Martin Kiama na Kipindi Cha Radio Cha Wanafunzi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,445
Reaction score
34,000
KIPINDI CHA RADIO KWA WANAFUNZI: VIONGOZI WA AFRIKA

Kipindi hiki akitangaza Mkurugenzi mwenyewe wa TBC Martin Kiama.

Niko Majengo Middle School, Moshi mwaka wa 1963.

Kipindi kinafunguliwa na nyimbo hiyo hapo chini.

Kipindi hiki kulikuwa cha historia.

Napenda historia na napenda hiyo "signature tune" inayofungua kipindi.

Hiyo nyimbo ni Lemmy Special kutoka Afrika ya Kusini bingwa wa saxophone na filimbi.

Nami kwa kiasi changu nilikuwa bingwa wa kukopi nyimbo hizo kwenye filimbi yangu.

Aliyekuwa akinitisha katika uwanja huu alikuwa kijana mmoja akiitwa Juma Ngereza.

Juma alikuwa na kipaji kingine alikuwa akicheza mpira vizuri sana.

Turudi kwa Martin Kiama.

Wanafunzi wa darasa la tano wote tunaingia kwenye ukumbi wa shule na radio iko mbele kwenye meza.

Kipindi kinaanza kwa nyimbo ya Lemmy Special "See You Later," hapo mimi siko katika ukumbi nasikiliza saxophone nangojea Lemmy amalize kipande chake kisha mimi nampokea na filimbi yangu haiko mkononi iko kichwani.

Vidole vinatembea "chromatics" zote nimehifadhi.

Nina umri wa miaka 11.

Katika vipindi vyote ninachokikumbuka hadi leo miaka 63 ni "Viongozi wa Afrika": "Haile Selassie wa Ethiopia Simba wa Yuda.''

Martin Kiama utapenda kumsikiliza.

View: https://youtu.be/6Lgf9CBHpSQ?si=RhyzJf_kSO3ue_RC

Nilimuhadithia rafiki yangu Harith Ghassany historia hii ya udogoni kwangu.

Siku alipokuja kunitembelea nyumbani akitokea Marekani alikuja na CD ya Lemmy Special.
 
Thanks for this
Sasa ni wakati wa kuandika kitabu cha historia ya maisha yako,
Kwa vile wewe ni msimulizi mzuri, AI imekurahishia kazi, wewe unajirekodi tuu audio au video, kisha una i feed kwenye transcribe, AI inakuandikia kila kitu, inakupangia chapters, wewe unabaki na kazi ya kuisert pictures tuu na captions zake.

Mzee Pasco
 
PM,
Sidhani kama maisha yangu ni muhimu kiasi cha kuandikwa.
 
Ni kawaida, nabii huwa hakubaliki nyumbani, kitu cha muhimu kutoka kwako, sio umuhimu wako, bali hicho kilicho ndani yako, kuhifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.
P.
 
Back
Top Bottom