Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 27, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WanaJF,

  Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

  Kwanini nimewachanganya Pamoja?

  Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.

  Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.

  Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.

  Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.

  Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Joseph Mbilinyi-Sugu na wengine wengi.


  Mafanikio yao

  Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.

  1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
  2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
  3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
  4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
  5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
  6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
  7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
  8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
  9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
  10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

  Maadui wa Chadema wanatakaje?

  Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

  Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.


  Changamoto zao.

  Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

  Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.


  Mwisho
  Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.

  WanaJF Karibuni kwa mjadala!
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu fmpiganaji, hakika umeandika kwa kirefu ufasaha na rahisi kwa mwanachama yeyote kuelewa. Hii ni analyisis ya hali ya juu. Hakika kwa uliyoandika kuhusu hawa viongozi ni wazi usione vyaelea vimeundwa.

  Asante sana.
   
 3. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha kujadili hapo zaidi ya kuwapongeza. Au labda tusubiri Wanamagamba na Wake zao (CUF) waje mapovu yakiwatoka na maneno mbovu mbovu
   
 4. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Freeman na slaa walijiunga lini chadema kutokea ccm?
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Big up fmpiganaji
   
 6. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli umenena ukweli mtupu! Changamoto kubwa iliyobaki ni kuaongeza nguvu na kasi ya CHADEMA vijijini na hatimaye 2015 kazi ni moja tu, kuchukua nchi!
   
 7. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  UMENENA TUWASUBII MAGAMBA WAJE NA CCM B TUwASIKIE
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hukukosea hata kidogo, muda mfupi baadaye...


   
 9. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nawewe ulijiunga lini na ccm kutoka ukiwa kwenye akili zako timamu?
   
 10. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  FF na Malaria sugu hawajaiona hii!
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naona umeshaanza.Karibu Magamba/Dilunga jamvini.
   
 12. M

  Mkono wa Tembo Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fantastic analysis! BIG UP
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Watakurupushwa hata kama wako bafuni ili waje kuchangia
   
 14. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hakuna cha maana ulichoandika zaidi ya kueleza historia zao ambazo kila mwanadamu hakosi historia.

  Labda utuambie hizo historia zao zinaisaidia nini Tanzania?
   
 15. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  hakika cdm tuna mwenyekiti mwenye msimamo mkali usioyumba, ni kati ya wafanyabiashara wachache sana walioingia kwenye siasa bila kuogopa kuaribiwa na ccm angekuwa legelege tusingekuwa hapa leo hii..binafsi napenda kumpongeza mwenyekiti zaidi
   
 16. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Ndugu mwanamagamba, hongera kwa kuchagua avatar nzuri inayo-reflect jinsi magamba wanavyoonekana mbele ya jamii.
   
 17. Hagga

  Hagga Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kutumia muda wako kufanya uchambuzi wa kina uliojikita katika hoja.
   
 18. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hakuna kipengele kwenye katiba ya CDM kinachosema urais utagombewa na mwenyekiti, sioni kwanini uandike eti Mbowe anastahili credit kwa kumwachia Dr Slaa kugombea urais. Hiki ni chama cha kidemokrasia, hivyo mwaka 2015 mwanachama yeyote anayejiona anazo sifa za kuongoza nchi hii, ruksa kuchukua fomu. Hatutaki yaanze kujengwa mazingira ambapo mwanachama tofauti na hawa tuliowazoea akichukua fomu ataonekana msaliti au mamluki. Tuache demokrasia iamue nani atatufaa.
   
 19. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyo jamaa ni mnafiki jana kuna thread aliianzisha kuhusu Zitto, Warioba, Dr Slaa na Dr Salim walivyofanikisha kuonana na kikwete na katika moja ya post zake akajifanya yeye anaijua Chadema vizuri na amekua mwananchama wa muda mrefu bahati mbaya nbatumia simu ningekua kwenye Computer ningeikopi hiyo Post na kuibandika hapa...
   
 20. mbogoshi ya boganga

  mbogoshi ya boganga Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu uchambuzi umetulia huo,CHADEMA NDIO CHAMA PEKEE kinaongelewa hata na wanfunzi wa shule ya msingi. Unaweza kuwa dhehebu fulani kwasababu umewakuta wazazi wako wanasali dhehebu hilo,lakini unaweza kuwa unasali dhehebu fulani kwa sababu ulipenda utaratibu wao na ukaamua kujiunga na dhehebu hilo: my note, Mlio CCM hameni sasa mko huko kwa sababu wazazi wenu na babu zenu wamelelewa huko na hamko huko kwa sababu mlielewa sera na utekelezaji wa CCM.
   
Loading...