Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

hahahaaaaa MCHUZI WA BATA...kweli bata MCHAFU..yaaaaaan feasibilty study ya nguvu kias hichi unajifanya hujui.....utajua tuu hata ucku!
 
Mi nadhani wa step down wawapishe kina myika na wenzio kwa jinsi historia inavyosema
mafanikio yao na ya wengine yanaenda sawa kabisa,hata mrema na marando walijenga chama kisha kikapotea,seif sharif na lipumba nao
sasa nadhani wao wawe wajanja wawahi kukimbia kabla mambo hajaenda kombo
sasa nadhani ni wakati wa vijana kuchukua nafasi mapema katibu nyika mwenyekiti zitto
magamba 2015 watatutambua



hivi ni vitu vya kufikirika tu,si hoja za msingi na watanzania wa 1995 si 2015
 
Hakuna kipengele kwenye katiba ya CDM kinachosema urais utagombewa na mwenyekiti, sioni kwanini uandike eti Mbowe anastahili credit kwa kumwachia Dr Slaa kugombea urais. Hiki ni chama cha kidemokrasia, hivyo mwaka 2015 mwanachama yeyote anayejiona anazo sifa za kuongoza nchi hii, ruksa kuchukua fomu. Hatutaki yaanze kujengwa mazingira ambapo mwanachama tofauti na hawa tuliowazoea akichukua fomu ataonekana msaliti au mamluki. Tuache demokrasia iamue nani atatufaa.

Wewe acha uzushi wewe, unamaanisha nini unaposema "tofauti na hawa tuliowazoea", Hawa Mabwana
kila mmoja amegombea urais mara moja moja, Mbowe akashindwa na Slaa akashinda, MARA MOJA TU. sasa
unaposema tuliowazoea sikuelewi unataka kujenga hoja gani, acha uzushi aisee,

Wakati pekee ambao ni sahihi kusema tumewazoea ni pale watakapotaka kugombea kuanzia mara ya tatu
na kuendelea,

Kama tayari unayemgombea wako, nguvu ya busara itawadhibiti nyote wawili, wewe na huyo mgombea.
Hata kama tunafuata ama tunataka kufuata democrasia, ni lazima tufate democrasia yenye manufaa.
Namaanisha kwamba Democrasia inamipaka yake.

Tuendelee na kujadili hoja ya msingi, ambayo kimsingi ninaiunga mkono.
 
inabidi bwana molemo ahojiwe kuhusu utimamu wake coz comparison ya obama na hawa majembe wetu does not correspond hata kidogo kutokana na mazingira wanayodili nayo so pls dont go any further coz umechefua jf
 
Nimeipenda analysis yako fmpiganaji. Naomba utoe analysis ya vichwa panzi FF, MS, RITZ na REJAO watakaposhika nafasi UV CCM.
 
Kabla ya udini wako na ukanda wako mlioutengeneza na serikali yako, tunaomba mturudishie viwanda vyetu mlivyopeleka majumbani mwenu. Nyinyi mnaona ni afadhali kuwanufaisha wafanyabiashara wa nje, waarabu, na wahindi kuliko wazawa na ndio maana vijana wanateseka. Hili suala lako la udini halina maana kama viwanda vyetu.
Tatizo la watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri badala yake wanaruhusu hisia zao kutawala na kuishia kutuhumu vitu ambavyo hawana uhakika navyo.Unakumbuka kabla ya ubinafsishaji hali ya viwanda ilikuwaje? Unakumbuka hali ya uchumi ilikuwaje?
Hao akina Slaa na mbowe wamefanya nini significant kwenye uchumi wetu? kazi tu kupiga porojo na kutoa lawama. Wawauige menzao Zitto Kabwe na Mnyika, atleast hawa wawili wana ABC za uchumi na siyo PHD za sheria za kanisa na UDJ!
 
Nice post/analysis.
Labda wazo moja, hapo kwenye kutafuta wanachama!

Kitu kikubwa ambacho CDM wanatakiwa kufanya ni kufanya study kwa nini CCM iliishia kuja kuwa na viongozi bomu? Bila shaka ilitokana na wanachama bomu, na wanachama bomu wanatokana na mfumo bomu wa kuwapata!

Hivyo ningeshauri waangalie mtindo wao wa ku recruit wanachama!
China yaweza kuwa mfano mzuri!nchi ina watu 1.4 bil, chama kimoja lakini wanachama ni only 80 mil!
Kwa sababu uanachama una apply au unakuwa invited, una-asesiwa ndo uwe mwanachama!

Sio hii Operesheni sangara mwishowe wanaingiza na magamba kama kina Shibuda!

Kuwa na wanachama wengi ni kitu poa sana ila ni vema kufanya mambo endelevu hata kama yanatumia nguvu nyingi na muda, mana faida si lazima iwe kwetu, hata vizazi vyetu pia!

Nina watu kibao ambao ni wanachama wa CCM lakini hupigia kura CDM and vice versa!So wanachama ni kujenga chama, na wapiga kura ni the entire mass wanachana na wasio kuwa wanachama.
 
Udini ulikuwepo mbona mnasahau mpema yule mk...wnu mlimwambia kwamba ni chama chakigaidi baada ya ndoa mkasahau mkaangalia upepo unauvumia wapi mkahamanao mkaja chadema.Ila chadema hakuna udini nikuwaelekeza watu ambao mmewapotosha ili muendelee kuwaibia bila kuhoji nakuhakkshia wakielewatu mjue tunawazi na hatafufuka milele.
Hebu andika tena vizuri mkuu...sielewi hapo umeandika nini!!
 
