trachomatis
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 3,758
- 746
Hongera zao..
nyie cdm acheni upendeleo haka kaumarufu uliopo umechangiwa saana na vijana wawili yaani Mnyika na Mdee.Zitto alianza vizuri ila siku za karibuni amekuwa mtu wa kuropoka tu .Natumaini kijana mwingine mwenye mvuto ni SilindeHongera zao..
nyie cdm acheni upendeleo haka kaumarufu uliopo umechangiwa saana na vijana wawili yaani Mnyika na Mdee.Zitto alianza vizuri ila siku za karibuni amekuwa mtu wa kuropoka tu .Natumaini kijana mwingine mwenye mvuto ni Silinde
Freeman na slaa walijiunga lini chadema kutokea ccm?
Hakuna cha kujadili hapo zaidi ya kuwapongeza. Au labda tusubiri Wanamagamba na Wake zao (CUF) waje mapovu yakiwatoka na maneno mbovu mbovu
Ndugu siasa sio kama mchezo wa kiduku ukichuchumaa watu wanashangilia.
Kwa hiyo msipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, sifa mnazowamwagia hawa jamaa ni sifa za kienyeji zaidi.
Mwisho wa siku mtasema Mbowe na DK Slaa, wanamzidi Obama, kwa siasa.
WanaJF,
Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.
Kwanini nimewachanganya Pamoja?
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.
Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.
Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.
Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.
Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.
Mafanikio yao
Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.
1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.
Maadui wa Chadema wanatakaje?
Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.
Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.
Changamoto zao.
Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.
Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.
Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.
WanaJF Karibuni kwa mjadala!
Tatizo la watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri badala yake wanaruhusu hisia zao kutawala na kuishia kutuhumu vitu ambavyo hawana uhakika navyo.Unakumbuka kabla ya ubinafsishaji hali ya viwanda ilikuwaje? Unakumbuka hali ya uchumi ilikuwaje?
Hao akina Slaa na mbowe wamefanya nini significant kwenye uchumi wetu? kazi tu kupiga porojo na kutoa lawama. Wawauige menzao Zitto Kabwe na Mnyika, atleast hawa wawili wana ABC za uchumi na siyo PHD za sheria za kanisa na UDJ!
muulize mkeo!!
Namsikitikia sana Zitto, nadhani anajuta lakini afanye nini.
Wewe unakijua? acha upuuzi wako kila mwanadamu atayaonja mauti haijalishi kwa muda na wakati gani
Endelea kusikitika tu na katika hilo hatuna cha kukusaidia!
Mlitaka kumtumia ili kufanikisha agenda yenu ya kuihujumu chadema lakini mipango yenu imekwaa kisiki.
Na Zitto anayo furaha kuendelea kuwepo chadema na kuiona ikizidi kustawi kwakuwa amewakatalia kuwa msaliti kwa chama ambacho ameshiriki kukijenga kwa mikono yake mwenyewe.
Pamoja na kujaribu kupandikiza propaganda ya ukabila na baadae singo ya udini, lakini mmeambulia patupu na ''chama cha msimu'' kimegeuka kuwa chama kiongozi katika nchi na wananchi wameendelea kukiamini na kukikubali!
Namsikitikia sana Zitto, nadhani anajuta lakini afanye nini.
Ndugu mwanamagamba, hongera kwa kuchagua avatar nzuri inayo-reflect jinsi magamba wanavyoonekana mbele ya jamii.
Umemaliza kila kitu kisha unasema karibuni kujadili. Umesema ungelikuwa mwanachama wa CHADEMA! Ila kwa namna ulivyochambua wewe ni mwenzetu ndani ya CHADEMA.
Wanaongoza nchi gani?
Zitto mwache awepo hapo, hajamalizia kazi yake, ikiisha humuoni hapo.
upuuzi mtupu hapo hakuna chochote cha maana alichochambua,eti nafasi ya mboe na slaa isiguswe au ndio namna ya uteteaji wa mfumo kristo ndio maana hutaki watoke kwy nafasi zao?