Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Imekuuma?

Huo ndio ukisikia Mhogo mchungu, unakera lakini unaula, una njaa ufanye nini?

Unaonaje ukikaa kimya maana huna pointi... kwani lazima uchangie? utapandisha presha bure! mchambuzi katoa analysis iliyoenda shule anayepinga sawa na kupiga ngumi ukuta utaumia mwenyewe.
 
Umekuja vizuri,analysis yako ipo sahihi,Japo inamapungufu ya Ubinafsi Tata,'NINGELIKUWA MWANACHAMA WA CHADEMA',ningeshauri Utata huo wa Utambulisho wa Itikadi yako Uutoe,au Unahtaji Kadi ya Uanachama iliuwe mwanachama wa chama Flani..?Amka,Upenzi/Uanachama udhihirika kwenye Kura,mengine Mbwembwe kutokana na Mfumo wa Maisha kubadilika.
 
Tunaomba tufahamishwe ni utaratibu gani ulitumika kuwapata wabunge wa viti maalum?
 
vipi kuhusu chagga development manifesto ya mzee mtei na waasisi wenzake ? chama ni kile chenye mfumo wa kitaasisi ambapo kila mwanachama ana haki sawa.suala la wlbroad slaa kugombea urais ilikuwa chambo na kabla ya kukubali alitoa masharti ya kuhakikishiwa maslahi yake ya ubunge.alifahamu wazi kuwa asingeshinda na hivyo alikuwa anasisitiza kubaki kwenye ubunge wake karatu.wenye chama wakakuballi ana na matakwa yake ya maslahi. masuala ya vyama vya siasa na uendeshaji wake sivyo kama yanavyoonekana. tunahitaji watu makini na wakati mwingine hawana vyama
 
Hata mimi ningemshauri hivyo hivyo.Kama si mwanachama aende makao makuu afanye mazungumzo zaidi na viongozi halafu achukue kadi.Tunataka vichwa kama hivi
 
Hakuna cha maana ulichoandika zaidi ya kueleza historia zao ambazo kila mwanadamu hakosi historia.

Labda utuambie hizo historia zao zinaisaidia nini Tanzania?

Historia sio mpaka mtu afe, akifanya kizuri msifie na umpe hongera na sio akitokas ndio uanze kumsifia aahaa jamaa alikuwa... Kitu gani? Mpe hongera ukiwa unamuona na akifanya kibaya mwambie pia huo ndio uungwana na maendeleo pia.

"Bila historia hakuna mandeleo" na "bila maendeleo hakuna historia"

NAJIEGESHA KIDOGO!
 
vipi kuhusu chagga development manifesto ya mzee mtei na waasisi wenzake ? chama ni kile chenye mfumo wa kitaasisi ambapo kila mwanachama ana haki sawa.suala la wlbroad slaa kugombea urais ilikuwa chambo na kabla ya kukubali alitoa masharti ya kuhakikishiwa maslahi yake ya ubunge.alifahamu wazi kuwa asingeshinda na hivyo alikuwa anasisitiza kubaki kwenye ubunge wake karatu.wenye chama wakakuballi ana na matakwa yake ya maslahi. masuala ya vyama vya siasa na uendeshaji wake sivyo kama yanavyoonekana. tunahitaji watu makini na wakati mwingine hawana vyama

Chizi si lazima atembee uchi.Utamjua tu kwa maneno yake
 
Tunaomba tufahamishwe ni utaratibu gani ulitumika kuwapata wabunge wa viti maalum?

Dr Barubaru,
Hakuna wa kukujibu ilo swali hata huyu muanzisha hii thread ambae anasema Mbowe na Slaa, wameleta demokrasia ndani ya Chadema hawezi kujibu.

Jibu lao kubwa wanakuambia angalia namba ukiwauliza mmetumia njia gani kupata hizo namba hawasemi.

Ukiangalia hiyo orodha ya wanawake 40 wanawake 15 ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro.

Namba kwa ndio kigezo kikuu cha demokrasia.
 
kila mtu ana haki ya kusema lakini kiukweli hli halina ubishi kwa sasa tz hii iliyochakachuliwa CDM ndio chama kinachotetea maslah ya wanyonge a nchi hii,
 
Habari hizi kwa wanaCD umewashika pazuri maake ndizo wanapenda kusikia masikioni mwao.Vipi uchaguzi lini maake Kitila Mkumbo anautaka Ukatibu Mkuu na Zitto- Uenyekiti (kamati ya Wazee ilimwomba asubiri Mbowe amalizie kipindi chake) sasa itakuaje?
 
Suala la Udini na Ukaskazini wamelishughulikia vipi?
Tukumbuke kabla ya hawa watu hawajaingia madarakani, siasa za Tanzania hazikuwa na chembe ya udini, hata kama hii dhana ilikuwepo, ilikuwa kwa kiwango cha chini sana.
Kabla ya udini wako na ukanda wako mlioutengeneza na serikali yako, tunaomba mturudishie viwanda vyetu mlivyopeleka majumbani mwenu. Nyinyi mnaona ni afadhali kuwanufaisha wafanyabiashara wa nje, waarabu, na wahindi kuliko wazawa na ndio maana vijana wanateseka. Hili suala lako la udini halina maana kama viwanda vyetu.
 
WanaJF,

Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Kwanini nimewachanganya Pamoja?

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.

Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.

Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.

Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.

Mafanikio yao

Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.

1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

Maadui wa Chadema wanatakaje?

Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.

Changamoto zao.

Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.

Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.

WanaJF Karibuni kwa mjadala!

Hakika wewe ni Mwanachama nguli wa CDM ila kwa sababu ka-unafiki kamo moyoni mwako, ndio sababu umekwepa kujitambulisha kama Mwanachama hai ili kukonga nyoyo za wasio na vyama kujiunga katika chama chako (CDM).
 
Suala la Udini na Ukaskazini wamelishughulikia vipi?Tukumbuke kabla ya hawa watu hawajaingia madarakani, siasa za Tanzania hazikuwa na chembe ya udini, hata kama hii dhana ilikuwepo, ilikuwa kwa kiwango cha chini sana.
Udini ulikuwepo mbona mnasahau mpema yule mk...wnu mlimwambia kwamba ni chama chakigaidi baada ya ndoa mkasahau mkaangalia upepo unauvumia wapi mkahamanao mkaja chadema.Ila chadema hakuna udini nikuwaelekeza watu ambao mmewapotosha ili muendelee kuwaibia bila kuhoji nakuhakkshia wakielewatu mjue tunawazi na hatafufuka milele.
 
WanaJF,

Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Kwanini nimewachanganya Pamoja?

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.

Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.

Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.

Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.

Mafanikio yao

Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.

1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

Maadui wa Chadema wanatakaje?

Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.

Changamoto zao.

Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.

Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.

WanaJF Karibuni kwa mjadala!

Mi nadhani wa step down wawapishe kina myika na wenzio kwa jinsi historia inavyosema
mafanikio yao na ya wengine yanaenda sawa kabisa,hata mrema na marando walijenga chama kisha kikapotea,seif sharif na lipumba nao
sasa nadhani wao wawe wajanja wawahi kukimbia kabla mambo hajaenda kombo
sasa nadhani ni wakati wa vijana kuchukua nafasi mapema katibu nyika mwenyekiti zitto
magamba 2015 watatutambua

Back
Top Bottom