- Thread starter
- #181
Tutaona nyumba ndogo anakuja juu siku hizi baada ya juice ikulu...??
Mkuu umenifurahisha sana maana umekiri kiutu uzima halafu unarudisha swali kuzuga.Nakushukuru mkuu Topizal.Usiku mwema.
Tutaona nyumba ndogo anakuja juu siku hizi baada ya juice ikulu...??
Mkuu umenifurahisha sana maana umekiri kiutu uzima halafu unarudisha swali kuzuga.Nakushukuru mkuu Topizal.Usiku mwema.
WanaJF,
Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.
Kwanini nimewachanganya Pamoja?
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.
Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.
Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.
Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.
Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Zitto Kabwe na wengine wengi.
Mafanikio yao
Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.
1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.
Maadui wa Chadema wanatakaje?
Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.
Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.
Changamoto zao.
Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.
Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.
Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.
WanaJF Karibuni kwa mjadala!
Hapa hakuna chama ukitaka kujua ubovu wa CDM ngoja ufike uchaguzi ndani ya chama nafasi ya uenyekiti wa chama taifa ndiyo utajua chama cha nani kwa sasa katibu mkuu huyohuyo na mwenyekiti huyohuyo ebu tutoe demokrasia ya wanachama wengine kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama fanyeni kama CCM usione wamekaa kimya wana nguvu tofauti na mnavyowafikiria kilichofanya wapoteze majimbo mengi uchaguzi uliopita ni kwa sababu ya kuwengua wale walioongoza kwenye kura zao za maoni kwa mfano jimbo la Iringa Mwakalebela alikuwa mshindi bila ubishi nani asiyejua hilo na ukitaka kujua ukweli majimbo yote yanayofanyika uchaguzi kwa sasa wanabeba Igunga.
Uzini na linafuata arumeru ngoja muone alafu mjiulize ni kweli mnapendwa au mvurugano wa kura za maoni kwa CCM wakati wa uchaguzi mkuu 2010 ndiyo ulikuwa mtaji kwenu sidhani kama CCM watarudia makosa tena.
CCM ni chama kizuri kina mfumo mzuri wa upatikanaji wa viongozi wake kuanzia shina mpaka ngazi ya taifa siyo kama CDM viongozi wake wanaletwa tuu na makao makuu wewe angalia ata viti maalum vya ubunge kwa wanawake jiulize wanapatikanaje tafakari kwa makini mfumo mzima wa chama na upatikanaji wa viongozi wake utaju kama chama hicho ni endelevu au si endelevu,u as great thinker chunguza hilo kisha chukua atua!
Hakuna cha maana ulichoandika zaidi ya kueleza historia zao ambazo kila mwanadamu hakosi historia.
Labda utuambie hizo historia zao zinaisaidia nini Tanzania?
I salute you sir!! shukrani kwa uchambuzi wako. Katika juhudi za kuhakikisha tunaimarisha chama, nashauri pia sisi wanachama kupitia kwa viongozi wetu utafutwe utaratibu ili kuweka mkakati wa kuanza ujenzi wa Ofisi za chama kila Wilaya ili kuendana na hadhi ya chama.
fmpiganaji, pongezi zangu ni nyingi kupitiliza. Nimesoma, nimesoma post ya mwanzo hadi mwisho. Nimehemo ya woga na kukata tamaa kwa wana magamba (wakiongozwa na bibi kizee faiza fox, king'asti wake Rejao na ritz,mchuzi wa bata n.k) imekuwa ya dhahiri na bayana. Hawataki wala kuamini kwamba ni kweli hayo uliyosema.
Nafarijika na najua wewe hukusoma shule za kata!
Wewe unasumbuliwa na na usemi wa Bendera hufuata upepo na wala huna data zozote. Ni wasomi wangapi wanaunga mkono CHADEMA? Unajua undani wa CHADEMA mpaka useme viongozi wake hawana migogoro? Slaa ni BMOWE ni kama X na Y kwa watu wa hesabu wanajua , mlinganyi kama Y =2x, Y inatemegea sana X ,Wale jama wanajuana na wanajua wanavyoitafuna CHADEMA.
SLAA anaishi kwa fedha za CHADEMA, Mbowe anaidai Chadema madeni kibao na ni kama Mzabuni wa CHADEMA, sasa atawezaje kumkoromea Slaa ambaye ni mtendaji wa Chama? Hebu jikumbushe episodi ya ZITTO na Mbowe katika kugombea ukuu wa Chama hicho. Unajua chanzo cha kifo cha Chacha Wangwe?
Mimi usiniambie kabisa kuhusu hao Mabwanyeye. Ni kweli kwamba wamefanikiwa kufanya harakati mbalimbali kama Migomo vyuoni, migomo ya wafanyakazi n.k. Hivi siku wakifanikiwa kushika hatamu watajidai kwamba walikuwa wapiganaji au wachochezi? Uliza fukuto la upendeleo wa uongozi kwa wanawake katika Chama hicho. Unajua chizi anaweza kujifanya anajua sana mbele ya watu wenye akili zao akadhani yeye ndo basi kumbe wanamsanifu tu.
Hakuna wasomi wanaokiunga mkono Chadema bali wanakiona kama kikundi fulani cha wasanii, si unajua wasanii wanavyoweza kushangiliwa kwenye majukwaa lakini siku ya siku JINA WASANII linatawafanya waendelee kuonekana wasanii tu.
WEWE UNASUMBULIWA na ufinyu wa kutosoma na kuelewa, na naona una matatizo na uelewa wa lugha - kiswahili (hilo tuliweke pembeni).
Hivi na wewe unajiweka kwenye kundi la 'great thinkers'? Unaamini migomo vyuoni ni kwa sbabu ya Dr. Slaa na Mbowe? Naona weweutakuwa *********. Lini Mbowe na Dr. Slaa wakatoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa elimu ya juu?
HIZI SHULE ZA KATA TUTAZIJUTIA DAIMA, wewe ukiwa 'product' mojawapo.
Mkuu uchambuzi umetulia huo,CHADEMA NDIO CHAMA PEKEE kinaongelewa hata na wanfunzi wa shule ya msingi. Unaweza kuwa dhehebu fulani kwasababu umewakuta wazazi wako wanasali dhehebu hilo,lakini unaweza kuwa unasali dhehebu fulani kwa sababu ulipenda utaratibu wao na ukaamua kujiunga na dhehebu hilo: my note, Mlio CCM hameni sasa mko huko kwa sababu wazazi wenu na babu zenu wamelelewa huko na hamko huko kwa sababu mlielewa sera na utekelezaji wa CCM.
sawa mtoa mada.mi ninasubiri awamu nyingine ya uchambuzi wako
sawa mtoa mada.mi ninasubiri awamu nyingine ya uchambuzi wako