- Thread starter
- #101
WanaJF,
Nawashukuru sana nyote kwa jinsi mlivyoipokea na kuijadili hii mada. Idadi ya watu walioipitia hoja hii na waliochangia mpaka sasa ukilinganisha na threads nyingine za leo imeonyesha wazi kwamba viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa ni majabali wa siasa za upinzani na Tanzania kwa ujumla.
Kwa kupitia maoni yenu nyote mpaka sasa imeonekana dhahiri wale Pro-CDM walioko hapa jamvini na waliojitambulisha rasmi wanawaunga mkono majabali hawa kuendelea kuongoza chama hiki na upinzani kwa ujumla. Nimegundua kitu kimoja cha ziada wafuasi wa Chadema wana imani kubwa na viongozi hawa wawili na wasingependa viongozi hawa kutenganishwa kwa njia yoyote walau kwa sasa.
Nimefurahishwa na comment moja hapa kwamba baada ya viongozi hawa wawili kuiingiza Chadema Ikulu 2015 basi Freeman Mbowe ataweza kuruhusiwa kukaa pembeni.Lakini sharti akiingize kwanza chama Ikulu.Nimeipenda hii!!
Wapo rafiki zangu kina Rejao,Faiza Foxy,Ritz,Kim Kardash,Barubaru na wengineo wachache ambao wanajulikana hapa jamvini kama wapinzani wakuu wa Chadema.Pamoja na kwamba hoja mlizoleta ni za mzaha zaidi dhidi ya majabali hawa wa kisiasa,lakini nimezipenda kwa sababu mbali na kujadili kwa mizaha mmeshindwa kupinga kwa hoja chochote kile nilichoeleza katika mada yangu juu.Lakini niwashukuru kwani michango na mizaha yenu inazidisha utamu wa mjadala
Wito kwa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa
Ningependa viongozi hawa wote wawili wasome yote yaliyoandikwa kwenye hii mada.Najua Dr Wilbroad Slaa yuko huku jamvini,sina uhakika sana kama Freeman Mbowe naye yupo. Lakini naomba walau wasaidizi wao wawatonye viongozi wao kuhusu hii mada ya leo.Pia naomba viongozi hawa wawili wasome kwa makini madai yote yaliyojadiliwa na wanaJF mpaka sasa na michango itakayoendelea kutolewa kwa sababu mjadala haujafungwa.
Kama kuna mapungufu yoyote watakayoelezwa kulingana na mada hii wajirekebishe ili azma yao ya kukamata dola 2015 itimie.Wanapaswa kufahamu kitu kimoja tu-wanachama wana imani kubwa nao!!
WanaJF nafurahi kuwa member wa hili jukwaa. Thank you all.
Tuendelee na mada yetu.