Kuna Watu ni wabinafsi, ila Mchepuko wangu kazidi. Nimemnyoosha

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
32,254
70,248
Wiki ilopita Mwanamke wangu alikuwa na ziara ya kikazi mikoani kwa gari ya ofisini kwao na wenzie watatu (jumla 4 na dereva wao) kwenda kukagua hesabu za vituo vyao vilivyopo uko mikoani.

Siku ya Jumatano alfajir kanitaarifu Yuko Safarini anarudi. Mida ya jioni kanipigia akinambia wamefika Dodoma CBE kwenye foleni, ila gari Yao imepata shida (imezima ghafla). Wameikokota mpK pembeni Ni Zaid ya saa nzima wanatengeneza ila haiwaki. Akaomba nimtumie nauli Elfu 50 atafte gar nyingine yoyote TU ili mradi arudi dar.

Nikamwambia sio busara umezunguka na wenzio Zaid ya siku 4 mikoani, afu hitilafu Ndogo TU mnarud dar ndo uwaache wenzio barabarani, na Kwasababu Ni ishu ya kiofisi washauriane wawasiliane na boss wao ili awatumie usafir mwngn au nauli watoke pale, gar iende gereji maana walipo Ni mjini kabisa.

Akasema hayo hatak kuskia keshachoka Sana, anataka arud TU dar apumzike. Nikamwambia labda nikuazimishie kwa wakala, ukirudi utamlipa mwnyw au waambie ofsn kwenu walipe Hilo deni. Sioni ulazima wa kuingia gharama zangu kwa Safar ya ofsini kwenu. Akasema sawa nimuazimishie TU akifika atalipa.

Basi nikawasiliana na mangi mmoja anakiduka na mpesa jiran na nyumban kwake,nikamfahamisha kwamba akirud atakuja kulipa mwnyw. Mangi kweli ile pesa elfu 50 akaituma ikaenda.

Siku ya alhamisi nmefunga duka naenda kwake, ikabd nipitie kwa mangi nimnunulie mkate wa chai kesho asbh. Mangi akanikumbushia Lile Deni la efu 50 mpesa, nikamwambia Atakua kajisahau huyu. Ila Naeleka uko uko ntamkumbusha aje alipe, ataileta TU usihofu. Mangi akasema sawa.

Nmefika, Tumefanya ya kufanya, nmemuachia posho ya meza, naaga ikabd nimkumbushe khs Deni la mangi. Akaanza kujichekesha na kunishika kidevu kua nilipe mwnyw Mimi ndo mwanaume wake. Nikamwambia alipe mwnyw au awaambie ofsin kwake walipe, Hilo deni la Safar ya ofisi yao halinulihusu Mimi. Akazid kujichekesha mi nikaaga nikaondoka zangu.

Kesho yake Tena ijumaa naenda kwake, nmepitia mkate kwa mangi mangi ananiulizia ile hesabu yetu.
Ikabd pale pale nimpigie simu mamaJ kumuuliza khs muafaka wa ile Elfu 50 ya mangi, Na Niko kwa mangi MDA huu na anaulizia pesa yake. Akajitetea kua walikua hawajaingiziwa posho yao ya Safar, leo ndo check zao zimetoka. Kwaiyo kesho yake asbh (jumamosi) ataenda kuziprocess benki ili apewe cash na atampitishia Ela yake mchana.
Mangi akaridhika na maelezo yale, akasema sawa. Tukaagana nikaenda kwa mamaJ. Nmefika, nmekaa kdg, stories za Hapa na pale, nmeaga,nmeacha posho ya meza, nmeenda zangu kwangu.

Kesho yake (jumamosi) jion nmefunga mapema nmeenda kwake,nmepita kwa mangi kuchukua mkate. Nikamuuliza Kama Deni lake kalipwa. Akasema
" mwanamke wako Kaja kununua vitu vingine ila kasema khs Deni nikuone wewe, yeye Hana ela. Utalipa wewe".
Dah! Nikaona hizi zishakua danadana. Huyu Mangi ataona sasa tunaidharau biashara yake. Ikabd baada ya kununua mkate na Lile Deni nimlipe pale pale, ila nikamwambia akija kulipa Iyo pesa utanirudishia. Mangi akasema "sawa". Basi nikaenda kwa mamaJ.

