hiyo ya kuku iko namna ya kuitengua na haina mashabiki wengi siku hizi...........iko hiyo unakuta kijana shababi kwelikweli,halafu ana mahela yakutosha...........anakuwa na wadada wengi wengi kwenye gari halafu kumbe jongoo hapndi mtungi!!...kijana ambae hana familia,anataka utajiri anaenda kwa mganga,sharti analopewa ni kutoa nguvu zake za kiume ila anapata utajiri wa haraka na mwingi kwelikweli!
Mtoa mada wewe ni mshirikina na una mapepo! Acha kuwaaminisha watu uongo.
Mimi ninafanya biashara hapa Tunduma, hakuna tajiri asiyejishughulisha hapa, watu tunajituma sana.
Siri ya mafanikio hapa ni biashara hasa za magendo, vipodozi, na bureau de change za kienyeji.
Hakuna anayeweza kuthibitisha huo uchawi wenu.
Wana JF tuwe makini na hizi rumours, tujitume katika kazi ndio msingi wa mafanikio.
Tupo Tunduma na tumekula Christmas hapa huku tukisubiri mwaka mpya
Mambo ya Tunduma yanatisha kama sio kushangaza
Tunduma ndio sehemu pekee Tanzania kama sio Africa ambayo vijana wadogo kabisa ni matajiri wa kutisha na wengi wao hawana hata elimu ya darasa la saba
baada ya kufanya utafiti mdogo tu kuhusisha watu kama kumi tumegundua kuina jambo linaloendelea hapa Tunduma na Mbeya ambalo bado halijawekwa wazi
watu wa tunduma hasa vijana wanatumia nguvu za giza au uchawi kupata mali nyingi wanazomiliki,kuna mganga maarufu hapa ambaye anafuga jogoo mkubwa sana mwenye afya ya kutosha
ukitaka utajiri unaenda kwa huyu mganga halafu anabashiri siku zako za kuishi duniani zimebakia ngapi
akishakupa idadi ya siku zako zilizobakia duniani anamleta jogoo wake mwenye afya tele
anarusha mahindi sawasawa na idadi ya miaka yako iliyobakia duniani.jogoo anaruhusiwa kudonoa mahindi yale,
kama miaka yako ya kuishi duniani ilibakia 10,mahindi kumi yanarushiwa jogoo,anadonoa na kula baadhi ya mahindi,akila mahindi matano ina maana utapewa utajiri na utaishi miaka mitano baada ya hapo utakufa
ile miaka mitano iliyobaki utaenda kuwatumikia wakubwa waliokupa huo utajiri,kuna mahimbo ya madini Congo DRC ndiko unakopelekwa
tulipoulizia maisha ya huko machimboni tuliambiwa kule unakunywa maji kila siku huku ukipiga kazi masaa 24
hiyo ndio taarifa ya Tunduma mji uliojaa vijana waliokata tamaa na kuamua kujitoa mhanga
hii taarifa ni ya kweli na tumefanya utafiti wa kutosha
Nimewahi kusikika hiyo! Ni balaa! Akila hindi moja je? Inaruhusiwa kukata rufaa kama hukubaliani na idadi ya mahindi yaliyoliwa na jogoo? If yes I could also try, akila chini ya mahindi arobaini nabadili mawazo.
Regards
Kwa hiyo ni kweli??Na hizo hela wanapata kweli au ndo kujipa matumaini kama ya kikombe cha babu??
umechanganya madesa. mwakipande alikuwa anaishi makete tarafa ya lupila. kawatajirisha sana wakinga...kwa sasa ni marehemu. but huo utajiri wa tunduma hiyo ni kweli na unajulikana sana kwa jina la utajiri wa mkataba.infact wewe hutaufaidi but ndugu zako ndo wanaenjoy....huyo mzee anaitwa Mwakipande
hiyo kitu nishasikia siku nyingi ilianzia nigeria iakeletwa uku,mbeya kuna jamaa fulani aliuwaga na mabasi yanaitwa matema beach nasikia naye utajiri wake aliupata kwa njia za waganga,alivyokosea masharti akafulia mwanzo alikuwa nauza karanga za kutembeza ghafla akanunua mbus na malori,maduka,ayo mambo inawezekana kweli yapo,tanzania kila kitu kinawezekana tu
98% ya watanzania ni washirikina.source Cnn.