CCM imekwama kabisa kukisambaratisha CDM ha haitaweza kamwe kwani kwa miaka yote hiyo wameweza kusambaratisha chama chochote ambacho kilikuwa kinaelekea kutishia kuikaribia CCM
NCCR ilisambaratishwa kwa mbinu za kijasusi ikafa hadi mnavyoiona leo ipo hoi bin taabani baada ya viongozi wakuu kutofautiana
UMD - chama kilichokuwa na nguvu sana kanda ya ziwa -- Mwanza, Tabora na Shy chini ya waasisi wake - Chief Fundikira RIP na Christopher Kasangatumbo na wengineo -- hiki kilikufa tu mwaka 1996 baada ya viongozi wakuu kutofautiana.

Sasa ukitaka kukiua CDM - ingiza mfarakano kati ya DR. Slaa na Mbowe hapo utakuwa umefanikiwa. Sasa kufanikisha hilo ndugu yangu sijui utumie njia gani maana kama mlete hoja alivyosema, pesa hazina nafasi, Majungu hayana nafasi kupandikiza wanachana mamluki haina nafasi --Kutumia wabunge kumchana mwenyekiti bungeni pia imekwama... sasa hata mimi kweli sioni njia ya kuisambaratisha hii combination.

Napendekeza kwamba hii ndiyo combination iliyofanya kazi nzuri ya chama cha siasa chochote ambacho kimeshaanziswa katika nchi hii. YES ningekuwa mimi ni mjumbe wa kamati kuu ningependekeza kwamba hawa watu wabakie kwenye madaraka hadi tukamilishe hii project ya kukitoa chama cha mapinduzi madarakani. 2015.
 
Mgamba wanaweweseka wanapo sikia haya majina mawili ya Slaa na Mbowe,


Kwa ushirikiano wa viongozi hawa wawili na viongozi wote wa CDM lazima JAHAZI litie nanga pale MAGOGONI 2015
 
Safi sana kamanda maelezo mazuri,hakika tukiendelea na umoja huu,Chadema tutachukua nchi kutoka kwa wanyang'anyi wa mali ghafi za watanzania.
 
Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

Napenda kuungana mkono namtoa hoja kwa hili la kujiestablish kuanzia ngazi ya chini kabisa.itakuwa rahisi sana kupata wanachama na wagombea wenye vigezo kama tutakuwa na miziz tangu kaya hadi taifa
 
Mi nadhani wa step down wawapishe kina myika na wenzio kwa jinsi historia inavyosema
mafanikio yao na ya wengine yanaenda sawa kabisa,hata mrema na marando walijenga chama kisha kikapotea,seif sharif na lipumba nao
sasa nadhani wao wawe wajanja wawahi kukimbia kabla mambo hajaenda kombo
sasa nadhani ni wakati wa vijana kuchukua nafasi mapema katibu nyika mwenyekiti zitto
magamba 2015 watatutambua


chama kinaenda kuchukua dola, kina mnyika bado wana nafasi kubwa tu ya kukiongoza hiki chama, kwa sasa tuachieni viongozi hawa wawili -- pia kuna wengine umependekeza hapo bado hawaaminiki na sisi wananchi wanyonge.
 
WanaJF,

Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Kwanini nimewachanganya Pamoja?

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.

Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.

Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.

Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.


Mafanikio yao

Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.

1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

Maadui wa Chadema wanatakaje?

Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.


Changamoto zao.

Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.


Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.

WanaJF Karibuni kwa mjadala!

Hapa ndo panapowaumiza kicha ccm, wao wanataka na wanajitahidi kwa nguvu zote hawa jamaa watengani kwa kuweka kirusi chao ili chama kianguke, naamini 2015 aidha chama kimeshinda au kushindwa mbowe itakuwa ni haki yake ya msingi kujiuzulu
 
Tunaposema jf ni ya magreat thinker mkuu umeonyesha kwa vitendo hlo nakupongeza kwa uchambuz mzur ambao umeonyesha uhalisia Wa CHADEMA nawapongeza pia viongoz we2 ninachoshaur hzo changamoto wazifanyie kaz mfano badala yakuwa na mabaloz wa nyumb kumi sisi tunaweza kuwa nayetu yanyumba ishirini hii itasaidia kuimarisha chama nchi nzima wetu wasiwe mabaloz wawe najina jingne Kama Makamanda kwani magamba waweza sema tumewaiga big up CHADEMA NA WAFUASI WAKE!
 
uchambuzi nimeupenda ukweli mtu
kuhusu ishu kuongeza nguvu vijijini.kazi imeshaanza.
 
WanaJF,

Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.

Hapa mkuu, umenifurahisha, kudos
 
huyo jamaa ni mnafiki jana kuna thread aliianzisha kuhusu Zitto, Warioba, Dr Slaa na Dr Salim walivyofanikisha kuonana na kikwete na katika moja ya post zake akajifanya yeye anaijua Chadema vizuri na amekua mwananchama wa muda mrefu bahati mbaya nbatumia simu ningekua kwenye Computer ningeikopi hiyo Post na kuibandika hapa...




Halafu ukishaibandika ndiyo umefanya nini? jibu hoja kwa hoja acha shutuma na kutafuta makosa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom