uchochezi haliwatokI mdomoni, mnalitumia tu hata pasipo husika, tumia akili, habari za siasa weka pembeni ktk suala hili,FACT.
 
Mungu tuone waja wako tuokoe na kikombe hiki hisicho na hata tone la busara!!
 
Ni jukumu la serikali kulinda amani ya nchi itakuwa ni serikali ya kijinga kuto kuchukua hatua salama ..naomba mtambua kuwa sio wananchi wote wanaopenda hali hiyo ya vurugu kwa hiyo wanastahili ulinzi tena mkubwa...wito serikali hata mkiweza hamisheni kambi kabisa mtwara ..mana watu tunataka kwenda kutafuta ridhiki lakini tunashindwa kutokana na wajinga wachache wasio taka kuelimishwa na kuelewa
 
hakuna busara mbele ya wahuni wewe,ulishaona wapi busara inatumika kumkabiri gaidi mwenye silaha na anayechoma majengo,hao ni risasi za moto tu na nguvu.


mkuu naomba niungane na wewe hapo ni kikundi cha watu wachache chenye maslahi binafsi.
 
serikali inagombana na nani?.. RAIA?!SERIKALI INAGOMBANA NA RAIA WAKE..Naamini wapo watu wanawadanganya watawala, kwamba wananchi hawawezi shindana na Dola. Kuna usingizi mzito watawala wamelazwa kwamba ukiwapiga risasi wawili watatu nchi itatulia, dam ya mtu asiye na hatia haitulii
 
serikal inatakiwa kuwa sikivu na si kuongeza jesh na mashambuliz bal ikae chin na kutafakal elim gan waitoe kwa wanamtwara ili kutuliza ghasia na kurudisha aman mtwara bunhe wataahirisha mpaka lin
 
WEWE unaunga mkono gesi isitoke au? Madai yao walitaka umeme uzalishwe pale na grid ya Taifa ifike mtwara hilo swala halijabadilishwa umeme utazalisha mtwara according to PM na JK, sasa hiyo gesi isitumike kwa matumizi mengine baada ya kua purified kama wao wanavyotaka purification ifanyike mtwara ok itafanyika then what next au itasafirishwa kwa mapipa kusambazwa sehem zote za tanzania? kwani gesi haina matumizi mengine tofauti na UMEME? nashidwa kabisa kuelewa.yani nahisi najichnganya kabisa issue ya mtwara.
watu wa mtwara wanatumika tu,madai yao yote ni ya kipuuzi tu hayana mantinki.
 
Mwisho wa yote wapenda maendeleo watashinda. Bomba la gesi litajengwa kutoka Mtwara hadi kinyerezi na bei ya umeme kwa nchi nzima itashuka.

Ila kwa kuua wananchi wa tanzania. hiyo gesi ni mali ya JK na washirika wake, umeme ukizalishwa Mtwara bei haitashuka
 
Kwa watawala wetu hawa wa sasa wasiona mbele ya pua zao,naiona vita ngumu na katili ya wananchi wa Tanzania kutetea maliasili zao ikianzia Mtwara! Songa mbele wananchi wa Mtwara,watala wezi na wala rushwa hawaaminiki kabisa.
 
Wakuu leo Mtwara hali nI mbaya zaidi kuliko jana kwa vitendo viovu VINAVYOFANYWA na askari wa jeshi la polisi.
Iko hivi;
-Polisi wanafyatua risai za moto kwa raia
-wanavunja mabanda ya biashara ya raia na kupora mali, fedha na chochote kilichopo KISHA KUYACHOMA MOTO
-Wanasachi na kunyang'anya fedha, simu na chochote alichonacho mfukoni kisha wanamjeruhi vibaya yeyote wanayekutana naye bila kujuwa kuwa ni nani
-wanavunja nyumba za raia na kubeba wanachoona kinawafaa

NB: Vijana wengi hasa wa mitaa ya Majengo, Mdenga na Magomeni wameyakimbia makazi yao wako mafichoni nje kdogo ya mji


Inaelekea huu ndo mtindo wa jeshi la polisi siku hizi, hicho wakifanyacho Mtwara town pia walikifanya wilayani Tandahimba last year. Walichoma mabanda ya biashara, soko na kupora mali za raia, HII HALI HAIKUBALIKI TUNAPASWA KUIKATAA KWA NGUVU ZOTE!
 
Hao mapoliccm wapo kimaslahi kwani sasa hivi vijana wakimaliza shule wanakimbilia policcm wakapore raia
 
Back
Top Bottom