Hivi mkuu ni kwa nini siku izi inakuwa ngumu sana Ch. ten kushika kwa kutumia dish? I mean kama imekuwa sensitive sana, ikisetiwa leo haipiti siku mbilim ishagoma. Mi nna miezi sasa sikamati ch.ten...
Wadau kesho October 21,2012 *Jumapili saa 12:00jioni msikose kutazama kipindi cha Barua kutoka kanda ya ziwa kupitia channel ten. Kumbuka vipindi hivi ni vya uchunguzi na keshotutarusha uchunguzi kuhusu ..wenye roho nyepesi tunawaomba radhi kwanikinaonesha mambo ambayo huwezi kuamini kama yanatokea *Tanzania. Kamakawaida nitume maoni baada ya kutazama kipindi hiki kupitia.baruatz@hotmail.com.
*
Keep watching channel ten.
*
Nk :Bado nimepata kwikwi katika ku.upload hivi vipindikatika youtube na Vimeo sijui ni computer zetu hapa au ni hizi website kwanifile la 95 mb linagoma kuwa uploaded on youtube/vimeo.lakini naendelea kutafutameans mtavipata hapa.
*
*
M.Byabato
Karibu sana tupate kufamu tusiyoyajua
Kazi nzuri Mathias,kipindi no 1 kimekubali katika youtube ambao hawakuona katika tv tzama hapa
Kazi nzuri Mathias,
Lakini kuna kitu SIJAKIPENDA. Namna ya kuwasilisha. Sina shaka na uwezo wako kiutendaji lakini nikushauri hii style achana nayo, waachie kina 'Angelo Mwoleka' (sijui kama nimepatia jina); ongea kawaida tu, ujumbe unafika na tutazidi kukupa ushirikiano.
Unahitaji kuungwa mkono, makosa madogo madogo huwa yapo kila mwanzo wa project lakini ukikosolewa ukarekebisha basi kila kitu kinaenda barabara.
Unaweza kuanzisha separate thread, ya VIDEOS inayo-update kila unapomaliza kurusha kwenye TV. Sishauri ulete JF kabla ya kwenda kwenye TV; ni vema uheshimu mwajiri wako lakini pia kuja hapa kwa hadhira ni jambo jema pia. Keep all videos on YouTube; itasaidia sana siku za mbeleni.
Kila la heri
Vizuri sana, uungwana ni vitendo!Kwanza Nashkuru kwa maoni yako. Najibu baadhi ya hoja
1.Kipindi hiki kinapita kwenye mikono ya watu zaidi ya 8,naonekana au kusikika mimi tu lakini nakuhakikishia kuwa mabadiliko ya mfumo wa uwasilishaji utaanza kubadilika na kuboreka kutoka kipindi kimoja na kingine
Naam, ni vema ingawa naelewa kuwa huenda mengine yakawa yanakera. Uvumilivu utakuvusha.2. Nitafanyia kazi maoni yote nitakayopewa na wadau
Vema tena,3. Mwanzo mgumu na ninakubali kukosolewa vyovyote
Vizuri sana, uungwana ni vitendo!
Naam, ni vema ingawa naelewa kuwa huenda mengine yakawa yanakera. Uvumilivu utakuvusha.
Vema tena,
Lakini niulize:
Is it a funded project?
Kama ni hapana, nitaachia hapa; kama ni ndiyo niende mbele:
Unaridhika na kiwango (quality) ya picha (video)? Mna mkakati wa kuboresha upande huu?
Again, nakuombea ufanisi; jamii inatakiwa kuwakilishwa vema, ninyi waandishi mkiitumie vema taaluma yenu mtakuwa mmewasaidia wananchi na mmejisaidia.
LAKINI, jaribu kuepa ile style ya kuwasilisha kama vile tatizo si lako na halikugusi. Kumbuka, tone yako ina mchango mkubwa katika kusababisha mrejesho ambao unaweza kuwa hasi au chanya.
Ahsante
Basi, hapo kwenye bold pamenituliza walau. Tuwasiliane kusaidiana kupata wa kukiwezesha kipindi kipate ubora zaidi.No hakuna fund yoyote na huwezi amini natumia gharama zangu kaunzia usafiri wa watu wa picha,mimi mwenyewe editing na production ingawa nimepata mdhamini baada ya program ya kwanza.
Kosa kubwa sana, kumbuka 1st impression ina maana sana na hivyo unapokosea mwanzo basi gharama yake kwako ni kubwa. Sitaki kumwaga mchele hapa lakini naamini unaelewa sababu.1.Kwanza kipindi cha kwanza hakikurekodiwa vizuri na wote tunajua hilo ingawa maudhui ilikuwa nzuri
Quality za YouTube sina tatizo nazo; video camera ilikuwa ina-shake sana na wakati mwingine iliashiria kama mpiga picha alikuwa ni mmoja tu. Ndo maana nikauliza kama una funding. Hapa nikilenga kuwa usiwe ndo unafanya kila kitu kuanzia shooting hadi kuingiza sauti.2.Naomba husijaji ubora kwa kutazama hii clip ya Youtube kwani imebadiliswa kutoka 900MB to 90M ili iwe iweze kuwa uploaded vema yotube na watu kuicheza
Kama Channel 10 wanapatikana online nitaangalia; zaidi ya hapo nitasubiri YouTube videos tu. Well, unashangaa hilo? Mbona kuna shocking stories kwenye magereza? Wewe si mwandishi? Fanya exclusive story ya kwenye magereza usikie maajabu ya TZ. Lakini, you'll need a spy camera na isiwe ya kichina.Kama uko karibu na tv naomba utazame kipindi cha leo HAKIKA hutaamini utakachoona. kama kinatokea nchini tanzania
Kaka una wazo zuri lakini nadhani bado una safari ndefu saana. Mimi kama mtazamaji mzuri wa documentaries, japo si mtaalam ninahisi kuna vitu waweza kuvirekebisha kwa awali.
Kwa kuanza rekebisha haya:
1. Uwe na sauti yako - kama trade mark, sauti yako inaingiliana sana na mtangazaji fulani.
2. Ubora wa picha uko chini saaaaaana. Utadhani unatumia smart phone za zamani sana.
3. Chagua unachotaka kuongelea, na si kuongelea vitu kwa ujumla. Kama kipindi cha leo tar 21 oktoba 2012, kuna sehemu unamwonesha bibi akitolewa kwenye tembe ili ichomwe. Inasikitisha sana, lakini sijaona mantiki ya kuonesha tukio hilo tena kwa kulirudia rudia na wewe hufuatilii linapoishia au ujumbe utokanao na hiyo picha. Sasa sijui nia yako ilikuwa kuongelea unyanyasaji wakati wa kuhamisha wavamizi wa misitu au...?
4. Sauti hu-edit vizuri.
5. Documentary hutengenezwa kwa muda mrefu kukupa nafasi za kufanya masahihisho muhimu.
6. Hitimisho - take home message
Hakikisha mpiga wako anatumia stand siyo kukimbia kimbia! mnakimbiza nini?
vinginevyo kazi nzuri