Nmefika nmemkuta Yuko chumban anakunywa bia, na seblen mlango uko wazi na Kuna Ela nyingi ( zA Elfu tano tano) ziko kwnyw mkoba na mkoba uko wazi. Ikabd nimuulize khs hizo Ela zimetoka wapi na anajiamini Nini kuacha mlango na mkoba wazi. Akanambia hizo pesa zote Ni million 2, Ni za kwake na wenzake wamelipwa kama posho yao ya safar,kazitoa benki alienda asbh kuprocess check yao ndo amepewa cash hizo Elfu tano tano zote.

Nikasema "kama mmelipwa Hapo safi,sasa Ndo ukalipe na lile Deni lako kwa mangi.Anasumbua Sana"
Akasema "wee Hilo deni silipi mimi, Ni wajibu wako mwanaume wangu kunilipia" huku anacheka.
Nikamwambia "Hilo deni Ni lako" kisha nikaenda zangu kuoga.

Nmemaliza kuoga, nimeaga naondoka, akaulizia khs posho mbona sijaacha.
Nikamwambia
"posho ya kula ntakupatia hiyo kesho, leo tayar ushaharibu hesabu zangu. Nilitoka na Elfu 60 tu ofsini ikiwa na bajeti kamili tayari.
lengo elfu 5 ninunue mikate, niache 15 kwako, niache 25 kwangu, Elfu 10 niende nayo kwenye bendi nikapate na bia mbili tatu na elfu 5 ninunue dawa ya mwanangu ya kikohozi. Pesa inakua imeisha hapo."

"Umezingua Sana pale kwa mangi, Nmeona hadi aibu imebd nimlipe tu mangi elfu 50 yake na baada ya kununua huu mkate. Na Hapa nmebak Elfu 8 TU mfukoni, hii naenda kununua dawa za mwanangu na mkate wa kesho chai nyumbani kwangu Kisha naenda zangu kulala."

"Kwaiyo hapa mfumo wangu mzima leo ushauvuruga na kwenye bendi nilikopanga kwenda siwezi tena. Sina hata pesa Ela ya kinywaji"

Akasema
"Twende tu bendi mi nna hamu na savanna, siku nyng sijazinywa mpenz wangu. wee mbona pale bar unafahamika tu, tutakunywa kesho utalipa au unaenda ATM unatoa Ela hata sio mbali "

Nikamwambia
"Kadi sijabeba nmeacha ofsin,
Afu mambo ya ulevi hayaendi hivyo mpenz wangu, habar za kukopa kopa pombe ovyo Ni Ujinga. Ujue Ulevi Ni gharama, na Kufilisika kwa ulevi kunaanzaga hivyo hivyo kwa kukopa kopa ovyo pombe. Baa Unapaswa kwenda na pesa yako kamili, unakunywa, pesa ikiisha Ulevi aishia Hapo hapo unaenda zako nyumbani kulala"

Akasema,
"Kwan mlnz wangu unahitaj sh ngapi?
Nina cash Hapa nikukope hizi hela za ofsin twende tukanywe, ila ukumbuke unirudishie nisije fukuzwa kazi"

Nikamuuliza
"sawa, kwani hizo pesa zinahitajika lini?"

Akasema
"Kesho kutwa Jumatatu asbh"

Nikasema
"Sawa, Basi Nipe tu cash laki moja, nakufanyia transfer sahv kwny nmb account yako utaenda kurudishia kwenye hiyo Ela ya ofsin kwenu"
Akasema "sawa" na muamala ukasoma kaingiziwa 100,000 kwenye account yake, na yeye akanipa 100,000 cash tukajiandaa, akasema anataka avae gauni kimini flexible ili ajiachie vizur. Nikasema sawa.

Keshavaa akasema hata Simu wala pochi hataki kubeba anasema asijelewa akavipoteza, anataka huko leo aumwagilie Moyo mpk wote uelee pombe. Nikasema sawa.
Basi Tukafunga milango, funguo nikazibeba nikatia kwenye mfuko wa koti langu,simu Yake akaiacha chaji, akapanda gari tukaenda kwenye bendi.

Tumefika kwenye bendi, koti nikaliachia kwenye Gari,tumeingia tumechukua meza yetu, mhudumu wa vinywaji kaja,nmeagiza dusseldorf moja na soda Sprite Moja.
MamaJ kaagiza savanna nne tukaanza kunywa kidg kidg huku mtu wa jikoni akindelea kuandaa mbuzi choma kilo 1.

Sasa wkt tukiendelea kunywa,
Meza ya jiran, wakaja mwanamke na Mwanaume wakiwa na mhudumu akiwahamishia pale kabeba meza kawawekea pale, baadae akaja na vinywaji vyao akawawekea mezani pale wakaendelea kunywa. Mama j kuona mwanamke yule anakunywa amarula, Akasema amezimiss amarula nimnunulie anywe.
Nikamwambia haina shida, malizia kwanza hizi savanna zako 4 Kisha amarula unazotaka zitafata. Akasema POA.

Akatoka kwenda msalani,
Aliporudi akaja na wadada wawili kunitambulisha kwamba kakutana nao chooni ni marafiki zake alikua akiishi nao kule alikohama zamani,kabla hajahamia huku kwa Sasa. wako meza ile wanakunywa (akinionyesha meza flani wamekaa na vijana wawili,mabinti wawili na nafas mbili ziko wazi walikokua wamekaa hao mabinti) Kisha wakarudi kwenye meza yao walikokua.

Sasa tumeendelea kunywa,akiwa bado na savanna ya kwanza, shoga yake mmoja kaja akamuinamia shingoni, akawa Kama anamnongoneza sikioni.
Mamaj akabeba savanna Moja akampatia, sikua na Tatizo na Hilo tukaendelea kunywa.

Ukafika MDA mamaJ akaenda chooni tena, wkt anarudi nikaona kasimama meza ile waliko wale shoga zake. Kisha kaja mezan kwangu na kuchukua savanna mbili na kuwapelekea wale wadada na kurudi kukaa na kuendelea kunywa ile yake Moja.

Mtu wa jikoni akawa ndo kaleta nyama zetu, zilipofika mamaJ kagida haraka ile savanna yake na kuimalizia kisha kamuita mhudumu kamuagiza alete amarula 4. Zikaletwa na akafungua Moja na kuanza kunywa.
Sijakaa sawa, shoga yake yule kaja Tena na kumnong'oneza Tena sikioni Kisha akarudi mezan kwake na Kuja na sahan tupu na kupakia minofu kadhaa ya mbuzi Kisha akaondoka kurudi kwenye meza yao.
Mi nikapotezea nikaedelea Kupiga wine yangu na Sprite mdg mdg.

Haikuchukua mda Sana, nikabanwa haja ndogo nikaenda chooni. Narudi nakuta amarula imebaki Moja mezani, tatu hazipo na nyama zimeisha. Nikamuuliza mamaJ zimeenda wapi. Akanionyesha kidole pale kwenye meza ya wale mabinti na vijana. Vijana wa kiume nao wanakunywa na kula. Nikamwambia Hii Tabia yako ya kiswahili Sana, sijaipenda.

Akasema Ni rafiki zake, atafanyaje Sasa. Basi nikakaa kimya, nikamuagiza mtu wa jikoni aniletee nyama nyingine niendlee na wine yangu. Hhakukawia sana Nyama nyingine zikaletwa, mamaJ nae nikamuagizia amarula nyingine akaendelea kunywa.

Tukiwa tunaendlea kula na kunywa,
Shoga yake mwngn akaja na glass tupu, kasogeza kiti na kukaa na sisi huku anajichekesha chekesha kisha akisema"Shemej kawine basi kidogo" akisogeza glass ishara ya kwamba nimuwekee.Sikumjibu kitu, Nilimkata jicho Kali akaondoka anajichekesha.

Sasa mpaka MDA huo hasira zishanipanda, nikaona Hapa Bora niondoke TU hata Raha ya bendi siioni, kughasiwa ghasiwa na Hawa watu kama chawa Ni kama wananitoa kwny mood. Basi nikamwita mhudumu na kumwomba anaipe bill yangu, akanambia kwenye vinywaji bill yangu inasoma 215,500. Nikamuuliza kivipi nipe mchanganuo mbona sijatumia sana kiivyo, akasema kajumlisha bill zote mbili meza yetu na ile ya wale mabinti. Nikamwambia sijaja nao hao,hesabu nilivyokunywa tu Hapa vinavyonihusu.

Akasema hivyo vinywaji kaagiza huyu (akimyooshea kidole mamaJ), aisee nikatahamaki sana.

Nikamuuliza mamaJ idhini ya kuagizia watu pombe na umekuja na Mimi umeitoa wapi, bajeti nilitoka nayo nyumban unaijua hiki unachofanya Ni uhuni. Hii bill Ya watu wako utailipa mwnyw. Na tukienda nyumban unipe na Elfu 50 ya mangi. Mamaj aKasema
"kha! Mwanaume unagubu Wewe? Hivi nisipokula Ela yako unataka aile Nani? Nakwambiaje sasa silipi Ela yoyote Mimi, wee ndie mwanaume wangu. Unapaswa kunilipia, siwez kuishi maisha ya shida na Mwanaume wangu upo" huku anacheka.

