Unaweza kunipenda bila kuniona?.....

Unaweza kunipenda bila kuniona?.....

Ahsante kwa ushauri dadaangu..
Lakini wanasemaga kuna 'telepathy'..yaani kuna wakati 'avatars' zinazungumza kumhusu mhusika..
Hebu fuatilia utaniambia...

Mkuu Telepathy haiko kwenye MAPENZI kama unavyofikiri, wataalamu wanasema telepathy ipo kwenye damu hasa kwa akina mama, inayobashiri kwa wanao...over..
 
Avatar inaweza onekana ni picha tu... Lakini si kweli.. Inawakilisha personality ya mtu. Na hiyo personality huwa mwenye avatar anachagua kuwa anataka awe natural ama fake.

Mara nyingi kwa mchangiaji ambaye ni hodari sana, kama ile personality kajenga ni fake (unakuta once in a while kwa wale makini kuwasoma watu) humsoma true colors. HASA ambao hujenga personalities za kujisafisha asivyo... Mfano mtu ambaye anapenda sana ngono (kujifanya hapendi); ama mtu ambaye anakumbatia sana ushoga (kujifanya hakumbatii); ama mtu ambaye ni muongo sana (kujifanya ni mkweli na kuaminika).

Uzuri huja kwa mtu ambae yupo natural... Tutolee mfano The Boss... Hatoi maoni kujisafisha au kuonekana ni mzuri. Maoni yake siku zote mara nyingi sana hutoa yale ambayo yapo kichwani kwake kwa masuala yoyote yale iwe mahusiano ama nje ya mahusiano.

Mwisho wa siku unapata traits kama vile The Boss ni Muislam (sababu ikiwa Ramadhani you see the change in him), The Boss ni typical African man(Tokana na misimamo yake juu ya mahusiano upande wa wanaume) , The Boss ana sifa za Uanaume na si za Kivulana (Tokana na kuelewa majukumu yake kama mwanaume kwa kujiuliza mara mbili mbili kama anaweza mwambia afanye maarifa), The Boss ni Charming (kwa kufurahia kila member bila kujalisha ni mgeni); na mengine meeengi....

Huo ni mfano tu... So ikitokea member anapenda traits za such a person awe M/ke ama M/me mwenzie, inatokea tu kuwa atampenda na kumkubali.

Zion Daughter na saudari... Pamoja saana. Mie penda sana nyie pia.
 
Last edited by a moderator:
SnowBall, mimi niungane na Mwl gfsonwin kuwa mtu anaweza kutamani kwa kupitia avatar ya mtu na si kupenda. Kupenda huja baada ya kuonana na mtu physically. Kama itatokea mtu kapenda kupitia avatar na bahati mbaya hiyo avatar haijabeba uhalisia wa mtu aliyependwa, basi ni ukweli usiopingika kuwa siku wakionana ndo itakuwa mwanzo na mwisho wa mahusiano yao ya kimapenzi na baada ya hapo itakuwa ni kukimbiana tu!

Nikupe mfano halisi, ukiweke picha ya mjusi, je mtu anaweza kukupenda kupitia avatar hiyo? Lakini jaribu kuweka avatar yenye mvuto labda wa mdada au mkaka aliyependeza halafu ona matokeo yake yatakavyokuwa. Hili pia nimeliona sana hata kule fb ambako watu huumizana sana kwa kurushiana picha nzuri na kuvutiana na kufikia hatua hata ya kuwa wachumba, ila siku wanayokutana ndo na siku wanayobwagana!

Moyo umeumbwa kupenda kupitia macho kuona na ndiyo maana baadhi ya watu kwa kuona avatar tu hata kama wanajuwa ukweli avatar karibu zote si halisi, basi hujikuta wanaangukia kumzimikia mtu. tabia hii ninaiita ni uvivu wa kufikiri na ni vyema kuwa makini na kuepuka kuiweka mioyo yetu rehani kirahisi namna hii au ktk hatari ya kujeruhiwa kimahusiano.

Nimecheka jamani hapa Duh!
Mtu kaweka Avatar bomba, siku ya kukutana nae, ni kumkimbia mpaka Thread zake hutochangia tena.
 
Last edited by a moderator:
Kaunga naogopa kukita genious ila kiukweli wewe unajua..na unaweza kudadavua...umeichallenge mada vizuri sana...na bainafsi nimekusoma vizuri sana..labda nikuulize kaswali kangu...'hivi wakati mtu anachangua avatar huwa pia anawafikiria waangaliaji wa avatar yake???.......

