Uchaguzi 2020 Uoga: 2020 Mwaka wa uchaguzi umefika lakini CCM yaendelea kuzuia Mikutano ya hadhara, Msajili wa Vyama aufyata

Ili kuhalalisha uvunjifu wa Katiba ya nchi, Mwenyekiti wa CCM ndugu Magufuli alinukuliwa akitoa marufuku ya shughuli za kisiasa kwa kisingizio dhaifu cha kuleta maendeleo na kwamba wenye hamu ya kufanya siasa wasubiri mwaka wa uchaguzi 2020, Polisi wakadaka amri hiyo haramu kama kifanyavyo kidaka tonge kwenye chakula , wanasiasa waliojaribu kupinga amri hiyo haramu wakakamatwa, wakapigwa, wakateswa na baadaye kuswekwa lupango na kisha kufunguliwa kesi za kizushi na kufungwa jela, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya kusini Mh Suleiman Methew ni miongoni mwa wanasiasa waliofungwa kwa vile walifanya mikutano kinyume cha katazo la Magufuli (Majina ya Polisi wote waliotumika tunayo)

Kama wasemavyo Wahenga, Usiku wa deni hauchelewi kwisha, basi ndicho kilichotokea, 2020 imefika na bado waliosema tuisubiri wanaogopa kuruhusu mikutano ya hadhara, wanaomba siku zirudi nyuma lakini haiwezekani, hawajui cha kufanya na wamekwama, kile kilichoitwa kuzuia siasa ili kuleta maendeleo hakipo, bali ifahamike kwamba badala ya maendeleo hali ya kiuchumi imekuwa mbaya zaidi, hakuna ajira kwa miaka yote minne, wala hakuna nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wachache wasiozidi laki 6 wa serikali, hali ni mbaya hata kuliko kabla ya zuio la mikutano.

Hata hivyo wananchi wametambua kwamba kukataza siasa haikuwa sababu ya maendeleo bali ulikuwa uoga wa Mwenyekiti wa CCM ambaye alikuwa hana ajenda ya kuwaambia wananchi baada ya kuingia ikulu Kibahati .

Itaendelea...
Dictatorship and tyrannic!
 
Zuio la mikutano ya Siasa siyo la kisiasa, inabidi muwe mnaelewa! Wewe unalalamika mbona walioozuiwa hawlalamiki, wewe huwezi kujiuliza kichwani kwako?
 
Hivi kuna waziri aliyewahi kuwa muongo kushinda Mwijage ?
Kosa kubwa lilikuwa kupambana na wafanya biashara kama wezi, wakulima kudhulumiwa mazao, bei zikadorola!!
Vyeti feki ikawa feki!!
Viwanda vingi na maduka vimefungwa, ajira hakuna!!
Sijui maendeleo yako vipi!!
Agenda ni nill wataeleza nini kwa wananchi??
 
Tuliambiwa mapema kwamba , NIKIWA RAIS MTALIMIA MENO
 
Back
Top Bottom