Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,049
- 773
Novemba 18,2012 iliyopita tulirusha kipindi cha barua kutoka kanda ya Ziwa kuhusu tukio la maziko na harakati za kumuenzi Kardinal Laulian Rugambwa. ambao hawakutazama channel ten siku hiyo wanaweza kutazama hapa chini.
Kwa wenye roho nyepesi-Picha zinaweza kuwaogopesha.Pia hii kazi imerekodiwa studio hivyo ilikuwa haijafanyiwa croma key kubadilisha background.lakini ujumbe ndiyo huo.
Leo ni siku nyingine ya kutazama kipindi cha Barua kutoka kanda ya Ziwa Channel ten saa 12:00 jioni.Leo tunatazama sekta ya afya.Kipindi cha leo kitakuwa tofauti kidogo lengo ni kukithi matakwa ya watazamaji.Maomba mtazame kipindi hiki na kutupatia maoni yenu.Vipindi vilivyopita vinapatikana hapa JF na Youtube.
Tuma maoni kupitia baruatv@hotmail.com au unaweza tazama kupitia www.youtube.com/baruatz .
Asante
<font size="4">
Wadau leo october 28 ,2012 msikose kutazama kipindi cha "Barua kutoka kanda ya Ziwa" Leo saa 12: 00 jioni Channel ten.Leo tunatazama changamoto zinazowakabili wazee nchini Tanzania(video hapo juu).Karibu kwa maoni.Nawashukuru wote wanaotutumia maoni hpa JF,FB na email ya baruatv@hotmail.com. Pia tembelea www.youtube.com/baruatz kuvitazama online.
Siku moja nitatoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja hapa JF,wengine nawajibu kule kule chemba au kwa email zao. Asante
M.Byabato
Wadau October 21,2012 *Jumapili saa 12:00jioni msikose kutazama kipindi cha "Barua kutoka kanda ya ziwa" kupitia channel ten.
Kumbuka vipindi hivi ni vya uchunguzi na keshotutarusha uchunguzi kuhusu serikali inavyoendesha operation za kuondoa wavamizi katika hifadhi za taifa . Kamakawaida nitume maoni baada ya kutazama kipindi hiki kupitia baruatv@hotmail.com.
Keep watching channel ten.
Bado nimepata kwikwi katika ku-upload hivi vipindikatika youtube na Vimeo sijui ni computer zetu hapa au ni hizi website kwanifile la 95 mb linagoma kuwa uploaded on youtube/vimeolakini naendelea kutafuta means mtavipata hapa.
M.Byabato
Wanabodi.
Kuanzia leo Octoba 14,2012 channel ten itaanza kurusha kipindi kipya (recorded program) kiitwacho "Barua kutoka kanda ya ziwa" kipindi hiki ni cha dk 30, ni kipindi cha kwenye field siyo studio na kwa asilimia kubwa mfumo wake ni wa uibuaji wa masuala yaliyojificha katika jamii hasa maeneo ya pembezoni hasa vijijini (Ni cha uchunguzi).
Mtayarishaji mkuu wa kipindi hiki ni mimi mwenyewe .
Kitaanza kurushwa leo saa 12 jioni lakini mipango ya baadaye ni kurushwa muda wa PRIME.
Naomba watakaopata fursa ya kutazama watusaidie maoni kuhusu kipindi hiki (baruatv@hotmail.com) ili vijavyo viweze kuboreshwa .
Nitawajuza mengi kuhusu kipindi siku zijazo.
Wasalaam,
Mathias Byabato
baruatv@hotmail.com
MAONI YA WADAU KWA LENGO LA KUBORESHA KIPINDI HIKI
Kazi nzuri Mathias,
Lakini kuna kitu SIJAKIPENDA. Namna ya kuwasilisha. Sina shaka na uwezo wako kiutendaji lakini nikushauri hii style achana nayo, waachie kina 'Angelo Mwoleka' (sijui kama nimepatia jina); ongea kawaida tu, ujumbe unafika na tutazidi kukupa ushirikiano.
Unahitaji kuungwa mkono, makosa madogo madogo huwa yapo kila mwanzo wa project lakini ukikosolewa ukarekebisha basi kila kitu kinaenda barabara.
Unaweza kuanzisha separate thread, ya VIDEOS inayo-update kila unapomaliza kurusha kwenye TV. Sishauri ulete JF kabla ya kwenda kwenye TV; ni vema uheshimu mwajiri wako lakini pia kuja hapa kwa hadhira ni jambo jema pia. Keep all videos on YouTube; itasaidia sana siku za mbeleni.
Kila la heri
Last edited by a moderator: