Naipongeza juhudi inayofanywa na serikali kupanua barabara kuu Mkoani Mbeya. Lakini najiuliza ni kwa nini wajenzi wameanza na maeneo yasiyo na matukio ya kupoteza maisha ya wananchi?
Binafsi labda kama kuna sababu za kiufundi nadhani ujenzi ungeanza na maeneo hatarishi ambayo kila mwaka tunapoteza uhai wa wanaMbeya
Mfano
Mlima simike ambapo juzi tu kuna lori limesababisha ajali na kuua wananchi kadhaa
mtelemko wa iwambi kuelekea Mbalizi kila mwaka kuna matukio ya wananchi kupoteza maisha hadi ilibidi RC Makala kuamua kuweka kituo cha trafic kuzuia magari yawe yanapita kwa zamu.
Kinachonishangaza jana nimeona mkandarasi kaanza na maeneo salama kabisa (kama kule Ifisi) yasiyo na matukio yeyote ya kutisha.
Naomba serikali imuelekeze mkandarasi kuanza na maeneo hatarishi na yenye matukio mabaya kwanza ndipo aendelee na maeneo yasiyokuwa na changamoto kubwa kiusalama.
Tukifanya hivyo tutawahi hata kuondoa kero za kusimamishwa kwa dakika kadhaa ili kupishana malori na magari madogo pale Mwisho wa waya.