Unazikumbuka nyimbo za shule ya msingi (e.i. std i - iii)?

Unazikumbuka nyimbo za shule ya msingi (e.i. std i - iii)?

Ngoo ngoo ni nani wewe,mimi ni mtoto na safari,narudi nyumbani kwa baba na mama!!!!
 
Sasa ni saa ya kwenda kwetu,
Mama amepika,wali wa nyama e eh!
Kwaheri mwalimu, kwaheri yakuonana!!!
 
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 ndio mwisho, nilishona nguo haina mapindo nikampa cacico ajifungu tumbo! kibibi naumia tumbo naumia tumbo, tushike mabega tushike kiuno tushike tushike mbili mbili tupige saluti maligomba maligomba maligomba tiu u u u!
 
Last edited by a moderator:
jamani naomba mniwie radhi, huu wimbo siupendi ila enzi hizo tulikuwa tunauimba kwa furaha zoooooteeee

"Chama chetu cha Mapinduzi chajenga nchi, chama chetu cha mabwepande (jamani typing error, afu kifutio cha computer yangu kimeisha sababu ya kufuta sana) chajenga nchi "
Nyerere aaaaaaaah na Mwinyi wanajenga nchi x2
basi ikitokea kama Mwalimu Nyerere katembelea wilayani kwetu, tunapanga mistari tunaimbaje huo wimbo kwa nguvu kweli na jua kali likiwa linatupiga!!!!!!!!!

Hii ilikua inaimbwa sana na vijana wa chipukizi...enzi hizo mashuleni kulikua na vikundi kakamavu vya aina mbili ama skauti au chipukizi.
Chipukizi walikua ni yosso wa CCM na jezi zao zilikua ni full gwanda za kijani na skafu ya rangi njano plus kijani,na kofia ya kijani lol...
 
Makao makuu ya chama na serekali--Na--serekali yaliamiaaa uko dodoma dodoma ni..................nakumbuka nko shule ya msingi kwenye mchakachaka mm nlikuwa siuimbi kwa sababu niliichukia ccm toka utotoni wangu
 
Hima himaaaaaaaaaaaaa
Tanza............niaaaaa
Hima Himaaaaaaaaaaaa
Tanza.............niaaaaa
Sisi vijana wa chama........
 
haa. . . hv mmesahau wimbo wa taifa ulipokuwa unaimbwa kila asubuhi kabla ya kuingia darasan
Mungu ibariki Africa, wabariki viongozi wake.. . . .
aah utamalizia
 
"I WROTE A LETTER TO MY DARLING, BUT SHE DIDIN'T ANSWER NO. I DON'T KNOW WHY SHE DIDIN'T! x2. WHO IS KNOCKING AT THE DOOR, SISTER IS KNOCKING AT THE DOOR, DARLING IS KNOCKING AT THE DOOR, I KNOW!"
 
"I WROTE A LETTER TO MY DARLING, BUT SHE DIDIN'T ANSWER NO. I DON'T KNOW WHY SHE DIDIN'T! x2. WHO IS KNOCKING AT THE DOOR, SISTER IS KNOCKING AT THE DOOR, DARLING IS KNOCKING AT THE DOOR, I KNOW!"

jaman SALOK umenikumbusha mbali sana. thou sikumbuki sauti ya huu wimbo bt nlikuwa naupenda enzi hzo!
 
Last edited by a moderator:
itv ndio imeanza mwaka 94, tunaimba class wanawake kuweni wenye furaha, na raha, wakai wote, popote na jessy!
jessy, pedi mpya za kike za jessy, ni nyororo raha kuvaa na kupa kinga thabiti.
wakati wote, popote, na hazina mikanda!
khaaaaaaaaaaaaa! mwalmu akitusikia ni kupiga magoti juani lol! we used kuenjoy!

Umenikumbusha mbali sana my dearest sister,,Halafu hili tangazo sio mwaka 94, ni la mwaka 1992.. Natamani sana niende pale TBC kuwaomba kama wanayo matangazo haya wanipe niyaburn niwe nasikiliza na watoto wangu. I love the 90s
 
Kichekesho kichekesho,kumtazama chura;
hana mkia hana mkia wala masikiooo...
Ua kaka ua kaka ua kaka ua;
Ua kaka,ua kaka ua kaka uaaa!
 
Hi guys,

me naukumbuka huu, "hesabu ni nzuri sana weeee mwalimu nifundishe siwezi kusahau ee mwalimu ee mwalimu nifundishe"

mwingine "a e i o u hizi ni herufi kuu, tamka kwa sauti kuu, hizi a e i o u"

unazikumbuka nyingine??????????

Ile ilikuwa Tanzania tamu mno. Elimu ilikuwa juu sana, kila mtoto aligawiwa daftari, peni, darasani mwl alikuja na vitabu vinavyotosha wanafunzi wote, madawati yalitosha na kila shule ilikuwa na reserve ya madawati. mzee wangu alikuwa polisi likizo zao ni miezi 3 aisee ilikuwa nooma maana niliingia std one sijui kusoma wala kuandika, mwezi wa nane toka nianze std 1 likizo yake ikaja. Kwanza nilikuwa na nywele ndefu akanipiga pala kwa mkasi ikawa daily mazoezi ya kusoma na kuandika na hesabu! Wimbo alonifundisha ni aeiou hizo ni herufi kuu tamka kwa sauti kuu! dah sitausahau huo wimbo
 
tulikuwa tunakatikaje hapo sasa, je ule wa kuruka kamba wa ngurumo, ngurumo, mpaka maputo, sanda na ikweta mamaa ikwetaeee, aineme, ainuke, ainame salome........... nimesahau yeuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii tulikuwa tunapigwa na mama kila siku kuchelewa kurudi tuition ya mwalimu mndolwa mlimani primary! khaaaaaaaaa! kuruka kamba! we had some good times kwa kweli. morning chit chatters, morning my sugar Asprin!

Hii kitu umenikumbusha mbali sana.....kama sikosei mtiririko ulikuwa kama ilivyo hapo chini; ambapo kuruka upande mmoja mara tatu halafu unaruka tena upande wa pili;

Ngurumo ngurumo,
Hadi Maputo,
Isanga ikweta mamaa,
Ikweta eeeh,
Ainaame,
Ainuuke,
Ainame Salome sakina malembe,
Sure vaa lubega shika usinga tucheze zembwela,
Anatoa madoido kama hutaki sogea mbele.....
 
hii kitu umenikumbusha mbali sana.....kama sikosei mtiririko ulikuwa kama ilivyo hapo chini; ambapo kuruka upande mmoja mara tatu halafu unaruka tena upande wa pili;

ngurumo ngurumo,
hadi maputo,
isanga ikweta mamaa,
ikweta eeeh,
ainaame,
ainuuke,
ainame salome sakina malembe,
sure vaa lubega shika usinga tucheze zembwela,
anatoa madoido kama hutaki sogea mbele.....
mulemule besti! Looool! Long time sanaaaaa!
 
Umepotelea wapi mkuu wangu au ubusy nini umenishangazaje


hahahahahahahahhahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa


bai shoo alavyu bebi the bebi tuze samu samu tuzeyona zeyona tuzemen zemen tuzeputi zeya telewani ntu siriii tatakona terewantu hahahahhaaaaaa
hujambo cheupe?
 
HEEEEEEEEEEEEEE
2Q==
index.jpgUMEPOTELEA WAPI NA AHAPA NAKUONA HAPA HIVI NI WEWE BISHANGA AU NI MWINGINE AU NAOTA MIE
Nostalgia.......
 
Back
Top Bottom