Aisee!
Avatar.
Mimi nafikiri avatar tunazoweka (ambazo ni picha, na sio zetu), mara nyingi zinaeleza vile tunavyopenda/tamani kuwa na sio jinsi tulivyo.
Zile za vitu, zinaelezea kwa uchache tabia na interests zetu. So still kwa avatar you can learn a lot about the person.
What we post.
Again, kama avatar tunachoandika kwa asilimia zaidi ya nusu; linaelezea nini tunaamini, nini tunafanya au tuna strive kufanya hata kama hatufikii kwa asilimia 90.
What we 'like'
Apart of giving someone a like just to be nice or because l am expected to; zingine zinaelezea tabia zetu.

Hivyo vitu vyote vinachangia kujenga taswira ya mtu kitabia na kumuumba kimuonekano (jinsi tunavyotaka awe).
Issue ya kumpenda mtu ambaye hujaona sura yake, inawezekana kwani unapenda tabia yake ambayo inakuwa expressed kwenye michango yake (hasira, upole, uvumilivu, uarrogant, usweet, msaada etc). Ili kuijua kwa usahihi tabia ya huyo mtu it takes muda n lots of it. Kumtamani mtu, inaambatana zaidi na muonekano wa nje (huenda hapo ndipo mapenzi ya kiavatar yanapokuja na ndiyo yenye disappointment).

So kwa maoni yangu, it is possible to fall in love with a person ambaye hujamuona. Vipofu si wanapenda pia AU??????
 
Last edited by a moderator:
HorsePower naogopa kukuita genious mkubwa..ila umeongea vitu vya maana sana bro..
Lakini labda nikuulize swali moja..kipi kinatangulia siku zote ...'kupenda' au 'kutamani'????

Sijui wengine watalijibu vipi hili swali lako, lakini mimi kwangu "kupenda" ni kupenda na "kutamani" ni kutamini! Kipi kinatangulia? Hii inategema maana kuna uwezekano wa kumpenda mtu bila "kumtamani" na kumtamani mtu bila "kumpenda"! Ukipita sehemu ambayo wako wadada wanajiuza unaweza kuwaona ni namna gani wamejitengeneza kuvutia soko mpaka kufikia hatua ya kutamanisha. Wateja wa watu hawa ni simply watu waliotamani na siyo kupenda! Siamini kama kuna mtu anaweza kumpenda dada poa ktk hali ya kawaida! Ila sikatai kuwa mara chache, tamaa huleta kupenda!

Ktk kufafanua hili, inawezakana kabisa ukampenda mtu na usimtamani! Kuna wangapi ofisini kwako au nyumbani kwako ambao unawapenda kwa jinsi walivyo na heshima au wanavyofanya kazi kwa bidii au wanavyojitahidi darasani? Umeshafikiria kuwatamani? Na kama ni hivyo unaweza kuwatamani wangapi?

Na kuongezea, kutamani hufanyika kwa muda mfupi. Unatamani kitu/mtu akimpata basi, huna shida naye tena! Kumpenda mtu ni kwa muda mrefu. Ktk hali yeyote ile aliyenaye mhusika, unaweza ukampenda na kadiri mnavyoendelea kushirikia ndivyo vivyo upendo unapozidi. Even hapa JF, mimi kuna watu nawapenda simply kwa kusoma michango yao .....! Sijui mwenzangu!!!
 
Wanabodi habari za weekend??

Nakubali ndio MAPENZI ni 'phenomenon' ya ajabu...Mapenzi bana wanasema yanakujaga tu kama mvua...Na wengine wanasema ukipenda waweza kuwa kipofu..nyekundu ukaiona samawati na njano ukaiona kijani...Lakini pamoja na kizungumkuti kinachohusu mapenzi hivi katika hali ya kawaida..'WAWEZA MPENDA MTU KWA KUANGALIA AVATOR YAKE TU???............... Hebu ndugu zangu Eiyer, Nivea , Mr Rocky , Kaunga , Blaine , HorsePower, walimu wangu snowhite na gfsonwin , Mtambuzi , Jipu , saudari , Blue G, Kamanda Kazi, Yegoo na wengineo wengi nisaidieni hapa.....

Inawezekana, especially kwenye early stages. Kwani SnowBall huajwahi kusikia kwa mfano wadada wanasema "mi napenda wanaume weusi warefu"..nk? Hii ina maana akiona picha yako kuwa wewe ni mweusi mrefu 'atakupenda'...
 
Zion Daughter nimekusoma ndugu yangu...hebu imagine
avatar' ya ukweli halaf huyo mtu 'ponits' za kutafuta...unamuweka fungu gani???........

