Uongo mwingine wa Spika Ndugai kuhusu Yesu kwenda Yerusalemu

Jasusi Mbobezi

Senior Member
May 17, 2020
195
851
Nimesikia bwana Ndugai ameomba radhi kwa kusema Yesu ana mke, lakini hajaomba msamaha kwa kudanganya kuwa alikwenda Yerusalemu kuhesabiwa.

Hata kama alimaanisha Yusufu, bado alidanganya kuwa eti alikwenda Yerusalemu. Biblia haisemi Yusufu alikwenda Yerusalemu, Biblia inasema Yusufu alikwenda Bethlehemu, ngoja ninukuu maandiko hapa chini;

Luka 2:1-4
1 Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.
2Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.
3 Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.
4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

Kwahiyo alichokisema Ndugai ni uzushi wa kupuuzwa na ahojiwe na kamati ya maadili ili kukomesha vitendo vya ukurupukaji kwa viongozi wenye dhamana, pia ameliaibisha sana kanisa la Anglican.
 
Nimesikia bwana Ndugai ameomba radhi kwa kusema Yesu ana mke, lakini hajaomba msamaha kwa kudanganya kuwa alikwenda Yerusalemu kuhesabiwa.

Hata kama alimaanisha Yusufu, bado alidanganya kuwa eti alikwenda Yerusalemu. Biblia haisemi Yusufu alikwenda Yerusalemu, Biblia inasema Yusufu alikwenda Bethlehemu, ngoja ninukuu maandiko hapa chini...
Huyo ndiye mshauri wa askofu mkuu wa anglikana duniani
 
Ndugai anahitaji kufanyiwa "Deliverance" ili aweze kumfamu bwana katika "Roho na Kweli"..hivyo msameheni tu huyu kiumbe (AKA - Mshauri wa Askofu:)
 
Watu husomea hizo kazi. Si kila mtu anaweza kuwa mchungaji au kiongozi wa dini. Wengine ni Wabunge; wengine madereva; wengine madaktari nk. Matatizo kama haya hujitokeza kwa wale wanaodai kujua kila kitu.
 
Mheshimiwa pamoja na ile barua ya kuomba radhi Watanzania bado kafanya kosa juu ya kosa. Yusufu (na mkewe) alikwenda mji wa Daudi unaoitwa Bethlehemu na si Yerusalemu. Hili ndilo jambo ambalo watu wengi hawajaligundua. Tusome:

Luka 2 : 4-5
4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.
 
Mtu ameshakiri kwa barua, kwamba ulimi uliteleza kuendelea kujadili ni upungufu wa hoja period
Ulimi uliteleza na bado anaendele ku spewe ignorance that man is very dangerous asikae bila uangalizi ,alikua anajaribu kutuaminisha anajua maandiko matokeo yake anaishia anajipakata tu
 
Ulimi uliteleza na bado anaendele ku spewe ignorance that man is very dangerous asikae bila uangalizi ,alikua anajaribu kutuminisha anajua maandiko matokeo yake anaishia anajipakata tu
Huyu huwa Mara nyingi tu anaongea pumba na shit za kila aina..hajistukii

Nawaza kama no baba ana watoto sijui wao waweje
 
Back
Top Bottom