Uongo na Ukweli Kuhusu TANESCO Kuzuiwa Kufanya Maintenance

Gesi tumepigwa siku nyingi yule muhuni wa chalinze ni mtu wa ovyo kabisa
 
Sasa si umeuliza alifanya nini? Ulitaka nikujibu majibu ya uongo ama! We lini ulisikia umeme unakatika kwa sababu za hovyo kama anazotoa marope katika utawala wa Magufuli?
Huyo unaye mjibu ni zuzu
 
Je,unakubali kuwa JPM katika suala la umeme kutokatika Mara kwa mara alitengenezewa mazingira hayo na JK kupitia Kinyerezi I iliyoanza kuchangia zaidi ya MW 200 kwenye grid ya taifa mwezi oktoba 2015?
Wacha ujinga kukatika kwa umeme lengo lilikuwa tuuziwe umeme na mafisadi ya iptl hivyo mifumo ya serikali iliuliwa ili sekta binafsi za kifisadi ziuze umeme wa bei ya juu kama siyo magufuli leo tungekuwa tunanunua umeme unit 1sh1500 huo ndiyo ukweli
 
Mkuu 'Extrovert', huyo 'jamaa' niliyemjibu hapa na kumsifu kiaina anafahamika vizuri sana kwa misimamo yake iliyo wazi humu JF. Huyu naona ndiye 'mouthpiece' ya hili genge ambalo sasa linaiendesha serikali, kwa hiyo anakuja humu na hoja zao, nyingi zikiwa ni za kupotosha.

Sifa nilizommwagia ni juu ya juhudi zake kubwa za kutafuta taarifa ili kuunga mkono hayo wanayotafuta upotoshaji juu yake, na wala siyo kwa usahihi wa taarifa zenyewe anazoziweka hapa.
 
EeeenHeeeee!

Hapana, mkuu 'Extro', usiende huko kwenye kifo cha huyo jamaa. Achana kabisa na huko, maanake pako wazi kabisa. COVID-19 ilifanya kazi yake hapo. Woote waloomzunguka wakapukutika, na yeye wala hakutaka kujikinga, unadhani angepona, tena mtu mwenyewe mwenye 'predisposition condition'? Wewe si uliona Mkapa alivyodondoka? Naye unadhani ni hizo 'conspiracy theories' zinazodhaniwa hapa?

Jamaa angekuwa anadunda tu, anatamba hadi sasa kama angechukua tahadhari tu ya kujikinga. Sijui nchi ingekuwaje hadi sasa? Pamoja na haya mengine tunayomkubali kwayo, lakini binafsi nilikuwa na hofu kubwa sana juu yake kuhusu hatma ya nchi hii. Pengine ingebidi tuwe makondoo sote ili mradi jamaa atimize maono yake, 'whatever' maono aliyokuwa nayo yeye juu ya nchi hii.
Hata hivyo, tungefika huko alikokuwa anapaona yeye tukiwa hoi kabisa!
 
Wacha ujinga kukatika kwa umeme lengo lilikuwa tuuziwe umeme na mafisadi ya iptl hivyo mifumo ya serikali iliuliwa ili sekta binafsi za kifisadi ziuze umeme wa bei ya juu kama siyo magufuli leo tungekuwa tunanunua umeme unit 1sh1500 huo ndiyo ukweli
Thibitisha hapa hilo dai lako vinginevyo wewe ni zezeta.
 
Baada ya maelezo yako marefu, je wanatuhakikishia kuwa kwa vile sasa wanaweza kufanya matengenezo inavyotakiwa Tanzania haitakuwa na tatizo la upungufu wa nishati ya umeme? Je, matengenezo ya muda na kiasi gani yataondoa tatizo la mgao?
Umepatwa na nini mzee wangu?
 
Nitoshe tu kukuambia wewe ni mpumbavu sio tusi, ebu niambie watanzania wangapi ukiwepo na wewe ambao mpaka muda huu hawajachanja na hawachukui taadhari yotote ya hiyo corona na hatujafa. Je inamaana corona imeisha tanzania baada ya kufa watu muhimu wa magufuli wakina ben mkapa na magufuli mwenyewe na korona nayo ikaisha!? Acha ujinga wewe kwenye vitu muhimu.
 