Mie huwaga sibabaishwi na Avatar hata siku moja..japokuwa ukiweka avatar inayoleta walakini hakika ntaanza kuku judge..just imagine mtu kaweka avatar yenywe taswira ya kikojoleo cha mwanaume or something like that!!!Mie hata kama nilikuwa nakuheshimu siku hiyo narudisha heshima sifuri
 
Last edited by a moderator:
Madame B nimependa sana mchango wako mpendwa..
Hivi haijawahi kukutokea ukampenda mtu ukidhani wa jinsia tofauti lakini kuja kugundua ukajua ni wa jinsia yako????

Hyo inatokea sana.
Na huwa ndio majanga tunayokutana nayo huko Chemba.
Ila kuna haja gani ya KE kuweka Avatar au ID ya ME?
Nawe ME kuna haja gani ya kuweka Avatar na ID ya KE?
Hiyo yote yaonesha ni kwa jinsi gani wasivyojiamini.
 
Last edited by a moderator:
AshaDii umeongea mambo mazito saaana...ni kweli kama kuna watu wamekusoma ulivyotaka usomeke basi watakuwa wameshiba kwa nasaha zako...Hapo nilipobold ndipo nimeshindwa kukusoma katikati ya mistari..please kama hutajali hebu rudia kwa faida ya mimi mdogo wako na wengine ambao wangependa wafaidike na nasaha zako.....

Avatar inaweza onekana ni picha tu... Lakini si kweli.. Inawakilisha personality ya mtu. Na hiyo personality huwa mwenye avatar anachagua kuwa anataka awe natural ama fake.

Mara nyingi kwa mchangiaji ambaye ni hodari sana, kama ile personality kajenga ni fake (unakuta once in a while kwa wale makini kuwasoma watu) humsoma true colors. HASA ambao hujenga personalities za kujisafisha asivyo... Mfano mtu ambaye anapenda sana ngono (kujifanya hapendi); ama mtu ambaye anakumbatia sana ushoga (kujifanya hakumbatii); ama mtu ambaye ni muongo sana (kujifanya ni mkweli na kuaminika).

Uzuri huja kwa mtu ambae yupo natural... Tutolee mfano The Boss... Hatoi maoni kujisafisha au kuonekana ni mzuri. Maoni yake siku zote mara nyingi sana hutoa yale ambayo yapo kichwani kwake kwa masuala yoyote yale iwe mahusiano ama nje ya mahusiano.

Mwisho wa siku unapata traits kama vile The Boss ni Muislam (sababu ikiwa Ramadhani you see the change in him), The Boss ni typical African man(Tokana na misimamo yake juu ya mahusiano upande wa wanaume) , The Boss ana sifa za Uanaume na si za Kivulana (Tokana na kuelewa majukumu yake kama mwanaume kwa kujiuliza mara mbili mbili kama anaweza mwambia afanye maarifa), The Boss ni Charming (kwa kufurahia kila member bila kujalisha ni mgeni); na mengine meeengi....

Huo ni mfano tu... So ikitokea member anapenda traits za such a person awe M/ke ama M/me mwenzie, inatokea tu kuwa atampenda na kumkubali.

Zion Daughter na saudari... Pamoja saana. Mie penda sana nyie pia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Telepathy haiko kwenye MAPENZI kama unavyofikiri, wataalamu wanasema telepathy ipo kwenye damu hasa kwa akina mama, inayobashiri kwa wanao...over..

Hili suala la telepathy mkuu naomba ulianzishie uzi, maana ni refu kidogo...
 
Aisee!
Avatar.
Mimi nafikiri avatar tunazoweka (ambazo ni picha, na sio zetu), mara nyingi zinaeleza vile tunavyopenda/tamani kuwa na sio jinsi tulivyo.
Zile za vitu, zinaelezea kwa uchache tabia na interests zetu. So still kwa avatar you can learn a lot about the person.
What we post.
Again, kama avatar tunachoandika kwa asilimia zaidi ya nusu; linaelezea nini tunaamini, nini tunafanya au tuna strive kufanya hata kama hatufikii kwa asilimia 90.
What we 'like'
Apart of giving someone a like just to be nice or because l am expected to; zingine zinaelezea tabia zetu.

