Mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kati ya watani wa jadi nchini, Simba na Yanga ambayo awali ilipangwa kufanyika Aprili 27 sasa itachezwa Aprili 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema mabadiliko hayo yamefanywa na Bodi ya Ligi (TPLB) ili kutoa nafasi kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kujiandaa kwa mechi za mchujo za mashindano ya Kombe la Afrika 2015 (AFCON) raundi ya awali itakayofanyika kuanzia Mei mwaka huu.
Wambura alisema Aprili 19 ndiyo pazia la ligi hiyo ya Bara litafungwa na timu nyingine sita zitashuka kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu Alisema mechi nyingine iliyosogezwa mbele ni kati ya Simba dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo awali ilipangwa kuchezwa leo, lakini sasa itachezwa Machi 23, mwaka huu.
Aliitaja mechi nyingine iliyoahirishwa kuwa ni kati ya Yanga dhidi ya Prisons ya Mbeya ambayo sasa itafanyika Machi 26 kwenye Uwanja wa Taifa) na Machi 19, mwaka huu kwenye uwanja huo huo mabingwa hao watetezi wa ligi wataikaribisha Azam.
Pia alisema Machi 15, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili ambazo ni Azam dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Azam Complex, huku Mtibwa Sugar ikicheza dhidi ya Yanga kwenye Dimba la Jamhuri mkoani Morogoro huku Mgambo wakiikaribisha Azam Machi 26, mwaka huu jijini Tanga Mkwakwani, na Aprili 9, mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22, mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera na Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi). Machi 23, mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi 29, mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa) na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5, mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6, mwaka huu ni Coastal vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Amri Abeid), Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12, mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19, mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid) na Coastal vs Kagera (Mkwakwani).
Mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Uwanja wa Taifa Oktoba 20, mwaka huu, watani hao wa jadi walitoka sare ya mabao matatu.
*Simba ina pointi 36 na iko katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambayo itamalizika Aprili 19, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE