Kuna wakati unajiuliza hii kweli ni serikali ya wanyonge?Inasikitisha sana bodi iliyopewa dhamana kuwezesha kupata elimu inavyobadilika na kuwa sehemu ya kuwanyonya watoto wa msikini.
Ukiangalia statement ya marejesho unatakiwa kulipa administration fee, penalty na value retention fee.
Inashangaza sana hayo makato ukifikiria mtu kamaliza chuo hajapata kazi miaka 3 hadi 4 lakini mkopo unaendelea kuliongezeka kila kukicha.
Leo nitazungumzia kimojawapo. Ukiangalia hiyo wanaita: Value Rention Fee (VRF) is a statutory charge to maintain the value of money throughout your repayment period. It is charged at 6% of the outstanding balance per annum. However it accrue daily at the rate of 0.0001643836 (that is 6% divided by 365) of the outstanding principal loan balance per day. SO it continues to accrues until you finish paying the outstanding principal loan.
Kwa hali hii mkopo huu hautalipwa na watu wengi watafanya juu na chini kukwepa kutolipa.
Ni aibu mkopo wa serikali unageuka kuwa chombo kumaliza na kukandamiza watoto wa maskini, sasa haina tofauti na mikopo ya biashara, wizi mtupu
Hakuna mtu asiyependa kulipa kama unadaiwa lakini mnapoweka mashari na vigezo ambayo haikuwepo wakati wa kuchukua mkopo inakuwa hatari sana. Serikali iache kutumia mabavu
Wanyonge ni kina nani?