Mjadala: 'Namna ya Kutambua na Kuepuka Utapeli Mitandaoni' - Septemba 21, 2023

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
Mtandaoni ni mahali ambapo kunaweza kuwa na fursa nyingi; matumizi mazuri ya kimtandao yanaweza kutambua fursa chanya za kufungua faida nyingi zinazopatikana kwenye mazingira haya ya kisasa ya kimtandao.

Lakini Mtandaoni kuna masuala ya Utapeli pia. Je, Umewahi kukutana na matukio ya Utapeli kupitia Mitandao? Utautambuaje Utapeli wa Mtandaoni? Je, utauepuka vipi Utapeli wa aina hiyo?

Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na JamiiForums itaendesha Mjadala kuhusiana na Utapeli wa Mtandaoni na maswali hayo pamoja na mengine mengi yatajibiwa na kuwawezesha Wananchi kutumia mitandao kwa salama.

Muda ni kuanzia saa 11:00 hadi 12:30 jioni ya leo 21 Septemba, 2023, kupitia Mtandao wa X.

Jiunge nasi kupitia link hii: https://twitter.com/i/spaces/1RDGllEkYNEGL


Max 1.jpg
Tax.jpg

UTAPELI MITANDAONI UNAWEZA KUFANYIKA HATA KWA KUKUTANA ANA KWA ANA

Akielezea zaidi kuhusu hilo kupitia Mjadala wa Kutambua na Kuepuka Utapeli Mtandao, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Ithibati wa Vodacom Tanzania, Agapinus Tax, ametoa ufafanuzi kuwa Udukuzi ni pale ambapo Mtu anapata uwezo wa kuingilia vitu vyako kama Fedha na vingine

Wakati huohuo, Social Engineering ni kitendo cha Mtu kuweza kutumia njia tofauti tofauti kuweza kukulaghai ili aweze kupata Taarifa zako. Pia, kuna njia nyingi kama 'Phishing' - kutumia Picha, 'Smishing', au kutumia Ujumbe/sms

Meneja Uthibiti wa Matukio ya Utapeli kutoka Vodacom, Dingo Peter ameeleza Social Engineering imegawanyika kwa njia mbili ambazo ni Kwa kukutana na Mtu ana kwa ana na kwa kufanyika kupitia Mitandao

UNAWEZA KUTAPELIWA KWA KUREKODIWA TAARIFA ZAKO KUPITIA SIMU

Akitoa ufafanuzi kuhusu utapeli wa aina hiyo, Meneja Udhibiti wa Matukio ya Utapeli kutoka Vodacom, Dingo Peter, amesema utapeli wa ana kwa ana Mtu anaweza kujitambulisha kwamba anatoka sehemu kama Vodacom na anachokifanya ni kuweka kitu kinaitwa 'Screen Recording' ambapo anaweza kurekodi chochote unachokifanya kwenye Simu yako

Pia, Mtu huyo anaweza kukwambia uweke 'Password' kwenye Huduma za Kifedha kama M-Pesa au kwenye akaunti ya Benki, ukimaliza hapo anakuwa amepata moja kwa moja 'Password' zako

WATU WAEPUKE JUMBE ZA MATAPELI NA WAZIRIPOTI KWA NAMBA 15040

Meneja Udhibiti wa Matukio ya Utapeli - Vodacom, Dingo Peter, amesema Watu wanapaswa kuepuka kujibu 'SMS' ambazo zinatumwa zikiwa na maelezo ya Michezo ya kubahatisha ambapo Matapeli huamini kuna Watu wanakuwa wanafanya Miamala ya namna hiyo

Amesema Utapeli wa 'SMS' uko kwa njia nyingi ikiwemo kutangaza nafasi za kazi na nyingine ni kutuma jumbe zinazoonesha umeshinda Mchezo fulani, na unapowasiliana nao hapo ndio unajiweka hatarini kutapeliwa

Pia, njia nyingine ni Mtu anakupigia simu anajifanya yeye ni Mtu wa Vodacom na kusema kuna Pesa imekosewa kutumwa na mwisho wa Siku wanakuomba urejeshe, wakati huo wametuma SMS isiyo ya kweli. Ukipata jumbe hizo ripoti kwenda namba 15040

WATU WENGI HAWAJUI NAMNA YA KUKABILIANA NA UTAPELI WA MITANDAONI

Akizungumza kupitia Mjadala Namna ya Kuepuka Utapeli Mtandaoni, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, amesema hilo linasababishwa na kutokuwepo kwasababu hakuna njia za moja kwa moja za kukabiliana na Utapeli isipokuwa kwa Elimu kuhusu masuala hayo

Amesema wapo Watu wanaojua kuhusu masuala ya Utapeli lakini mara nyingine huwa ndio Matapeli. Pia, kuna wengine bado wanapata shida kufahamu kwa undani, mfano Wasaidizi wa Kazi ambao wengi wao hawana Elimu nzuri wanaweza kuambiwa hata watoe vitu ndani ya nyumba na wakatoa

Ameongeza kuwa namna nzuri ya kuwasaidia ni wale wenye uelewa kuhusu Utapeli Mitandaoni kuwasaidia wasio na uelewa huo na wanapoingia Mtandaoni ni vyema kuwasasidia kwa kuwapa uelewa wa namna ya kutumia Mitandao hasa wanaponunua Simu basi ni vizuri kuwaelewesha namna ya kutumia Vifaa hivyo

UKIWA NA 'PASSWORD' RAHISI UNAWEKA MAZINGIRA YA KUINGILIWA TAARIFA ZAKO

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, ameshauri watumiaji wa Mitandao kuhakikisha Wanalinda Vifaa vyao kwa kuweka 'Passwords' ambazo ni ngumu kwa Mtu mwingine kuzidukua

Akizungumza katika Mjadala kuhusu namna ya Kuepuka Utapeli Mitandaoni uliofanyika kwa Ushirikiano na Vodacom Tanzania, Maxence amesema "Password bora ni ile yenye herufi kubwa na ndogo, alama na namba. Unaweza kutumia jina lako na kuligeuza kuwa password nzuri. Mfano: Sehemu kwenye A ukaweka 4 na nyingine. Angalizo: Kamwe usiache password yako ukaitoa"

Ameongeza kuwa kuna njia ya kuongeza ulinzi katika kifaa chao kwa kutumia "Two Factor Authenification" japokuwa wengi hawaitumii kwa kuwa hawawajibi katika suala la Usalama. Suala lingine ni Watu kuweka password (Nywila) rahisi sana, wengi wanatumia Majina yao ya kuzaliwa au majina ya Watu wao wa karibu
 
Hii safi sana. Watu wa “Tuma pesa kwenye namba hii wamezindi mno…..”
 
Hii mada ya msingi sana aisee. Watu wanapigika vibaya mno, na hakuna matarajio ya kwamba kuna siku watu watakuwa salama kabisa dhidi ya haya mambo.
 
Huyo mkurugenzi wa Voda ndio atoe ufafanuzi kuhusu faragha za taarifa zetu. Matapeli na hao wanaotuita "wapumbavu" kisa hatujashiriki kubeti wanapata wapi namba zetu.?
 
Jamani Akaunti yangu ya instagram ime dukuliwa nifanye je
 

Attachments

  • Screenshot_20240225-195848.jpg
    Screenshot_20240225-195848.jpg
    23.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom