kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Hakuna umeme hata dar es salaam, viwanda, majumbani na kwenye biashara hakuna umeme, ni shida na hasara ya matrilion inapatikana: Mvua zinanyesha nchi nzima, mabwawa yamejaa na mafuriko kila kona ya nchi. Kwanini umeme hakuna?
Kipindi cha ukame mnasingizia mabwawa yamekauka na mabwawa yakijaa unasingizia miundombinu mibovu na hakuna anaeonekana kusikitishwa kwaajili ya nchi kukosa umeme. Kwa kipindi kirefu tunaambiwa kuwa maji yaliyoingia bwawa la nyerere yanamudu kuwasha mashine ya kufua umeme, baada ya hapo mvua zikaendelea kujaza mito na mabwawa hadi mafuriko kutokea, lakini unamsikia kiongozi anasema labda mwezi February 2024 ndio mashine ya kwanza inaweza kuwashwa ili kufua umeme, maneno na kauli ambayo haionyeshi kuwa kuna udharura wa upatikanaji wa umeme nchini. yaani hakuna userious wowote kwenye kauli wala muonekano wa msemaji, hovyo.
Shida ni nini, muundo wa tanesco, wafanyakazi wa tanesco, viongozi wa tanesco, wizara ya nishati au serikali nzima?