Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Unit 1.5 kwa siku tupo wapangaji vyumba vitatu mimi kwangu nina tv music pas fridge japo huwa nazima wakat wa night na kuwasha wakat wa day hatushindi nyumban na wote ni bachelors nadhani hiyo ndo sabb umeme kidog unatumika
 
Ah sema hapo sio mbaya mkuu kama madude yote unayo hayo. Mi nataka nijue AC inakula unit ngapi kwa siku!
Ac inategemeana na capacity yake pamoja a technology iliyotumika kutengenezea Kuna zinazotumia chini ya unit 3 kwa Siku hii nazungumzia kwa chumba kimoja .
Samsung na Lg wana efficient ac system Ila huwa ni ghali .
 
Ac inategemeana na capacity yake pamoja a technology iliyotumika kutengenezea Kuna zinazotumia chini ya unit 3 kwa Siku hii nazungumzia kwa chumba kimoja .
Samsung na Lg wana efficient ac system Ila huwa ni ghali .
Mkuu mfano mi naplan kununua Hisense ya BTU 12000 nina chumba cha 15*15 inaweza kuwa inakula umeme kiasi gani?
 
unatumia ngapi
Nilikuwa nikiweka umeme wa sh. 10,000 (unit 28.1) ulikuwa unakaa wiki moja hadi mbili. Na awali, ulikuwa unakaa mpaka tunasahau. Ghafla umeme huo unaweza usikatize wiki.
Kakague earthing system yako huenda kuna shida, kwa vifaa hivyo unatakiwa kutumia angalau 1 au 2
Kwa kweli itabidi kufanya hivyo. Tuliweka waya wa Earth mnene, na earth-rod ya ukweli, kwa maelezo kwamba inapunguza ulaji wa umeme. Mwanzoni mambo yalikuwa safi. Umeme unatumika mdogodinyo. Siku hizi sijui imekuwaje. Itabidi kutekeleza wazo lako la kumuita fundi kukagua mifumo.
 
Mkuu kuna haja nianzishw uzi nijibiwe zaidi. Na vipi kuhusu zile inverter types! Naona kama ni Technology ambayo inapigiwa chapuo kuwa ni energy saver.
Anzisha mkuu, naamini utapata majibu mazuri. Japo sio fani yangu haswa ila naamini wapo wataalamu wa refrigaration na a/c watakujibu.

Hiyo niliyokuambia hapo ni inverter type. Ila inatumia hizo units kwasababu pia hicho chumba kina vifaa vinagenerate heat ya kutosha.
 
Naomba kufahamu utaratibu wa kuwa na luku ya peke yangu katika fremu ya Biashara. Nina matumizi makubwa ya umeme ukilinganisha na fremu zingine. Natamani kufahamu hili ili kuondoa migogoro ya siku za mbeleni. Asante TANESCO
 
Umeme wa 1000
Siku 2 unit 2.9
Tv, redio, pass ,taa , kucharge simu
 
Back
Top Bottom