Kutokana na swali lako hili inaonyesha wazi wewe ni 'MJINGA', na hilo siyo tusi, ila ni wazi hujui chochote kuhusu haya magonjwa ya milipuko kama COVID-19.
Sitapoteza muda wangu hapa kukuelimisha wewe, kama wakati wote huu tokea corona imeingia hadi sasa, wewe bado hujaambulia chochote kuhusu taarifa zinazosambazwa kila mahala.
Ni watu kama wewe mliomdanganya akapime mapapai, mbuzi, oil, n.k.; kana kwamba hata hakuwahi kuingia darasani na kujifunza sayansi yoyote! Sijui hiyo Ph.D. ya kemia aliipatia wapi!
Kwa vyovyote na iwavyo, tambua kwamba kuondoka kwake kuliepusha taifa hili kupata madhara makubwa zaidi ya yanayoweza kutokea leo au kesho. That was good riddance! Umeelewa?
 
Wewe ni mpumbavu na mshamba ,nyie ndo wale mkiona mtoto mdogo anaongea kiingereza mnasema ni msomi


taifa lenye watu zaidi ya 60m mmeletewa chanjo hazifiki 2m nawasiwasi ata zile 1m za mwanzo hazikuisha,kama corona yako ingekuwa na impact ungeona mtaani mwenye
,wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani bro, unajifanya mjuaji mbele giza.na utaalamu wako wa kujivika wa magonjwa ya mlipuko mmeshindwa kuitetea chanjo yenu kwa wananchi ndo maana tunawachora na kusema nyie ni braliomashenzy bure kabisa
 
Ngoja matengezo yaishe na ITPL inaze kazi kusudi tupate umeme tena. Katika maisha yangu ya utumiaji wa Umeme ni kipindi chia Magufuli tu mabapo sikusumbuliwa na ukatikaji wa Umeme. Maintance kwenye power generation haihitaji uzime mitambo yote ya umeme nchi iwe giza. Hapo mimi ninaona ni misheni ya kutengeza tatizo lisilokuwapo kusudi lihalalishe upigaji tu. Yaani kwamba siku Kalemani alipofukuzwa tu, ndipo mitambo iliyokuwa haipati service nayo ikashindwa kabisa kufanya kazi nchi ikaingia gizani. JF inatunza records sana, tutazirudia records hizi siku zijazo.
 
Ngoja matengezo yaishe na ITPL inaze kazi kusudi tupate umeme tena.
Katika mipango ya TANESCO ya kukabiliana na hali hii kwa sasa, SIJAONA POPOTE ikitajwa IPTL ingawaje nafahamu watu aina yenu mngependa kuona IPTL ikiwashwa ili mpate cha kuongea!!
Katika maisha yangu ya utumiaji wa Umeme ni kipindi chia Magufuli tu mabapo sikusumbuliwa na ukatikaji wa Umeme.
Nimeshasema hapa mara kadhaa, kwanza sio kweli kwamba hapakuwa na matatizo ya umeme na nimeshaweka ushahidi kibao wa watu waliokuwa wanalalamika kuhusu umeme!!
'
Kama wewe haukuwa na matatizo ya umeme, haimaanishi kote kulikuwa vizuri!! Na kama hakukuwa na matatizo, I bet kama ni Dar es salaam basi itakuwa unaishi vile vitongoji vipya kama vile Mbezi Beach, Mbweni, Bunju, Goba, and the like!!

Amini usiamini, usishangae ukasikia Toangoma hakuna matatizo ya umeme lakini Kinondoni yapo, WHY? Kwa sababu Toangoma ni kitongoji kipya, na kwahiyo hata miundombinu yao ya umeme ni mipya!!

Sasa kama unaishi eneo ambalo sio among old residential areas, na kuna umeme wa kutosha, tatizo la umeme kwenu linaweza kuwa rare!

Sasa huo umeme wa kutosha ambao JPM unamfanya aonekane ndio ametatua tatizo, huo umeme ameukuta kwa sababu, almost 350MW ni mradi wa JK ulioanza kutumika October 2015, kwahiyo impact yake imeonekana wakati wa JPM, huku more than 100MW zikiwa zlizoingizwa kweney grid ya taifa back in 2013!!

Kwahiyo JPM ana-enjoy matunda ya waliomtangulia, matunda ambayo waanzilishi hawakuyatumi!
Nani amekuambia inazimwa mitambo yote?!