Nikamkazia sura,
"endelea kujichekesha huo upumbav wako, Hii pesa ya watu wako na ya mangi utazilipa tu"

Akasema
"Hata uniue silipi, Tena hiyo ya mangi ndo usiongelee. silipi ng'oo"

Nikasema "sawa, tutaona"

Mhudumu akawa Kama kahamaki tunavojibizana akasema
"kwaiyo Kaka tunafanyaje, nna wateja wengine wa kuwahudumia"
Nikamwambia "dada nenda kwanza nakuja mwnyw hapo kaunta" akasema "sawa"

Yule dada kaondoka nmebaki nmetulia na mawazo kibao, nafanyaje na mfukoni nilibeba laki TU. Ukiskia mtu mzima kuumbuka Basi ndo leo.
Kuna Akili ikanambia huyu mwanamke ningekua sifahamiki Hii bar, dawa yake ningemtelekezea hii bill you're wamnyooshe ili ashike adabu. Ikabd niende Moja kwa Moja kaunta.

Niko counter nishawalipa cash laki, naulizia uwezekano wa kuwafanyia transfer ya pesa ya 115,500 iliyobaki kupitia nmb mobile ya meneja. Naona kijana wa jikoni nae anakuja,anasema ananidai 51,000 Kama bill ya mbuzi choma kilo 3 na kachumbali ya 6,000. Nikauliza kilo 3 kivipi wkt nmeagiza kilo Mona Mara 2 TU. Akasema Kuna kilo nyingine imeenda kwa wale mashoga zake, kaagiza mamaJ.
Dah! Kichwa kikauma zaidi

Ikabd meneja ajumlishe yote na ikaja total bado nadaiwa 166,500. Akasema nitume jumla 170,000 maana kuitoa Kuna makato. Nikafanya hivyo. Nmemaliza kulipa nataka nimfate mamaJ tuondoke nakuta meza yetu wale mashoga zake wameshahamia kabisa wamekaa wanakunywa na kula. Nikamwambia mama j tuondoke akagoma, eti bado mapema.
Nikamwambia Kama huondoki shaur yako, Mimi naenda zangu kwangu.

Basi nikatoka pale na kuelekea kwny gari, nmewasha gar na kuelekea kwangu ila kifuani nna hasira Sana kwa uhuni ule alionifanyia na kunivurugia bajeti zangu mwanamke huyu. Nimeingiza Gari nmeshuka nmebeba koti nmeingia ndani mpaka chumban. Nmerusha koti kitandani ili nivue nguo, naskia funguo zinalia mfukoni kwenye koti. Nikapekua nikazikuta funguo za mamaJ.

Nikakumbuka huyu mtu hata Simu hajabeba-atanipataje, Hana pesa yoyote pale-ataendaje kwake na hata akifika kwake hawezi fungua mlango-funguo ninazo Mimi, Atalala wapi.

Ikabid nimuage wife kuwa natoka Tena Mara Moja, Kuna fundi wangu nampelekea funguo zake alizisahau kwenye gari yangu kanitext mda huu Yuko nje kwake, tulienda wote saiti pamoja leo mchana. Akasema "sawa".

Nmefika pale bar, nimeingia namkuta na wale shoga zake wanaendelea kunywa. Nikafika Nikamvuta kwa Nguvu na kampeleka kwenye gari na kuondoka nae kumpeleka kwake. Njia nzima analalamika Mimi kumdai ile Elfu 50 ya mangi. Na anatamba kuwa halipi liwalo na liwe. Sikumjibu chochote.

Nmemfikisha kwake, nmemlaza ile naondoka nikaona pesa zake kwenye mkoba zimezagaa Kama tulivyoziacha . Nikaona huyu Tambo zake za kipumbavu hili Deni la mangi anaweza asinilipe kweli na sahivi ametoka kuniingiza loss ya kipumbavu sana na mashoga zake.

Huyu dawa Yake nimkate juu kwa juu ili hii Tabia yake asiirudie tena. Basi kwa haraka haraka hesabu ikaja sisi bill yetu tulotumia na inayonihusu haizidi 120,000 kwa nilivyoagiza mimi.