Hivyo vitu vyote vinachangia kujenga taswira ya mtu kitabia na kumuumba kimuonekano (jinsi tunavyotaka awe).
Issue ya kumpenda mtu ambaye hujaona sura yake, inawezekana kwani unapenda tabia yake ambayo inakuwa expressed kwenye michango yake (hasira, upole, uvumilivu, uarrogant, usweet, msaada etc). Ili kuijua kwa usahihi tabia ya huyo mtu it takes muda n lots of it. Kumtamani mtu, inaambatana zaidi na muonekano wa nje (huenda hapo ndipo mapenzi ya kiavatar yanapokuja na ndiyo yenye disappointment).

So kwa maoni yangu, it is possible to fall in love with a person ambaye hujamuona. Vipofu si wanapenda pia AU??????

Kwa hyo avatar na michango yako yoote unadhan nitaacha kukupenda? Sijawah kukuona, sijawah kuzungumza nawe ila NAKUPENDA
 
Kaunga naogopa kukita genious ila kiukweli wewe unajua..na unaweza kudadavua...umeichallenge mada vizuri sana...na bainafsi nimekusoma vizuri sana..labda nikuulize kaswali kangu...'hivi wakati mtu anachangua avatar huwa pia anawafikiria waangaliaji wa avatar yake???.......

Of course tunawafikiria, anyway some of us are conscious on what we use na jinsi watu watakavyoitafsiri. Some don't care and some don't think kihivyo.
Asante kwa compliment SnowBall, na wewe ni kati ya watu MMU ninaowakubali sana na kuwategemea.
 
Last edited by a moderator:
HorsePower nimekusoma bro...big up
Haka ka kupenda na nakutamani ni katopiki kananisumbuaga sana...

Sijui wengine watalijibu vipi hili swali lako, lakini mimi kwangu "kupenda" ni kupenda na "kutamani" ni kutamini! Kipi kinatangulia? Hii inategema maana kuna uwezekano wa kumpenda mtu bila "kumtamani" na kumtamani mtu bila "kumpenda"! Ukipita sehemu ambayo wako wadada wanajiuza unaweza kuwaona ni namna gani wamejitengeneza kuvutia soko mpaka kufikia hatua ya kutamanisha. Wateja wa watu hawa ni simply watu waliotamani na siyo kupenda! Siamini kama kuna mtu anaweza kumpenda dada poa ktk hali ya kawaida! Ila sikatai kuwa mara chache, tamaa huleta kupenda!

Ktk kufafanua hili, inawezakana kabisa ukampenda mtu na usimtamani! Kuna wangapi ofisini kwako au nyumbani kwako ambao unawapenda kwa jinsi walivyo na heshima au wanavyofanya kazi kwa bidii au wanavyojitahidi darasani? Umeshafikiria kuwatamani? Na kama ni hivyo unaweza kuwatamani wangapi?

Na kuongezea, kutamani hufanyika kwa muda mfupi. Unatamani kitu/mtu akimpata basi, huna shida naye tena! Kumpenda mtu ni kwa muda mrefu. Ktk hali yeyote ile aliyenaye mhusika, unaweza ukampenda na kadiri mnavyoendelea kushirikia ndivyo vivyo upendo unapozidi. Even hapa JF, mimi kuna watu nawapenda simply kwa kusoma michango yao .....! Sijui mwenzangu!!!
 
Last edited by a moderator:
Hebu angalia comment anazotoa King'asti, Nivea, @lara1 halafu linganisha na avatari zao?

Kama utakuwa unampenda mtu kutokana na avatar yake, itakuwaje kwa wabadilisha avatar kama Nicas Mtei, @ blaine na Blue G. Lazima utageuka pendapenda.

Hahahahaha. Sitaki kuwa defined kutokana na avatar. Ni tatizo smtymz.
 
Last edited by a moderator:
Mashalah ingawa mimni ni mdada mwenzako lakini nimeipenda Avarter yako na imejionesha wazi hata ulivyochangia ni mtu wa hekima uliye katika Ndoa Imara
Kwangu naamini Avarter huwa inam-discribe mtu alivyo
Asante sana shosti wangu
Bora umesema ukweli Malkia wa Sheba ni wadada wachache sana wanaoweza kukubali uzuri wa Mwanamke mwenzake na ni kweli kuwa avarter ndio inayomuonesha mtu alivyo
 
Last edited by a moderator:
Me naona ni ngumu sana labda kusema umemtamani kupitia avatar aliyo weka na wengi wanaweka avatar pengine zinaweza zikawa zinawaelezea walivyo japo si asilimia mia!

Ubaya wakutamani kupitai avatar unapo kuja kumuona mtu alaf hakukidhi matarajio yako ndio hapo unapo vunjika moyo kabisa au kumkacha mhusika!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom