Updates: VodaCom Premier League 2009/2010

TIMU GANI ITAKUWA BINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA(Vodacom Premier League)

  • Total voters
    72
  • Poll closed .

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
HATIMAYE mbio za miezi saba ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara, zinaanza leo kwa miamba 12 kushuka dimbani huku bingwa mtetezi, Yanga akianza na wageni, African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Yanga, mabingwa mara 22 tangu kuanza kwa Ligi hiyo mwaka 1965, leo wanakuwa wa kwanza kuikaribisha Lyon kwenye ligi hiyo ambao ni msimu wa kwanza kwao.

Hata hivyo, ni mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vyao, ingawa Lyon wanazidiwa kwa uzoefu.

Katibu Mkuu wa Lyon, Jeshi Zacharia, amesema pamoja na ugeni wao katika Ligi Kuu, lakini ubora wa kikosi chao, unawapa kiburi cha kujiamini dhidi ya Yanga.

“Ni kweli Yanga ni wazoefu zaidi yetu, lakini kwa ubora wa kikosi au kiuchezaji, hilo ni suala jingine…nasi tunajivunia kwa hilo, tutajitahidi kuwajengea vijana hali ya kujiamini,” alisema Zacharia.

Naye Mwenyekiti wa Yanga, Imani Mahugila Madega, kwa upande wake ameifananisha Yanga kama ‘kinara wa mchezo’, ambaye kadiri itakavyokuwa, hauawi.

Alichomaanisha Madega ni kuwa, kadiri itakavyokuwa, Yanga leo itaibuka na ushindi dhidi ya Lyon, hivyo kutwaa pointi zote tatu na kuanza vizuri ligi hiyo itakayofikia tamati Machi 27, mwakani.

Vita nyingine ya ligi hiyo, itakuwa kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Ruvuma kwa wenyeji Majimaji kuwakaribisha Simba.

Ni mechi ngumu kwani wakati Simba wakitaka kushinda ili kuanza vema ligi hiyo, wenyeji Majimaji watakuwa wakipigana vilivyo kushinda katika uwanja wao wa nyumbani.

Majimaji, timu yenye historia katika soka ya Tanzania, leo watakuwa na kazi moja ya kudhihirisha kuwa hawakupanda Ligi Kuu kwa kubahatisha baada ya kuikosa kwa misimu kadhaa.

Hata hivyo, Simba walio chini ya Kocha Mzambia, Patrick Phiri, safari hii wamejipanga kutwaa ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu miwili, ukitwaliwa na watani wao Yanga.

Hata hivyo, vita ya ligi hiyo safari hii inaonekana itakuwa na radha ya aina yake, kwani wakati Yanga wakiwania kutwaa ubingwa wa 23, Simba wamekamia kufanya hivyo kwa mara ya 16.

Aidha, Mtibwa Sugar wenye rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara mbili, leo watakuwa katika Uwanja wao wa Manungu, Turiani kuwakaribisha Manyema Rangers.

Mtibwa Sugar, wanaingia katika kampeni ya kuwania ubingwa wa mara ya tatu wakiwa na kiburi cha ubingwa wa Kombe la Tusker na Ngao ya Jamii.

Kivumbi kingine cha ligi hiyo, kitakuwa kwenye Uwanja wa CCM-Kirumba, jijini Mwanza kwa wenyeji Toto Africa kuwakaribisha Moro United ya Dar es Salaam.

Aidha, katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, wenyeji Kagera Sugar wanaonolewa na Kocha Mganda, George Ssemogerere, watakuwa wenyeji wa Azam FC.

Mechi nyingine, itakuwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kwa maafande wa Prisons kuwakaribisha ndugu zao JKT Ruvu ya Pwani
.
Source: Gazeti la Tanzania Daima
 
majimaji 0 - 2 Simba
yanga 1 - 1 african lion
prison 1 - 2 jkt ruvu
toto 2 - 2 moro utd
mtibwa 2 -1 manyema
kagera 3 - 2 azam
 
Ni matokeo mazuri zaidi kwa simba,kagera na mtibwa kama hawatakuwa wametangulia kwa baiskeli za miwa!
 
Majimaji 1 - Yanga Dar african
Prison 1 - 0 African lion
Simba Sc 3 - 2 Toto Africa

Yebo yebomwaka huu mnalo, nasikia mmemtwanga mangumi refa inaonyesha soka limewashinda..ushauri wangu nendeni mkaungane na kina Rashid Matumla kwenye ndonga..
 
Majimaji 1 na sisi Yanga tuna ngapi? Mbona huwaweka magoli yetu, tafadhari mkuu tutanabaishe basi!
 
YY wabovu na sasa watachapana bakora kisawa sawa...! Hela za ufisadi za EPA-Manji- zina nuksi, na sasa ni kichapo mpaka mkome...
 
YY wabovu na sasa watachapana bakora kisawa sawa...! Hela za ufisadi za EPA-Manji- zina nuksi, na sasa ni kichapo mpaka mkome...

kuchapata bakora wanafanya makosa. Lakini maji maji ilikuwa lazima ishinde hata kwa goli la mkono, hata ingecheza na timu yeyote. Kumbuka gemu lililopita wachezaji wote walilia baada ya kufungwa JKT-Ruvu. Kocha aliponea chupu chupu kufukuzwa, mashabiki walifanya fujo. So, bila kushinda leo kusingekalika huko Songea.

Pia historia inaonyesha kuwa Yanga huwa inafungwa au kutoa draw kule Songea, ni kama Simba ilivyokuwa ikipingwa na Pamba au Milambo enzi zile.
 
YY wabovu na sasa watachapana bakora kisawa sawa...! Hela za ufisadi za EPA-Manji- zina nuksi, na sasa ni kichapo mpaka mkome...
nasikia kaanza kusitisha huduma taratibu sasa ukijumlisha na kichapo sijui kama atabaki..na bado j4 hatoki kwa JKT Ruvu..
 
wana JF hivi tv ngani hapa bongo itaonyesha mechi ya brazil na Argentina..
 
tatizo la yeboyebo hawana kocha,jamaa waliyenae ni msimamizi wa mazoezi tu,vipaji vya wachezaji na migogoro iliyotokea Simba in the last two years imemfavour lakini si chochote
 
wana JF hivi tv ngani hapa bongo itaonyesha mechi ya brazil na Argentina..

Game imeisha na Brazila kashinda tatu bila.Game imepigwa usiku sana kwa mitaa ya huko bongo kama hauja angalia basi hayo ndo matokeo!
 
kuchapata bakora wanafanya makosa. Lakini maji maji ilikuwa lazima ishinde hata kwa goli la mkono, hata ingecheza na timu yeyote. Kumbuka gemu lililopita wachezaji wote walilia baada ya kufungwa JKT-Ruvu. Kocha aliponea chupu chupu kufukuzwa, mashabiki walifanya fujo. So, bila kushinda leo kusingekalika huko Songea.

Pia historia inaonyesha kuwa Yanga huwa inafungwa au kutoa draw kule Songea, ni kama Simba ilivyokuwa ikipingwa na Pamba au Milambo enzi zile.
Yanga tunawajua kwa visingizio, eti wanasingizia historia ya kufungwa Songea miaka 15 iliyopita?

Poleni sana watani kwa kipigo!
 
hii inauma sana kwa wanayanga,sijui kama kutakalika huko jangwani mchawi lazima atafutwe hata kama yanga imefungwa mechi moja na liverpool ya uingereza imefungwa mechi mbili bado haiwezekani....
''Mvumilivu hula mbivu.....ila mvundika mbivu hula mbovu''
QUOTE=Crashwise;575078]Majimaji 1 - Yanga Dar african
Prison 1 - 0 African lion
Simba Sc 3 - 2 Toto Africa

Yebo yebomwaka huu mnalo, nasikia mmemtwanga mangumi refa inaonyesha soka limewashinda..ushauri wangu nendeni mkaungane na kina Rashid Matumla kwenye ndonga..
[/QUOTE]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom