Acheni kuamini viongozi wa Dini

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,411
Natamani kuleta Somo ila naamini nitalileta ,kuhusu Jinsi viongozi wa Dini walivyofanikiwa kuwateka na kuwafanya mandondocha wanaojiita waumini ,Leo hii BBC wamefanya uchuhguzi wakina na hata mwanae TB JOSHUA amethibitisha tuhuma mbalimbali za Baba yake,lakini waumini na wafuasi wa hawa manabii wa uongo huwaelezi kitu wanakwambia BBC haiwapendi waafrika,mara BBC wazushi wanawachukia wakristo. Nakumbuka Gwajima alipozini na video yake kuvuja ,waumini wake walikuja juu sana na kudai ni video fake kana kwamba video original za porn wanazijua, nawakadai baba yao anaonewa ,

Leo tumuangalie Gwiji mmoja Daudi mwana wa Yese, kipenzi Cha Mungu achana na bla blaa za Waislamu wanasema Muhammad eti ndio kipenzi Cha Mungu ,

Daudi ndiye kipenzi Cha Mungu ,imefika hatua Mungu akampa na mtaa huko mbinguni unaitwa Sayuni yaani mji wa Daudi ...

Ikafika kipindi Mungu anasema Kwa nabii Samweli ,nimemkataa Sauli nimemchagua Daudi sababu anaupendeza Moyo wangu


Hata Wafalme wote wa israel waliofata baada ya Daudi walikuwa wanapimwa matendo yao Kwa kufananishwa na Daudi

Wafalme wote waliofanya vizuri ,Maandiko yanasema AKAFANYA MEMA KAMA DAUDI BABA YAKE...

Lakini hebu tumuangalie huyu Daudi upande wa pili

Kama angeishi nyakati hizi na kufa kwa nyakati hizi kisha maandiko ya BIBLIA yakaandika habari zake, basi wengi wangekataa na kuona anachafuliwa mtumishi wa MUNGU. kwa sababu kuna wenye mtazamo kuwa Watumishi wa Mungu kuna dhambi hawawezi kufanya,

Mfalme DAUDI akiwa ni mfalme wa pili baada ya SAULI, Wafalme waliwekewa utaratibu wa ufalme wao, kwa kuambiwa

Kumbukumbu 17:18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi;

19 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya;

Mfalme alipaswa kuisoma na kuishika Torati siku zoteza maisha yake, yaani TORATI ndiyo katiba ya uongozi wake, na mfalme DAUDI alisoma maandiko haya ya Torati yaliyosema;

Walawi 18:20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.

Na akasoma hapa tena:

Kumbukumbu 5:21 Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako.

Lakini pamoja na DAUDI kuyasoma yote hayo, nini basi alichofanya MFALME DAUDI?

2 Samweli 12:2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

3 Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?

4 Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.

Ukiendelea kusoma, utaona yule mwanamke alipata mimba, Daudi akataka kupambana ili kuficha kwa kumtaka URIA MHITI alale na mkewe kisha ile mimba ionekane kuwa ni ya URIA MHITI na siyo DAUDI, bado inashindikana mwisho DAUDI akaamua kupanga URIA MHITI, apangwe safu ya mbele ili auawe na ikwa hivyo.

2 Samweli 11:14 Hata ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria.

15 Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe.

tujiulize nyakati hizo zingekuwa ndizo hizi za leo kila mmoja yupo kivyake na dhehebu lake, nani angehusika kumuonya DAUDI kwa uovu mkuu namna hiyo, unalala na mke wa mtu ukiwa Mtumishi wa MUNGU uliyeaminiwa na bado unamuua mtu uliyemchukulia mkewe? au ni nani angeijua siri hii kama NATHANI asingepelekwa kwa DAUDI kwenda kumuonya?

2 Samweli 12:9 Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni.

10 Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako.

Habari hii kama isingeandikwa ni nani angeyajua haya? au ni nani basi angeweza kusadiki kuwa kweli DAUDI namna ile aliyokuwa nayo mtu aliyechaguliwa na MUNGU angeweza kuyafanya haya yote? au DAUDI angejipa Ukuu kama wanaojipa leo viongozi wa madhehebu, ni nani angethubutu kumkemea?


Kwa kufupisha tu ,Daudi pia aliiba wake wengi tu wa watu ,mfano Abigaili ,

Lakini kitu kimoja alichokuwa nacho Daudi na ndipo kinamtofautisha Daudi na Sauli


Daudi alikuwa akiambiwa umezini ,Hana habari yakubisha au kujitetea ,anakubali anatubu

Ndicho kimefanya MUNGU amuite Daudi kipenz chake ,ndio kimefanya Daudi apewe na mtaa huko mbinguni

Akapewa heshima ,ya Masihi kutoka kwenye ukoo wake

Yesu jina lingine anaitwa mwana wa Daudi
 
Back
Top Bottom