Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Mkuu mfano mi naplan kununua Hisense ya BTU 12000 nina chumba cha 15*15 inaweza kuwa inakula umeme kiasi gani?
12,000BTU ni roughly 3.5kW = 3500W, kwa power ya namna hiyo kama unatumia hiyo AC 10hrs mfulilizo maana yake ni kwamba 3500W X 10hrs = 35,000Whr sawa na 35kWh. Unit moja ni 1kWh hivyo kwa masaa kumi itatumia 35Units. Hapo sijaweka factor ya size ya room which is also very important.

Kama nimekosea nirekebishwe fastaaa!
 
Naomba kufahamu utaratibu wa kuwa na luku ya peke yangu katika fremu ya Biashara. Nina matumizi makubwa ya umeme ukilinganisha na fremu zingine. Natamani kufahamu hili ili kuondoa migogoro ya siku za mbeleni. Asante TANESCO
Ongea na mwenye frame, siku hizi tanesco hawakusajili wewe kama ni mpangaji tu, lazima authorization itoke kwa mwenye nyumba na majina kwenye mita yatakuwa yake...
 
12,000BTU ni roughly 3.5kW = 3500W, kwa power ya namna hiyo kama unatumia hiyo AC 10hrs mfulilizo maana yake ni kwamba 3500W X 10hrs = 35,000Whr sawa na 35kWh. Unit moja ni 1kWh hivyo kwa masaa kumi itatumia 35Units. Hapo sijaweka factor ya size ya room which is also very important.

Kama nimekosea nirekebishwe fastaaa!
Dah kama ni hivyo watu wasingemiliki AC!
BTU zinaongeza tu cooling effect per room size. Ila sidhani kama zinakula umeme kiasi hiko!
 
Niwakumbushe tu kua
Vitu vya umeme havipimwi kwa mtazamo wake au ukubwa wake vinapimwa kwa watts inayoandikwa kwa kifaa husika!
Kuna kasumba imejijenga kwenye akiri za watu
Utasikia mim sina fridge!
Ila nikukumbushe tu kua huenda mwingine ana fridge ya watt65
Nayo inakifaa maalumu chakuhisi kama baridi ipo level sawa inajikata
Kipindi imejikata inakua on
Ila complesa haitumii umeme hivyo ni sawa na kusema fridge haifanyi kazi
Ila meingine ana taa tu! Ila za watts 40 zipo 6 je
Nan anaetumia umeme sana
Kwahyo kwa matumizi bora ya umeme ni bora kusoma real printed data kuhusu kifaa husika!
 
Unatumia yuniti ngapi za LUKU kwa siku?

Wajemeni, siku hizi naona kama mita ya umeme inakimbia. Hivi kwa wastani yuniti ngapi za LUKU hutumika kwa nyumba ya kawaida tu?
Mimi natumia 1.5 per 24hours au mpaka unit 2 kwa siku
 
12,000BTU ni roughly 3.5kW = 3500W, kwa power ya namna hiyo kama unatumia hiyo AC 10hrs mfulilizo maana yake ni kwamba 3500W X 10hrs = 35,000Whr sawa na 35kWh. Unit moja ni 1kWh hivyo kwa masaa kumi itatumia 35Units. Hapo sijaweka factor ya size ya room which is also very important.

Kama nimekosea nirekebishwe fastaaa!
Kuna kitu kinaitwa Energy efficiency ratio umesahau. Ni kitu muhimu sana hapo. Mfano upate a/c yenye rating ya 8. Utachukua hiyo 35kWh gawanya kwa 8 ambayo ni average 4.4kwh.
Hapo ndio zitakuja other factors kama ukubwa wa chumba na joto kiasi gani linazalishwa humo ndani
 
Dah kama ni hivyo watu wasingemiliki AC!
BTU zinaongeza tu cooling effect per room size. Ila sidhani kama zinakula umeme kiasi hiko!

Binafsi sina uwezo wa kutumia AC kwa sababu wengi niliongea nao wanaomiliki AC wanasema umeme wa 10,000 (28+units)kwa siku hautoshi, especially kama unatumia nonstop.

Umeshawahi kuishi nyumba yenye AC na kununua umeme wake? Labda unaweza kuwa na practical experience.
 
Kuna kitu kinaitwa Energy efficiency ratio umesahau. Ni kitu muhimu sana hapo. Mfano upate a/c yenye rating ya 8. Utachukua hiyo 35kWh gawanya kwa 8 ambayo ni average 4.4kwh.
Hapo ndio zitakuja other factors kama ukubwa wa chumba na joto kiasi gani linazalishwa humo ndani

Asante mkuu, energy efficiency ratio!..kwa hiyo 4.4kwh inaweza kuwa reasonable sio.?

Pia nataka watu wenye practical experience ya kutumia AC, hasa za nyumbani sio ofisini.
 
Binafsi sina uwezo wa kutumia AC kwa sababu wengi niliongea nao wanaomiliki AC wanasema umeme wa 10,000 (28+units)kwa siku hautoshi, especially kama unatumia nonstop.

Umeshawahi kuishi nyumba yenye AC na kununua umeme wake? Labda unaweza kuwa na practical experience.
Mkuu sijawahi miliki AC ila kwa umeme huo ni kiboko, ina maana AC inakula umeme namna hio!
 
12,000BTU ni roughly 3.5kW = 3500W, kwa power ya namna hiyo kama unatumia hiyo AC 10hrs mfulilizo maana yake ni kwamba 3500W X 10hrs = 35,000Whr sawa na 35kWh. Unit moja ni 1kWh hivyo kwa masaa kumi itatumia 35Units. Hapo sijaweka factor ya size ya room which is also very important.

Kama nimekosea nirekebishwe fastaaa!
BTU 12000 ni 1.25hp sawa na 0.95kw,hiyo ni cooling capacity ya AC,Tukiweka factor za efficiency tuseme input power kwa AC mpya inaweza kuwa 1.2kw,equivalent to 1.2 unit per hour.factor za ukubwa wa chumba zita determine AC iwake continously kwa muda gani.so kwa wastani AC ya ukubwa huo kwa siku inaweza kula 15units sawa na sh 6000 za kitanzania=serengeti lite 3=liter 3 za petrol.so kupanga ni kuchagua,kakae bar unywe bia tatu,ukirudi ukalale kwenye joto,weka mafuta kwenye gari ukapige misele huku ukiliwazwa na AC ya gari ukirudi ulale kwenye kwenye joto au uweke umeme nyumbani wa kutosha ushinde umelala na kipupwe😂😂😂
 
Unatumia yuniti ngapi za LUKU kwa siku?

Wajemeni, siku hizi naona kama mita ya umeme inakimbia. Hivi kwa wastani yuniti ngapi za LUKU hutumika kwa nyumba ya kawaida

Unatumia yuniti ngapi za LUKU kwa siku?

Wajemeni, siku hizi naona kama mita ya umeme inakimbia. Hivi kwa wastani yuniti ngapi za LUKU hutumika kwa nyumba ya kawaida tu?
Mita za umeme zipo constant, kadri matumizi yako ni makubwa hvyo cost zinakuwa nyingi, vtu vya umeme vinakuwa rated na kitu kina inaitwa "watt" hapo ndipo siri kubwa ilipofichwa ambayo watu wengi hawaijui, soma taa zako zina watt ngapi then zidisha mara masaa ya kuwaka kwake then gawanya kwa 1000 hapo ndipo utajua chombo chako kinatumia unit ngapi then baada yahapo unaweza kupunguza matumizi. " watt×hrs/ 1000 = total unit consumption
 
Back
Top Bottom