Na pale bar nmelipa jumla 270,000. Maana Yake 150,000 iliyozidi ndio wametumia wale shoga zake.

Nikaona Ujinga huu,
Nikainyofoa kwenye hela zake,
Afu nikanyofoa na ile 50,000 ya Mangi
Jumla nikawa nimetoa laki 2 kwenye pesa zake. Kisha zilizobaki nikazifunga vizur na kuzirudisha kwenye mkoba wake.

Nmeondoka pale nmefika home,
Ikabidi nimtumie sms nikijua fika akiamka akawasha Simu yake atakutana nayo.
"Kwenye hizo pesa zako,
Nmetoa 200,000 ambapo 150,000 Ni bill walotumia shoga zako bar bila ruhusa yangu na 50,000 Ni deni la jombaa ulotumiwa kama nauli yako"

Kisha nikaoga na kukala zangu usingizi

Cha kushangaza sasa
Nmeamka asbh nmekuta sms zake akilalamika khs laki 2 Nilizomkata akilalamika sana kana kwamba hakustahili kukatwa.

1. Nmemkata 150,000 ya bill walotumia shoga zake maksudi ili kumfundisha nidhamu ya pesa siku nyingine asirudie tabia aliyoionesha pale bar, maana ule Ni uhuni na uswahili na anajua fika pale nmekwenda pale na pesa Kias gani mfukoni.

2. Nmemkata 50,000 ya Deni lake kwa mangi maana tayari ashaonesha uhuni na Nia ya kutolipa pesa ya watu kwa kisingizio Cha kwamba Mimi Ni mpenz wake kwahyo napaswa kumlipia hata madeni mengine yanayoihusu ofisi Yao. Huu Ni upuuzi, Ile safar haikua yangu, ilikua ya ofisi yao.

Lengo jifunze kutenganisha kauli ya niazime na naomba. Ile pesa alisema akopeshwe na sio apewe bure. Kwahiyo nna Haki ya kumdai.

Mahusiano yetu hapo yanapaswa yakae kando kwanza.

3. Kakasirika ananidai Hadi Elfu 10 ya mwaka jana ambayo alininunulia umeme wa nyumbani kwangu tukiwa pamoja Coco Beach baada ya kupokea simu na kuambiwa nyumbani umeme umeisha. Nikaomba aninunulie kwenye Simu.

Wakati huo huo umeme wa nyumbani kwake namnunuliaga Mimi kila siku ya Mungu, yeye kuninunulia tu siku 1 tayari ameshaweka kisirani.

4. Kakasirika ananidai Elfu 5 ya boda mwaka huu January nikiwa kwake nilijisahau MDA wa kazi nikaenda kwake na funguo ya stoo. Dukani inahitajika akasema nisiende kokote akampigia boda wake akaipeleka.

Kumbe aliweka kisirani leo kakasirika kaikumbuka Elfu 5 aliyolipia funguo iende dukan kwangu.
Anasahau alipokua na Gari mafuta ya kwendea kazin kwake nilikua namuwekea Mimi, sahv Hana Gari Ila kila nnapoacha posho na nauli yake huwa namuachia.

5. Anatishia nisiporudisha pesa yake ataniacha. Anajikuta Nani labda?

Hivi Ukiondoa hicho kidudu chake,
Ana kitu gani kingine Cha ziada kuoffer kwenye mahusiano haya zaidi Mimi ndie nnaemgharamia kila kitu?

Au Kuna mtu uko Keshamdanganya kuwa siku nikiachana nae kiuchumi ntafilisika?

Hivi wakuu huyu mwanamke anajitambua kweli?

Ananichukuliaje Mimi, danga lake au?

Mbona najitahidi Sana kumthamini kama mwanamke wangu halafu bado ananichukulia POA poa Sana.

Aisee,
NILICHOAMUA sasa
Ni kumpeleka kijeshi jeshi zaidi,
Hii Pesa nishamkata Deni lake tayari na simrudishii hata Mia mbovu

ASINILETEE UPUMBAVU WAKE, AKIONA HAJARIDHIKA AENDE ZAKE UKO. OVER
Screenshot_20220911-095348.jpg
Screenshot_20220911-095401.jpg
Screenshot_20220911-095430.jpg
Screenshot_20220911-095505.jpg
Screenshot_20220911-095513.jpg
Screenshot_20220911-095556.jpg
Screenshot_20220911-095724.jpg
 
32 Reactions
Reply
Top Bottom