Unapojali watu...



Hapo unawuzia wenzio sanamu badala ya picha au mbuzi kwenye gunia....!!

Wenzio tulishazoea kuwa moyo ukifunguka tu, basi tunakimbia kuingia humo ndani...

Kumbe wako unafunguka lakini watu hawaruhusiwi kuingia????

Hii ni mpya kwa kweli dada ED na wala usiwalaumu hawa jamaaa!!

Babu DC!!
 
Heshima haijengwi chupini, sasa ndio hapo unapoweza kuwagundua wafujaji kutoka kwa wanaume wa kweli. Kwa haki akikulilia hali unaona kabisa jamaa kafa, kaoza huo ushujaa wa kitandani hamuna kitu


Kwani na wewe ni member wa club ya 1947?

Sie tunajua watoto wa dot com ni chu.pi mkononi na zipu wazi wazi??

Haya bwana,

Babu DC!!
 

Hapana nikuwa mimi nakubali ile hali ya kuwa mahusiano hayatakuwa kama nyuma tena, hatokuwa kimbilio langu tena ninapokwazika nitajifikiria mara mbili..............mimi nipo siwezi mchunia hiyo ni juu yake sasa kurekebisha sasa kama anataka urafiki regardless hisia zake
 
Babu DC No means NO..... au siku nyingine NO hubadilika na kuwa YES?


Mbona unaniangusha sasa ndugu yangu BAK??

Kwani wewe hujawahi kukuna na bonge la NO na msonyo juu halafu baada ya muda inabadilika na kuwa YES +++!!

Haya bwana....may be wengine tumekutana na mengi!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Ulikuwa wapi wewe @FP,

Mie namweleza huyu ED...eti anawafungulia moyo marafiki wa kawaida halafu ni wanaume....

Duuuuuhhhh...hapo hata mie ningeuvaa mkenge!!

Babu DC!!
kosa kubwa ni kuwafungulia moyo, rafiki wa kawaida ni rafiki tu. na akilijua hilo tangu mwanzo ni better for him/her. tatizo watu wengi hawajui ku-handle marafiki zao wa jinsia nyingine, anakaa naye in such a way that huyo mtu anakuwa na hisia kwamba mwenzake na feelings naye.
mimi kwa mfano nina marafiki wengi wanaume. na naweza kusema karibu robo tatu ya hao marafiki wameshanitaka kimapenzi na wote nimewakatalia na urafiki unaendelea kama kawaida. kama rafiki yangu The Boss alivyosema kumkasirikia mtu sababu kakutosa ni ushamba. mimi ni mtu mzima na najua mambo ya mapenzi, sio wote wanakutongoza sababu kweli wana shida na hiyo kitu, ukiwa rahisi ukawapa wala hawakatai, ukiwa brave enough ukawanyima hakuna linaloharibika.
shida huwa napata kwa mtu ambaye kweli anaonyesha kukuzimikia, inabidi kukaa naye muda mrefu sana kumwelewesha. kumuacha aumie siyo solution, na kumpa ili tu kumridhisha pia siyo solution.
 
Last edited by a moderator:

Hapa sasa mie nakuachia uwanja @FP,

Kama ni kusema nimeshampa wosia wangu huyu ED.....

Hao jamaa wako kwenye mchakato wa kawaida wa maisha...hawana kosa hata kidogo! Tena asipokuwa mwangalifu yeye ndiye atageuka kuwa mwenye makosa kwa kuwatosa washikaji...

Soon ataambiwa kuwa dada anaringa kuliko mtoto wa Queen!!

Babu DC!!
 

Hapa tunachanganya madawa Babu................kwani ukiingia moyoni unapata access hadi ya kule kwingine? mi navyojua moyo ni mkubwa unaweza accommodate Baba Mama Babu Bibi shangazi mjomba................wewe ukiambiwa unajaliwa na kupendwa basi damu inakimbilia chini? loh! makubwa
 

Sasa mtu wa namna hiyo unamsaidiaje??

Nadhani kuna mtu anaona anapata kila msaada toka kwa ED...kwa nini asipewe na dinner??

Babu DC!!
 

Kwa mtu mwingine ambaye hatuna uhusiano wa damu, sijui kama tunaweza kufunguliana mioyo!

Lazima akinifungulia moyo na kengele ya ikulu italia tu...

Bado sijaelewa huo moyo wako ukoje kwani inaonekana una utajiri wa vyumba...may be hata sie wapita njia tuna pa kupumzikia!!

Babu DC!!
 

Ndio najifunza hivyo mama, lakini ni vibaya kuwajali watu na kuwapenda? Basi ndio nachukua point kutoka kwako na Babu Dark City
 
Last edited by a moderator:

Mbona unakaribishwa sana................lakini usilete ukengefu
 
Uraiani unaweza kufanya hivi, lakini kwa mwajiri ambaye anakuwezesha kujidai mjini hili linaweza kabisa kusababisha kibarua chako kuota majani na vibarua vyenyewe siku hizi ni vya kubembeleza.

Mbona unaniangusha sasa ndugu yangu BAK??

Kwani wewe hujawahi kukuna na bonge la NO na msonyo juu halafu baada ya muda inabadilika na kuwa YES +++!!

Haya bwana....may be wengine tumekutana na mengi!

Babu DC!!
 
Moja nimemueleza, mwengine sijui hata kwa kuanzia kwani huyo nilimchukulia kwa namna ya pekee na ndiye aliyekuwa my confidant ebu can you imagine?

Funga vioo vinginevyo watajua unataka sitaki na kinadada wengi hubadilisha maamuzi yao ya awali kwa kuwa na moyo wa huruma wa kuona kama atawanyima raha, kwa mwanaume mzoefu usipomfungia vioo kila siku atakuja. kikubwa hapa ni kufunga vioo itafika muda atazoea au atampata mtu mwingine ambae atamfanya akusahau na mwisho wa siku mtarudi katika mahusiano ya dada na kaka
 
Ndio najifunza hivyo mama, lakini ni vibaya kuwajali watu na kuwapenda? Basi ndio nachukua point kutoka kwako na Babu Dark City
kujali watu na kuwapenda, ule upendo wa agape siyo mbaya kabisa, na ndo urafiki. mtu hawezi kuwa rafiki yako kama humjali wala kumpenda. lakini matendo yako je yanafanana na mtu anayejali au kupenda kwa agape? au ndo kutega tu watu halafu ndo unasema unawapenda?
 
lakini pia asiwakatalie wote,amkubalie japo mmoja awe kinga yake!!!te te te ha ha ha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…