Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Naomba kufahamu utaratibu wa kuwa na luku ya peke yangu katika fremu ya Biashara. Nina matumizi makubwa ya umeme ukilinganisha na fremu zingine. Natamani kufahamu hili ili kuondoa migogoro ya siku za mbeleni. Asante TANESCO
Kitu cha kwanza tafuta fundi atenganishe mifumo,namaanisha akutoe kwenye mfumo wa pamoja akutengenezee wa kwako peke yako,
hapo utahitaji kuingia gharama za kununua main switch yenye earth leakage circuit breaker,wire 10-16mm sq mita kadhaa kutegemea hiyo main switch yako itawekwa umbali gani toka kwenye mita. Earth rod na earth wire, na wire 1.5mm sq na 2.5mmsq kwa ajili ya kuextend waya zako endapo itatakiwa hivyo.
Baada ya hapo huyo fundi atakuchorea mchoro wa wiring aliyoifanya na kuithibitisha kwa muhuri wake wa usajili(contractor). Kisha utaenda Tanesco
utapeleka maombi utapewa fomu za kujaza,utazijaza,watakuja kukagua na kuchora michoro yao.
Baada ya hapo watakupa makadrio ya fedha unazotakiwa kulipia ili uunganishwe na nishati hiyo.
Nadhani kwa hapa utapata mwangaza. kinyume na hapo nitafute inbox.
 
Bila shaka wewe ni fundi umeme
Mita za umeme zipo constant, kadri matumizi yako ni makubwa hvyo cost zinakuwa nyingi, vtu vya umeme vinakuwa rated na kitu kina inaitwa "watt" hapo ndipo siri kubwa ilipofichwa ambayo watu wengi hawaijui, soma taa zako zina watt ngapi then zidisha mara masaa ya kuwaka kwake then gawanya kwa 1000 hapo ndipo utajua chombo chako kinatumia unit ngapi then baada yahapo unaweza kupunguza matumizi. " watt×hrs/ 1000 = total unit consumption
 
Inawezakana kutumia umeme huo, nina familia ya watu 3 kwa mwezi natumia umeme wa 5000 sawa na unit 41 nawasha friji, feni 3, tv 2, rice cooker, brender, pump ya maji, pasi na vacuume cleaner, natumia hizo unit 41 confortably hadi mwezi mwingine, maji natumia unit 3 hadi 4 kwa mwezi
This is too good to be true.
 
Inawezakana kutumia umeme huo, nina familia ya watu 3 kwa mwezi natumia umeme wa 5000 sawa na unit 41 nawasha friji, feni 3, tv 2, rice cooker, brender, pump ya maji, pasi na vacuume cleaner, natumia hizo unit 41 confortably hadi mwezi mwingine, maji natumia unit 3 hadi 4 kwa mwezi
huu ni uwongo, unless kama ivyo vifaa haviwashwi mwezi mzima
friji peke yake jipya la around 50W inalamba unit 1 kila siku ( likiwa on 24 hrs )
 
Back
Top Bottom