Unyama wa Mwanadamu: Ukatili na Madhara Yake

Unyama wa Mwanadamu: Ukatili na Madhara Yake

Kigongoi kwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2018
Posts
550
Reaction score
654
Kama ni kweli kabisa binadamu anaweza kumteka mwenzie kwa sababu kamkosoa au ametofautiana nae katika hoja na mawazo tofauti nakuamua kumuua; huyo ni MNYAMA.
Kama ni kweli mwanadamu anashindana na kikundi kingine lakini alie kwenye kiti anatumia vyombo vyenye silaha kumwaga damu na wakati mwingine kuua kwa kisingizio cha aina yoyote ile;mwanadamu huyo ni MNYAMA.
Kama mwanadamu anatumia mamlaka yake kuminya au kuondoa haki ya mpinzani wake na wakati mwingine kum mimia marisasi ili yeye aendelee kuishi peke yake au aishi na watu mabubu wasioweza kuhoji na ambao wanabaki kumuomba na kumsujudia yeye; huyo ni MNYAMA.
Kama kweli mwanadamu anaweza kuingilia mifumo ya utoaji haki kwa kulazimisha hukumu inayo m favor yeye hata kama anachoshtakiwa nacho hakipo au kimepikwa na watu wake; huyo ni MNYAMA.
Kuingia kwenye nyumba za ibada,iwe kanisani au msikitini bila kua na aibu au huruma kabisa kabisa;hizo ni tabia za kinyama.
Kukanyaga katiba au kuipindisha ya chama chako au ya Dola kwa manufaa yako,wewe ni MNYAMA
Pamoja na unyama woooote huo unaoweza kufanya kumbuka kwamba kuna mwisho. Lakini ni vizuri mwisho huo ukawa mzuri kwako Siku hazigandi,
 
Binadamu ni mnyama katika hali yoyote, ila ni mnyama mwenye akili zaidi.
 
Ukishaua once, wewe ni katili na sidhani kama hutaacha kuua second, third time....hilo ndio li abdul la mama Samia..
 
Back
Top Bottom