Unataka Utajiri? Njoo Tunduma haraka!

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,889
3,412
Tupo Tunduma na tumekula Christmas hapa huku tukisubiri mwaka mpya.Mambo ya Tunduma yanatisha kama sio kushangaza
Tunduma ndio sehemu pekee Tanzania kama sio Africa ambayo vijana wadogo kabisa ni matajiri wa kutisha na wengi wao hawana hata elimu ya darasa la saba.

Baada ya kufanya utafiti mdogo tu kuhusisha watu kama kumi tumegundua kuina jambo linaloendelea hapa Tunduma na Mbeya ambalo bado halijawekwa wazi watu wa Tunduma hasa vijana wanatumia nguvu za giza au uchawi kupata mali nyingi wanazomiliki.Kuna mganga maarufu hapa ambaye anafuga jogoo mkubwa sana mwenye afya ya kutosha ukitaka utajiri unaenda kwa huyu mganga halafu anabashiri siku zako za kuishi duniani zimebakia ngapi akishakupa idadi ya siku zako zilizobakia duniani anamleta jogoo wake mwenye afya tele anarusha mahindi sawasawa na idadi ya miaka yako iliyobakia duniani.

Jogoo anaruhusiwa kudonoa mahindi yale, kama miaka yako ya kuishi duniani ilibakia 10,mahindi kumi yanarushiwa jogoo,anadonoa na kula baadhi ya mahindi,akila mahindi matano ina maana utapewa utajiri na utaishi miaka mitano baada ya hapo utakufa ile miaka mitano iliyobaki utaenda kuwatumikia wakubwa waliokupa huo utajiri,kuna machimbo ya madini Congo DRC ndiko unakopelekwa tulipoulizia maisha ya huko machimboni uliambiwa kule unakunywa maji kila siku huku ukipiga kazi masaa 24.

Hiyo ndio taarifa ya Tunduma mji uliojaa vijana waliokata tamaa na kuamua kujitoa mhanga.

Hii taarifa ni ya kweli na tumefanya utafiti wa kutosha.
 
hiyo ya kuku iko namna ya kuitengua na haina mashabiki wengi siku hizi...........iko hiyo unakuta kijana shababi kwelikweli,halafu ana mahela yakutosha...........anakuwa na wadada wengi wengi kwenye gari halafu kumbe jongoo hapndi mtungi!!...kijana ambae hana familia,anataka utajiri anaenda kwa mganga,sharti analopewa ni kutoa nguvu zake za kiume ila anapata utajiri wa haraka na mwingi kwelikweli!
 
@episodes,

Nimewahi kusikika hiyo! Ni balaa! Akila hindi moja je? Inaruhusiwa kukata rufaa kama hukubaliani na idadi ya mahindi yaliyoliwa na jogoo? If yes I could also try, akila chini ya mahindi arobaini nabadili mawazo.

Regards
 
Hiyo ya punje za mahindi nmeshaisikia. Ila mm niliisikia iko sana makambako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tupo Tunduma na tumekula Christmas hapa huku tukisubiri mwaka mpya
Mambo ya Tunduma yanatisha kama sio kushangaza
Tunduma ndio sehemu pekee Tanzania kama sio Africa ambayo vijana wadogo kabisa ni matajiri wa kutisha na wengi wao hawana hata elimu ya darasa la saba
baada ya kufanya utafiti mdogo tu kuhusisha watu kama kumi tumegundua kuina jambo linaloendelea hapa Tunduma na Mbeya ambalo bado halijawekwa wazi
watu wa tunduma hasa vijana wanatumia nguvu za giza au uchawi kupata mali nyingi wanazomiliki,kuna mganga maarufu hapa ambaye anafuga jogoo mkubwa sana mwenye afya ya kutosha
ukitaka utajiri unaenda kwa huyu mganga halafu anabashiri siku zako za kuishi duniani zimebakia ngapi
akishakupa idadi ya siku zako zilizobakia duniani anamleta jogoo wake mwenye afya tele
anarusha mahindi sawasawa na idadi ya miaka yako iliyobakia duniani.jogoo anaruhusiwa kudonoa mahindi yale,
kama miaka yako ya kuishi duniani ilibakia 10,mahindi kumi yanarushiwa jogoo,anadonoa na kula baadhi ya mahindi,akila mahindi matano ina maana utapewa utajiri na utaishi miaka mitano baada ya hapo utakufa
ile miaka mitano iliyobaki utaenda kuwatumikia wakubwa waliokupa huo utajiri,kuna mahimbo ya madini Congo DRC ndiko unakopelekwa
tulipoulizia maisha ya huko machimboni tuliambiwa kule unakunywa maji kila siku huku ukipiga kazi masaa 24
hiyo ndio taarifa ya Tunduma mji uliojaa vijana waliokata tamaa na kuamua kujitoa mhanga
hii taarifa ni ya kweli na tumefanya utafiti wa kutosha
Uongo tu wa kuwaaminisha watu na kuwafariji..Huo utajiri wa kutisha mbona hatujasikia.Hiyo Tunduma si ingekuwa kama Marekani basi au Dubai.
 