Tatizo mmezidisha mahaba, matokeo yake hata nyie wenye uwezo wa kufanya kautafiti kidogo mnashindwa kufanya utafiti kufahamu ikiwa wakati wa Kalemani pale Ubungo hali ilikuwaje?! The problem, hata mtu akiwawekea ushahidi, mahaba yanawafanya MUUKTAKATE ushahidi ili muendelee kujiaminisha kila kitu kilikuwa njema!!

Do your own research kwa kutafuta SPECIAL PERFORMANCE REPORT 2019 ambayo ilichunguza utendaji wa TANESCO kisha rudi tena hapa utueleze kama hayo matatizo yameanza baada tu ya Kalemani kuondoka!!
 
Kwahiyo kukatika kwa umeme issue ni machine au ni kupungua kwa maji? Mbona mnatuchanganya? Mi naona huu ni ule wizi wa makaratasi, data nyingii ambazo zinatengenezwa na binadamu ili kuhalalisha jambo fulani. Katika taarifa ya CAG je alitahadharisha kwamba maintanance isipofanyika kuna shida ya umeme itatokea? maana hata magari yetu kuna kipindi tunazidisha kilometres bila kufanya service na yanaendelea kutembea bila shida yoyote.

Jambo lingine ni kwamba CAG siyo mungu wala malaika na taarifa yake siyo msahafu kwamba ina ukweli 100%. Kama aliweza kusema kituo cha mabasi cha mbezi hakina tija na kitasababisha foleni na mpaka leo hatujaona hiyo foleni, tunawezaje kumuamini kwenye masuala mengine?

Shida ya taarifa za CAG huwa haziwi challenged na mamlaka nyingine yoyote ile, akishatoa taarifa yake basi inabebwa kama ilivyo mpaka Bunge lije liifanyie kazi. Mi nadhani ingekua vizuri ukatuwekea taarifa ya Bunge baada ya kuwaita TANESCO kutoa ufafanuzi wa hizo hoja za CAG kuhusu kutofanya maintanance ya mitambo yao ili tubalance story .
 

Kama matatizo yalikuwapo kwa nini watu walalamike sana leo? Siyo hapa JF tu, wewe pita mitaani ndiko utakapopata feedback halisi. Kujaribu kuhalalisha makosa ni kosa zaidi kuliko kutenda makosa yenyewe. Kati ya makosa yaliyofanywa na unaowatetea ni kule kufanya makosa yao so abrupt kiasi kuwa demarcation line ya effects inakuwa so obvious. Ni mara tu baada ya uongozi wote wa Wizara ya Nishani na Tanesco kuondolewa ndipo blackout ikaanza mara moja- ndani ya wiki mbili au tatu tu.

Hiyo ya ITPL imekuwa latently covered na na hayo madai ya kuwa "kuwa na vyanzo vingi" wakati sis tunataka kuwa na vyanzo robust, siyo uwingi wa vyanzo unao-matter.
 
Ni wazi , kutokana na kiwango chako, siwezi kuwa na msaada wowote kwako.
Endelea na ujinga wako hivyo hivyo!
 
Karibu kwenye mjadala...

Hata hivyo, mjadala huu utakuwa na tija ukiweka kwanza data zako ambazo ni za ukweli kwa sababu haina maana kukujibu kwa kutumia data za uongo!
Bwawa la Mtera maji yametoka lini mto Chato?
Nasikia na mto Ruvu umejaa kwa hisani ya Makunduchi
 
Huyo JPM wako na kikwete wako ni wanachama wa chama gani na walihudumia nchi gani?
Mmekalia siasa za watu huku watanzania wanateseka na mnaposhindwa tatua changamoto mnazozisababisha mnatafuta marehemu wa kuwasingizia, muone aibu basi.
Tunataka huduma za jamii, Bei za bidhaa zishuke pia.
Hizi porojo zenu hatuhitaji sie Watanzania mnatuchoshaaaa
 
Tanesco kama mko hapa....
Fanyeni mrudishe umeme hapa MBAGALA KIPATI,mbele ya kituo cha sabasaba na karibu na St Antony....mmekata umeme toka saa 9 alfajiri....na haujarudi mpaKa sasa.

Kama kuna hitilafu umeme umeshindwa rudi mtujuze.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…