Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,242
- 12,762
Ni wazi shirika hili limeshindwa kazi yake. Wiki hii nilipo umeme umewaka mchana siku moja tu. Hatuwezi kuendelea namna hii.
Shirika livunjwe. Kuwe na shirika la uzalishaji umeme ambalo litasimamia mitambo yote ya kuzalisha umeme ya serikali, na kuwe na mashirika ya usambazaji wa umeme kwa kila mkoa. Mashirika haya ya usambazaji yaweze kununua umeme kutoka shirika la uzalishaji la serikali au kutoka kwa wazalishaji binafsi.
Mzalishaji binafsi akitaka kuweka solar farm ya 5MW na kuliuzia shirika la usambazaji la Shinyanga aruhusiwe. Anayetaka kujenga geothermal plant huko Rungwe na kuliuzia umeme shirika la usambazaji umeme mkoa wa Mbeya na afanye hivyo. Anayetaka kuzalisha umeme wa makaa huko Songea na afanye hivyo. Wakujenga microhydrodams na kuzalisha MW5 na azalishe. Mkoa kama Njombe ungeweza kualika wazalishaji wa kutumia mabwawa madogo na ungesahau kabisa habari za mgao. Lakini kwa vile TANESCO wamehodhi uzalishaji na usambazaji mambo hayo hayawezi kufanyika.
Tusidhani MW 2100 za bwawa la Nyerere zitatutosheleza kabisa. Bwawa hilo litatupeleka kwenye kama MW3500 tu. Nchi ya Africa kusini inayoongoza kwa kuzalisha umeme Africa ina MW 58,000. Tuna safari ndefu sana. Tunahitaji wazalishaji wengi binafsi. Tunahitaji MW nyingi sana.
Ni wakati wa kubinafsisha kwa dhati suala la uzalishaji wa umeme.