Some people are deluded
Gaijin I was blessed with a chance to live in Mbeya for some two good years, This is a story I have been hearing al along but sikubahatika kufanya uchunguzi wa kina kama mleta mada.

Ninaachoomba mleta mada anieleze alifanya vipi huo uchunguzi? ulienda kwa huyo mganga? ulipewa taarifa na m2 aliyewahi kwenda? Kwani wanatoaga hizo ''siri''?
 
Last edited by a moderator:
Tupo Tunduma na tumekula Christmas hapa huku tukisubiri mwaka mpya
Mambo ya Tunduma yanatisha kama sio kushangaza
Tunduma ndio sehemu pekee Tanzania kama sio Africa ambayo vijana wadogo kabisa ni matajiri wa kutisha na wengi wao hawana hata elimu ya darasa la saba
baada ya kufanya utafiti mdogo tu kuhusisha watu kama kumi tumegundua kuina jambo linaloendelea hapa Tunduma na Mbeya ambalo bado halijawekwa wazi
watu wa tunduma hasa vijana wanatumia nguvu za giza au uchawi kupata mali nyingi wanazomiliki,kuna mganga maarufu hapa ambaye anafuga jogoo mkubwa sana mwenye afya ya kutosha
ukitaka utajiri unaenda kwa huyu mganga halafu anabashiri siku zako za kuishi duniani zimebakia ngapi
akishakupa idadi ya siku zako zilizobakia duniani anamleta jogoo wake mwenye afya tele
anarusha mahindi sawasawa na idadi ya miaka yako iliyobakia duniani.jogoo anaruhusiwa kudonoa mahindi yale,
kama miaka yako ya kuishi duniani ilibakia 10,mahindi kumi yanarushiwa jogoo,anadonoa na kula baadhi ya mahindi,akila mahindi matano ina maana utapewa utajiri na utaishi miaka mitano baada ya hapo utakufa
ile miaka mitano iliyobaki utaenda kuwatumikia wakubwa waliokupa huo utajiri,kuna mahimbo ya madini Congo DRC ndiko unakopelekwa
tulipoulizia maisha ya huko machimboni tuliambiwa kule unakunywa maji kila siku huku ukipiga kazi masaa 24
hiyo ndio taarifa ya Tunduma mji uliojaa vijana waliokata tamaa na kuamua kujitoa mhanga
hii taarifa ni ya kweli na tumefanya utafiti wa kutosha
Huwezi kufanya utafiti wa mambo ya kichawi wakati wewe si mchawi,umebakiza miaka mingapi ya kuishi?
 
Nimepamiss Tunduma kwani kuna vijimambo vingi ila vingine ni stori za kwenye kahawa! Utajiri gani wa kutokujenga nyumba nzuri na kuzaa watoto kama siyo ujuha tu wa vijana?
 
Gaijin I was blessed with a chance to live in Mbeya for some two good years, This is a story I have been hearing al along but sikubahatika kufanya uchunguzi wa kina kama mleta mada.

Ninaachoomba mleta mada anieleze alifanya vipi huo uchunguzi? ulienda kwa huyo mganga? ulipewa taarifa na m2 aliyewahi kwenda? Kwani wanatoaga hizo ''siri''?

Nilikuwa rafiki na director mmoja wa documentaries nchi moja huko nje

Akaja Tanzania kufanya documentary kuhusu migodi na mambo ya albino.

Akaenda kwa waganga watatu, watu kwa msururu wanasubiri huduma, wengi wao wachimbaji migodi.

Kwa hiyo kuwa watu wanakwenda kwa waganga hilo halina ubishi kwa Tanzania.

Ila hiyo ya vijana kupata utajiri wa ghafla kutokana na nguvu za giza na kutumikishwa katika migodi huko Congo bila ya "kuonekana ulipo" huku ukiwa unakunywa maji tu, vinaweza kuaminiwa na hao wanaoenda kupata huduma kwa waganga tu si vinginevyo
 
Wengine tumeishi Tunduma zaidi ya miaka hizi ni hadithi tu za abracadabra vijana wanapiga deal za mpakani zikiwemo haramu za unga, dola feki, kuvusha makontena feki vitu washaiba sasa wanadanganya kuwa kuna jogoo sijui nini. Mimi nilikuwa nawatania kuwa ukienda huko unaweza kukuta jogoo anadonoa punche ya mhindi na inapasuka vipande vinne then anakula kimoja maana yake unarobo mwaka. Ila element ya ushirikina siifuti kwa 100% kwani ni sehemu ya maisha ya waafrika. Ila sio kwa kiwango anachosema mtoa uzi.
 
Nimewahi kusikika hiyo! Ni balaa! Akila hindi moja je? Inaruhusiwa kukata rufaa kama hukubaliani na idadi ya mahindi yaliyoliwa na jogoo? If yes I could also try, akila chini ya mahindi arobaini nabadili mawazo.

Regards

ukishaingia kwenye hatua hiyo hakuna kurudi nyuma, ni either usonge mbele kwa kuufaidi huo utajiri kwa miaka hiyo utakayopewa au ufe hapohapo.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom