Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 408
Tupo Tunduma na tumekula Christmas hapa huku tukisubiri mwaka mpya
Mambo ya Tunduma yanatisha kama sio kushangaza
Tunduma ndio sehemu pekee Tanzania kama sio Africa ambayo vijana wadogo kabisa ni matajiri wa kutisha na wengi wao hawana hata elimu ya darasa la saba
baada ya kufanya utafiti mdogo tu kuhusisha watu kama kumi tumegundua kuina jambo linaloendelea hapa Tunduma na Mbeya ambalo bado halijawekwa wazi
watu wa tunduma hasa vijana wanatumia nguvu za giza au uchawi kupata mali nyingi wanazomiliki,kuna mganga maarufu hapa ambaye anafuga jogoo mkubwa sana mwenye afya ya kutosha
ukitaka utajiri unaenda kwa huyu mganga halafu anabashiri siku zako za kuishi duniani zimebakia ngapi
akishakupa idadi ya siku zako zilizobakia duniani anamleta jogoo wake mwenye afya tele
anarusha mahindi sawasawa na idadi ya miaka yako iliyobakia duniani.jogoo anaruhusiwa kudonoa mahindi yale,
kama miaka yako ya kuishi duniani ilibakia 10,mahindi kumi yanarushiwa jogoo,anadonoa na kula baadhi ya mahindi,akila mahindi matano ina maana utapewa utajiri na utaishi miaka mitano baada ya hapo utakufa
ile miaka mitano iliyobaki utaenda kuwatumikia wakubwa waliokupa huo utajiri,kuna mahimbo ya madini Congo DRC ndiko unakopelekwa
tulipoulizia maisha ya huko machimboni tuliambiwa kule unakunywa maji kila siku huku ukipiga kazi masaa 24
hiyo ndio taarifa ya Tunduma mji uliojaa vijana waliokata tamaa na kuamua kujitoa mhanga
hii taarifa ni ya kweli na tumefanya utafiti wa kutosha
Hii kitu ni kweli iko Tunduma na hata Mbeya mjini. Wenyewe ambao wanafurahia huo utajiri wanasema kila kitu kinawezekana 'ujasiri wako tu'. Sasa kuhusu hizo sentensi nilizoweka red, mimi nilipata maelezo tofauti kidogo;
1. Jogoo akichagua mahindi kadhaa, ina maana sawa kuwa utakuwa tajiri wa kufa mtu kwa kipindi hicho. Tofauti inayobaki ni kuwa unafanywa msukule. Muda wa kutumika msukule ukiisha, then unauawa moja kwa moja
2. Kipindi kile ukiwa msukule, wanasema unapewa 'rejesho' unalotakiwa kurudisha kila siku. Hii inatokana na 'matajiri wapya' waliopo kwenye mng'aro ambao wewe unakuwa unawatumikia. Ni kwamba wakati wewe ulipokuwa ukifaidi utajiri ni kuwa kuna watu waliofanywa misukule ndio walikuwa wanakuletea mali, hivyo sasa inakuwa zamu yako kuwatumikia wengine
3. Huo msukule kazi unazofanya ni kuiba kimazingara fedha na vitu vya thamani toka nyumbani kwake i.e. kuchota ule utajiri wake alioucha na kuupeleka kwa mganga ili awagawie 'matajiri wapya'. Na kama haujitoshelezi basi unahamia kuiba kwa ndugu na jamaa zako.
4. Inasemekana pia ukishindwa kufikisha 'rejesho' la muda uliopewa basi unapata viboko vya haja. Kwa hivyo salama yako iwe kuwa 'rejesho' ni dogo kuliko uwezo wa wewe kurejesha, la sivyo kila siku unalalia fimbo